Kuna mbegu nimenunua eti inasafisha tumbo na kuondoa sumu, bado sijaitumia nataka ushauri kwanza

Hiyo ni mbegu ya MIBONO ni kweli ukila utaharisha sana.Lakini swala la kuwa dawa inasafisha tumbo halina ushahadi.Mtu anapoharisha mara nyingi anaharisha vitu ambavyo amekula.Sasa angalia mtu kala mayai asubuhi saa 4 kala nyama mchana kala ugali na bamia na jioni kala pilau halafu kalala kesho anaanza kuharisha.

Hivi huo mkorogo aliokula kama ungewekwa kwenye chombo kimoja ukiuangalia unaweza kuukimbia kwa jinsi unavyotisha.Sasa hawa jamaa wa tiba mbadala wanaweza kujenga hoja za uongo kuwa dawa inasafisha tumbo kwa vile mhusika amehara uchafu. Usitegemee mtu kuhara manukato hata kama alikula biryani.
 
Sitasahau siku nimepita jion ubungo nikakuta watu wanauza hizo dawa za kusafisha tumbo nikanunua then asubuhi nikamix yote kwenye soup nikagonga.

Nikaingia kwenye bus tayari kwa safari ya kuelekea Iringa Laahaula kufika maili moja blow down valves zikaanza kutuma signal na konda ananiambia hasimami... Sitasahau ile siku kwakweli.
 
Inaitwa Habbat Mulk,nilishawahi kuitumia miaka5 iliyopita,niliharisha vitu vya ajabu ajabu Sana,yani nililuwa natoa kama ukoko mweusi hivi wakati Ata "fegi" sijawahi piga!!na kumbuka kwamba dawa hii ni ya ajabu ukisema upige usingizi haisumbui,but ukifanya movument yoyote ndio utasikia habari yake,make sure hutoki home siku hiyo na uandae maji mengi ya kunywa na ugali dona wa kutosha sana!
 
Hiyo Mbegu ni nzuri kwan ukishaimeza baada ya dakika 15 ivi utaanza kuharisha yan utaendesha na utatoa uchafu wote then utaarisha mucus km majimaji au makamasi ivi hadi tumbo linakua safi kabisa....Haina tatizo lolote mie binafsi nshaitumia japo itabidi km masaa mawili uwe nyumbani na itapendeza zaidi km ukiwa na choo cha ndani....NB wajawazito sio vizur kuitumia
 
Andika jina la mbegu hiyo tukusiadie, si vizuri kununua dawa za kieanyeji bila kufahamu miti iliyotumika kutenveneza sawa hizo.
 
Ipo kama harage hv ? . Nliwahi inunua kwa wamasai Dodoma nljutaaa maana niliharisha mpaka nkaishiwa maji nlkimbizwa hospital ya Chuo.
 
Inaitwa Habbat Mulk,nilishawahi kuitumia miaka5 iliyopita,niliharisha vitu vya ajabu ajabu Sana,yani nililuwa natoa kama ukoko mweusi hivi wakati Ata "fegi" sijawahi piga!!na kumbuka kwamba dawa hii ni ya ajabu ukisema upige usingizi haisumbui,but ukifanya movument yoyote ndio utasikia habari yake,make sure hutoki home siku hiyo na uandae maji mengi ya kunywa na ugali dona wa kutosha sana!

Muda sahihi wa kuitumia hiyo 'Habbat Mulk' ni muda gani, asubuhi? au hata usiku baada ya kula?

-Kaveli-
 
Muda sahihi wa kuitumia hiyo 'Habbat Mulk' ni muda gani, asubuhi? au hata usiku baada ya kula?

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom