Zegota
JF-Expert Member
- Jun 5, 2020
- 274
- 584
Nilikuwa na mahusiano ya mda mrefu na binti mmoja tangu tukiwa masomoni kiasi kwamba mpaka ndugu na wazazi wa pande zote wakayafahamu mahusiano yetu.
Tuliendelea kuwa pamoja hata wakati ambapo tulikuwa tumemaliza masomo yetu ya elimu ya juu. Tuliishi wote nikiwa nimepanga baada ya kupata kidogo sapoti ya wazazi nikawa napambana na maisha ya kitaa nikijua Niko mtu ambae ni mwenza sahihi kwangu.
Huyu binti alipatq ujauzito na vipimo vilithibitisha hivo, akaomba kurudi kwao nikamruhusu. Nikabaki mjini napambana ninachopata namtumia kumsapoti kutunza mimba, alivojifungua ikabidi kama miezi minne hivi Mimi na binamu yangu tukasifiri kwenda kuona mtoto, tulipofika kimuonekano yule mtoto najiona Mimi kabisa kwa ule mfanano lakini baada ya maongezi ya mda mrefu na kutoa zawadi tulizopeleka, Binti akiwa na macho makavu kabisa tukiwa wa3, Mimi, yeye na binamu akinambia "nashukuru kwa sapoti Yako kwa kipindi chote ambacho tuko wote, lakini niombe samahani kukuambia kuwa huyu mtoto sio wako" na kadi nikapewa likionesha baba yake sio Mimi. Hapa naambiwa maneno haya Niko kwao tena nikiwa na binamu yangu
Sikuwa na jinsi zaidi ya kujikaza kiume kama vile hakuna kitu kilichotokea, baadae tukaaga tukaondoka, tulivyorudi nikawaeleza wazazi yote yaliyotokea wakanipa ushauri wao na maisha mapya yakaendelea.
Baada ya Miaka 3 kupita, maisha yangu yamebadilika kwa kiasi kubwa sana tofauti na mwanzo ambavyo nilikuwa Sina kazi, napokea simu kutoka kwa huyu binti wiki iliyopita, Akisema " Yule mtoto ni wangu na yeye ananipa taarifa tu nijue tu Ile ni damu yangu suala la kumhudumia yeye Hana shida nalo nikiamua nihudumie nisipoamua niache na kwamba kipindi kile alisema vile kwa kuwa sikuwa na uwezo wa kumhudumia hivyo kulikuwa na mtu ampa sapoti ya kutosha"
Ukimwangalia mtoto ni Mimi kabisa Wala siwezi kukataa hilo, kwa Sasa huyu nadhani kibosile wake aliyekuwa anampa jeuri hayuko nae tena anataka kurudisha mpira kwangu.
Pamoja kwamba alidai hahitaji sapoti kwangu amekuwa msumbufu sana mpaka kwa ndugu