Kuna matatizo makubwa ya umeme PSPF Plaza Dodoma

Zamazamani

JF-Expert Member
Jun 13, 2008
1,859
763
Wadau

Naendelea kushangaa kwa huu uwekezaji wa jengo la PSPF PLAZA hapa Dodoma kwani pamoja na jengo kuonekana la kisasa na kuvutia lakini hakuna umeme wa uhakika

Ni ajabu kwa kweli kwa zama hizi kufanya uwekezaji kama huu halafu suala la standby power likapuuzwa. Sasa hivi karibia wiki nzima hakuna lift inayofanya kazi, tunapanda kwa ngazi...hivyo tunapigana vikumbo na Mawaziri na viongozi wengine kwenye ngazi sasa fikiria Waziri na viongozi wengine anapanda gorofa ya kumi na moja kila siku kwa ngazi...

Hivi ninavyoongea umeme umekatika zaidi ya mara tatu ….Yaani sasa watu walitegemea kwa usasa wa jengo hili umeme utakuwa si tatizo hivyo wengi hawana UPS kumbe ni majanga matupu sasa….

Jamani kama kuna wahusika tunaomba mtuokoe kwenye hili janga ..maana yake kero zimekuwa tooo much!!!
 
Back
Top Bottom