Kuna mengi yaliyojificha nyuma ya uchomaji makanisa Unguja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna mengi yaliyojificha nyuma ya uchomaji makanisa Unguja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, May 31, 2012.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0  Hii issue ya maandamano ya Uamsho, vurugu zilizotokea na uchomaji wa makanisa ina mengi yaliyojificha kuliko tulivyoona na kuamini (au kuaminishwa).

  Kuna wanaoona kuna mikakati ilibuniwa rasmi na kupangwa kimakusudi kwa lengo la kupindisha ajenda ya awali waliokuwa nayo Uamsho ya kuuhoji Muungano au hata kutaka uvunjwe.

  Haijulikani mikakati hii ilifanywa na akina nani lakini kulikuwapo thread moja humu JF siku chache zilizopita ambayo iliondolewa iliyosema kuwa kule Visiwani wengi walikuwa wanaamini kuwa Usalama wa Taifa (UWT) ndiye walipanga mikakati hiyo kwa madhumuni hayo hayo ya kupotezesha lengo halisi la mikakati ya Uamsho.

  Mikakati hii ya UWT kama kweli wao ndiyo walitekeleza itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani dhoruba kali tayari imewaangukia Uamsho kwani hatimaye wamejikuta wanabebeshwa lawama la uchomaji wa makanisa, kitu ambacho wengi katika taasisi hiyo wanaamini kuwa siyo wao waliotenda kitendo hicho, ingawa katika mazingira yalivyokuwa itakuwa vigumu kutohusishwa nayo.

  Tutegemee vyombo vya dola iwapo kweli watawakamata watu wale hasa waliochoma makanisa hayo, na siyo kamata-kamata tu ya holela. Kuna usemi unaosema kwamba Uchomaji wa majengo (yaani arson) ni rahisi sana kutenda lakini ni vigumu sana kuwabaini mhusika/wahusika halisi. (It is easy to commit arson than to detect those responsible).

  Kuna watu wameicheza hii kama Messi. Ni dhoruba ambayo kwa waliokusudia wanaona wamefanikiwa kuizima kabisa mikakati yote ya ajenda ya kuuhoji na/au kuuvunja Muungano kwani hakuna tena huko Unguja atakayeweza kuja na kitu hii – kwani wataambiwa ‘Nyie hamna lolote – ajenda yenu kumbe ni udini tu, na siyo Muungano!”

  Ni hakika watu wa uamsho wamejinasa. Dola imepata sababu kubwa ya kupiga marufuku tena maandamano/harakati zozote kuhusu kuhojiwa Muungano kule Unguja.

  Hii inatokana na ukweli kwamba suala zima la Muungano katika mchakato wa kuandika Katiba mpya limawakalia vibaya sana watawala kwani wameshasema kwamba Muungano usiguswe. Na ugumu mkubwa ulikuwa unatoka Visiwani lakini sasa inaonekana wamefanikiwa kulizima – pengine labda kwa muda tu.

  Sasa hivi Tume ya Katiba inaweza kuingia Visiwani na kufanya kazi bila hofu, pamoja na kwamba kutumika kwake Zanzibar bado ni kitendawili kutokana na sheria iliyoiunda ktk Bunge la Muungano kutothibitishwa na Baraza la Wawakilishi.

   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MKONO WA CCM UPO KWA 100%MAANA HAWAKUBALI KUSHINDWA MUASISI WA WIZI WA KURA MALECELA SASA WAMESHINDWA KUIBA WANAONA WATUMIE WAISLAM WA ZANZIBAR KUWAGAWA WATANZANIA SHAME ON YOU CCM MUNGU ATAWALAANI NA VIZAZI VYENU KWA KUTAKA KUTUTENGANISHA WATZ:violin:
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mmm! Kama kuna kaukweli hivi...ngoja waje wajuzi wa mambo.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Hata mie hayo usemayo yamekuwa yananitatiza sana.
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Wewe ni great thinker.

  umesahau kuongeza na mkakati wa just baad ya masaa 12, kualikwa mabalozi wa canada n US na wengineo na kisha tamko kutolewa naubalozi wa US.

  Kimsingi serikali wameshinda, nimemsikiliza nimesoma maelezo ya shein leo nkajua ndio basi tena.

  Shein anasisitiza watu wasubiri tume ya katiba! lakini haijulikani ni kwa kiasi gani hiyo tume itayachukua hayo maoni na kuyatekeleza.

  Bahati mbaya kuna baadhi ya member humu wameingia katika mtego huu kwa makusudi au kwa bahati mbaya. inasikitisha sana.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa UWT are capable of doing virtually anything under the sun. They can murder (eg Gen Kombe murder) and get away with it. Siwezi shangaa kama itakuwa ni wao!
   
 7. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu wamefanikiwa kwakweli, Inaonyesha ni kweli uchomaji wa makanisa Ulipangwa!
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakika Wapemba wamewezwa. Wamekatwa midomo kuhusu kuhoji Muungano.
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Kama ni serikali itakuwa imefanya hivyo, basi imefanya na kufanikiwa kwa mgongo wa Wazinzibar wajinga!!! Na hapa simtukani mtu........Idadi kubwa ya wale vijana waliokuwa wanaandamana na kuchoma matairi/makanisa si waajiriwa wa TISS.

  Uamsho & Co wamewashindilia watu chuki wakawa kama mafuta ya taa....kinachofuata ni kama kumsukuma mlevi.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Nilishasema hilo suala la uchomaji wa makanisa ni mkakati wa serikali ya CCM.
  Uamsho sio wajinga kiasi hiko hata kama wana chuki na Wakristo lakini wasingeweza kutumia mbinu ya kuchoma makanisa.
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari nilizopata zasema kuna timu maalum ya wataalamu ilitoka Bara kwenda Znz Ijumaa usiku au jumamosi asubuhi na vifaa maalum vya kuchomea makanisa huku wachomaji wakiwa mbali, vifaa vinaitwa flame thowers.

  Ile vurugu na milio ya milipuko ya mabomu ya machozi usiku kucha iliweza kufunika harakati hizi za uchomaji.
   
 12. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  JAMANI HAYA MAMBO YAKO WAZI HAWA VIJANA WAMEANDAMANA SIKU TATU ,NA KANISA WAMECHOMA SIO MARA MOJA,
  • SIKU YA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WAO WAKIWA KWENYE MAANDAMANO KWENDA KWEREKWE WAKACHOMA KARIAKOO AU KUNA UTATA?
  • SIKU YA PILI WAMEWASHA MATAIRI BARABARANI HAO UAMSHO WANAFUKUZWA NA MABOMU WANARUDI ILI KIONGOZI WAO ATOE AU HILO LA KUCHOMA MATAIRI ROAD LINA UTATA?
  • WAKICHOMA MATAIRI MITAA YA KISONGE NAKWEREKWE MCHANA KWEUPE WAKAENDA KUCHOMA KANISA LA MPENDAE TENA WAKIWA WANATOKEA KWEREKWE AU KUNA UTATA?
  • WAKIWA KISONGE WAMEWASHA MATAIRI MAGARI HAYAPITI WANASHINIKIZA KIONGOZI WAO AACHIWE WAKACHOMA MAGARI YA WATU AU KUNA UTATA?
  • MAANDAMANO YAO WALIYOKUWA WANAFANYA KUTOKEA MSIKITINI NA KUSABABISHWA BARABARA KUFUNGWA NALO LINA UTATA KUWA PENGINE WALIOKUWA WANAFUKUZWA NA MABOMU AMBAO HATA KWENYE TV NA MAGAZETI WAMEONEKANA NAO SIO UAMSHO?
  • MIKUTANO YAO WANAYOENDELEA MSIKITINI NA WANAYOENDELEA KUITANGAZA HUKU VIONGOZI WAO WAKISEMA WATAENDELEA NA MIKUTANO NAYO WAMESINGIZIWA?

  hapo kuna nini kisicho wazi ndani ya siku tatu maandamano na kuchoma makanisa kila siku yote hiyo wamesingiziwa?kama sio kikundi cha fujo hiyo kuchoma matairi na vurugu barabarani serikali imedanganya?naombeni majibu
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hizi habari zinazidi kutungua ngoja kwanza niwe msomaji kwanza Mzee Mwanakijiji pita huku utupe mchango wako.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu, ukisoma thread No 11 hapo juu ya Counterpunch yanayoelezwa yanawezekana. UWT walichukulia hasira za vijana hao nao kufanya vitu vyao -- hata kwa siku ngapi. They are capable of doing it!
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Kuna nini kimejificha nyuma ya pazia? Kolimba alipohoji Muungano mambo yalotokea kila mtu anauliza mpaka leo, Jumbe nae alipotaka kugusa babu wa watu kipofu mpaka leo, Komandoo Salmin nae kutaka kubadili zenji nae kapofuka ! na wengine walowahi kuwa huko nyuma kama Almarhum BAbu kila aliejaribu kugusa basi kilichomtokea ni makubwa, hili huenda lina ukweli na kama ni kweli basi tutegemee mengi kule Zanzibar , nina imani kuna linalojificha nyuma ya pazia MUUNGANO UNA NINI?
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Bado ni vigumu kuwatenganisha UAMSHO na uchomaji makanisa kwa sababu zifuatazo
  1. Walishatamka maneno hadharani kuonyesha chuki yao dhidi ya makanisa. Rejea kauli zao kuwa 'kanisa lisiwaingilie mambo yao'
  2. Sio mara ya kwanza kuchomwa makanisa Zanzibar. Ingawa kuho vyuma waliochoma inawezekana hawakuwa UAMSHO (kwa sababu pengine haikuwepo), inamaanisha kuwa kuna watu/makundi ya watu yana chuki dhidi ya ukristo zanzibar. Ni rahisi sana wakajipenyeza ndani ya UAMSHO
  3. Kulikuwa na chance kubwa na nzuri kwa mtu yeyote Zanzibar kuanzisha vuguvugu la kudai 'uhuru' bila kuhusisha dini. Kitendo cha UAMSHO kutumia vikundi nya kidini, maimamu na mihadhara ya kidini kudai Zanzibar yao hakiwatenganishi na UDINI kamwe
  4. UAMSHO wanafanya pia mihadhara ya kiislamu. Kila mtu anafahamu kuwa mihadhara ya kiislamu imejaa matusi na kebehi dhidi ya UKRISTO. Watu wengi wanazisikia cassettes za kutoka kwenye mihadhara zinavyotunaka UKRISTO. hakuna jambo jingine zaidi ya chuki za kidini linaloweza kumhamasisha mtu kutukana dini ya mwenzake


  JUMIKI wanahusika, na hawawezi kupinga hilo kuwa hawajachoma makanisa...
   
 17. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono 100% sasa wameumbuka jamani! watu wameanza kuujua ukweli! ipo siku Mwenye ez Mungu atalipa hakika! dhulma wanayoifanya ni kubwa na hasira za Mwenye ez Mungu siku moja zitawaangamiza wote wanaotumia muungano kukandamiza na kuua watu !
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hata vile vipeperushi dhidi ya Wabara kuhama etc inawezekana pia ni UWT. Lakini kikubwa ni motive. hakika suala la muungano lilikuwa shubiri kwa watawala wa pande mbili za Muungano na walionekana hawana mwanya wa kutokea. Wakabuni kitu hii. They are smart in some ways, lakini inawezekana hii ni short term relief.
   
 19. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Sioni ni kwa vipi UWT wangetumia mbinu dhaifu hivyo kuiangamiza JUMIKI. Tumewaona kwenye vyombo vya habari waandamanaji wa JUMIKI wakichoma matairi barabarani na kuziba barabara. Why should that happen?
   
 20. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa kiasi kikubwa umejibiwa na Mkomatembo (post No 15). Kumbuka kwamba Muungano ni 'no go area' in so far as CCM govt is concerned. Ni kitu ambacho wanapatia uhalali kuendelea kutawala (kwa fikra zao) na ni kitu ambacho CCM wanategemea sana kitawaokoa mwaka 2015. Kuvunja Muungano ni kitu ambacho CCM haina compromise kabisa!
   
Loading...