Kuna maswali Rais Magufuli alitamani kuulizwa

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Novemba 4, mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli, alifanya mazungumzo na waandishi wa habari katika sura ya mahojiano, Ikulu, Dar es Salaam.

Jinsi Rais Magufuli alivyojibu maswali, inaonesha kuwa maswali mengi yaliyoulizwa hakuyatarijia. Namna alivyokuwa anarukia ufafanuzi mrefu unaotofautiana na maswali aliyoulizwa, ilionesha wazi kuwa yapo maswali alitamani kuulizwa.

Mathalan, swali lililoulizwa na mtangazaji wa kujitegemea, Pascal Mayalla, kuhusu mgawanyiko wa mihimili ya dola, kwamba kila mmoja unapaswa kuheshimu mwenzake bila kuuingilia, kwamba Rais Magufuli amekuwa akiingilia mihimili mingine, lilijibiwa ndivyo sivyo.

Swali hilo ni wazi liliulizwa nje ya matarajio ya Rais Magufuli. Jawabu lake kuwa Serikali ndiyo inayotoa fedha za kuendesha bunge na mahakama, akitumia maneno kuwa mhimili Serikali umechimbiwa chini zaidi, lilienda kinyume na dhana nzima ya mgawanyiko wa mihimili mitatu na lilitia ukakasi misingi ya utawala wa sheria.

Suala la Serikali kutoa fedha ni sehemu ya mgawanyo wa majukumu ya mihimili hiyo mitatu, Serikali, Bunge na Mahakama. Serikali ndiyo inayokusanya mapato ya nchi. Bunge na Mahakama haikusanyi mapato.

Katika mirathi, mtoto mmoja akiteulizwa kuwa msimamizi haimaanishi kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka makubwa zaidi, kwa hiyo anaweza kuwapangia hata ndugu zake namna ya kuishi.

Serikali ina wajibu wa kulipa Bunge fedha, vilevile Mahakama kwa sababu za kimajukumu. Ni kama ambavyo Serikali haitungi sheria wala haitafsiri sheria, yenyewe inatekeleza kama ilivyotungwa au kama ilivyotafsiriwa. Majukumu hayo mawili ya utunzi na kutafsiri sheria yanafanywa na Bunge na Mahakama.

Katika mihimili hiyo mitatu, Serikali imepewa mamlaka ya kusimamia rasilimali za nchi. Jinsi rasilimali zinavyotumika vizuri na kuipa nchi mapato. Serikali inasimamia shughuli zote za kiuchumi kwenye nchi. Kila kinachopatikana kinaingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali, yaani Hazina.

Bunge mbali ya kutunga sheria, jukumu lake lingine ni kuisimamia Serikali namna inavyoendesha mambo yake, inavyofanya usimamizi wa rasilimali za umma. Inavyokusanya mapato na jinsi inavyotoa huduma kwa wananchi.

Mahakama pamoja na kazi ya kutafsiri sheria, yenyewe ndiyo kituo kikuu cha utoaji haki kwenye nchi. Utaona kuwa kila mhimili una unyeti wake. Aina ya majukumu yaliyopo kwenye mhimili mmoja, hayafanyi kuonekana ni mkubwa kuliko mwingine.

Swali lingine la Mayalla kuwa Rais Magufuli alitumia kifungu kipi cha Katiba kufungia shughuli za kisiasa mpaka mwaka 2020 halikujibiwa kabisa. Hapa ni kuonesha kuwa swali hilo halikuwa kwenye matarajio ya kiongozi huyo.

Maswali mengi alipishana nayo

Lipo swali lililoulizwa kwa Kiingereza na mtangazaji wa BBC kuwa Rais Magufuli amekuwa akitumia kigezo cha kuleta maendeleo kuminya demokrasia, alijibu hajawahi kuminya demokrasia kisha akatolea mfano wa mgogoro Chama cha Wananchi (Cuf), japo hakutaja jina.

Mmoja wa waongoza mahojiano hayo, Tido Mhando akachomekea hapo kuwa jinsi anavyoongoza imekuwa ikikosolewa kuwa analeta udikteta, Rais Magufuli akajibu: “Udikteta ni mtazamo, hata wewe ulikuwa BBC, ukahamia TBC, sasa hivi upo Azam, watu wanaweza kusema huko unakohamahama kuna udikteta.”

Rais Magufuli alisahau kusema kuwa Tido alikuwa Mwananchi Communication kabla hajahamia Azam Media. Alisema: “Shughuli za vyama zinaendelea, mbona kuna chama kimoja kilifanya uchaguzi wakaanza kugombana wao kwa wao, hiyo ndiyo demokrasia.”

Swali kuhusu kubana matumizi sehemu nyingine ili kujielekeza kununua dawa, Rais Magufuli hakukonga moyo, maana alisema Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa na bajeti kubwa ya dawa kuliko awamu zilizopita.

Hoja hapa ni dawa kutosheleza, siyo ukubwa wa bajeti. Unaweza kuwa na bajeti kubwa lakini isitosheleze mahitaji ya wakati. Vilevile bajeti inaweza kuwa kubwa lakini fedha kutoka ikawa tatizo au zisiwepo kabisa, matokeo yake dawa zikawa hazinunuliwi na uhaba ukawepo kama yalivyo malalamiko ya sasa.

Swali kuhusu Katiba Mpya ndiyo hakuacha kuweka hisia zake wazi kwa kumwambia Tido kuwa ana maswali ya kichokozi. Akasema yeye kwenye kampeni zake hakuwahi kuzungumzia Katiba, kwa hiyo akataka aachwe ili anyooshe nchi kwanza.

Rais Magufuli angejiandaa kwa swali hilo bila shaka angelitolea majibu yenye kutosheleza. Kusema aachwe anyooshe kwanza nchi ni kama vile hatambui kuwa kama taifa, gharama ya Katiba Mpya ni kubwa na iliachwa kiporo.

Bunge la Katiba lilishapitisha Katiba Inayopendekezwa mwaka 2014, kwa hiyo kilichokuwa kimebaki ni kura za maoni, ili wananchi waikubali au waikatae. Angalau hapo shughuli itakuwa imefikishwa kileleni.

Umebadilika utawala lakini Serikali ni ileile, Katiba Inayopendekezwa ilishakabidhiwa serikalini na aliyekuwa Spika wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta. Haifai baada ya kuingia kiongozi mpya ndiyo michakato ya ungozi uliopitwa izikwe jumla. Hiyo siyo sawa.

Rais Magufuli anayo nafasi moja kati ya mbili, ama kuitisha tena Bunge la Katiba ili kutii malalamiko yaliyopo kuwa bunge lililopita lilisigina rasimu ya Tume ya Katiba au kuacha kura za maoni zichukue nafasi ili wananchi wenyewe waamue kama ni kuikubali au kuikataa. Siyo kusema aachwe anyooshe nchi wakati Katiba na yenyewe inahitaji unyoofu ili aweze kuongoza vizuri.

Yapo maswali alijiandaa kujibu

Rais Magufuli alitaka aulizwe kuhusu majipu aliyotumbua. Aeleze kinaubaga kuhusu wale aliotengua uteuzi wao na masuala yote kuhusu watumishi hewa. Alihitaji mno swali kuhusu nidhamu ya utumishi wa umma namna ambavyo ameweza kuirejesha katika mwaka wake wa kwanza Ikulu.

Utumbuaji wa majipu na suala la wanafunzi wa diploma maalum ya ualimu wa sayansi, waliokuwa wanasoma Udom, aliyazungumza kwa ufasaha katika maswali ambayo yalihusu masuala mengine.

Suala la mahakama ya mafisadi lilikuwa na majibu ya kutosha. Kimsingi mahojiano ya Dk Magufuli na waandishi wa habari kuzungumzia tathmini ya mwaka wake mmoja Ikulu, yamembakisha Rais Magufuli yuleyule wa tangu alipoingia madarakani.

Rais Magufuli ni yuleyule wa kulalamikia uozo ambao anasema ameukuta serikalini. Katika eneo hilo anaziba mdomo watu wasihoji kwa kueleza kuwa yeye yupo ndani ya Serikali, kwa hiyo anaona kuliko waliopo nje.

Ni yuleyule wa kulalamikia meli kutia nanga Bandari ya Dar es Salaam na kuondoka bila kulipiwa kodi. Tofauti ya nyakati zilizopita na sasa ni kuwa angalau katika mahojiano hayo alisema mpaka idadi, kwamba meli 60 zilikuwa zinafika bandarini, kila moja ikiwa na makontena yasiyopungua 3,000, lakini yote yanashushwa bila kulipiwa kodi.

Kilio chake ni kilekile kwamba kuna watu waliigeuza Tanzania pepo ya kufanyia ufisadi, kwamba wapo watu ambao ilifikia hatua wakatengeneza mazingira, badala ya kulipa kodi, wao ndiyo wakawa wanaidai Serikali kodi na wanalipwa.

Eneo la namna ambavyo ameweza kutumbua majipu ndani ya mwaka wake wa kwanza, lilikosa maswali ya kutosha na kwa sababu alipenda kulizungumzia, alilazimika kutoa ufafanuzi kila alipoulizwa swali ambalo aliona linakaribiana na masuala ya utumbuaji majibu.

Hakujipamba inavyotakiwa

Suala la kutamka kuwa meli 60 zilitia nanga bandarini na kushusha makontena bila kulipiwa ushuri ni sawa, ila angejipamba vizuri zaidi kama angeweza kutamka moja kati ya mambo mawili; mosi, mapato ya sasa bandarini yameongezeka au pili, mapato ni yaleyale.

Dhana iliyopo sasa ni kuwa mapato yamepungua kwa kiasi kikubwa bandarini. Hoja kuwa meli zilikuwa hazilipi kodi, inatakiwa kubebwa na utetezi kuwa kipindi kile meli nyingi lakini sasa hivi meli chache lakini mapato yameongezeka au yamebaki yaleyale.

Hapo inakuwa na uthibitisho kwamba kweli wakwepa kodi wamedhibitiwa, hivyo wamekimbia na meli zao, wale waliokuwa wakifanya biashara safi meli zao zinaendelea kuweka nanga ndiyo maana mapato yamebaki yaleyale au yameongezeka.

Suala watumishi hewa kudhibitiwa lakini gharama za Serikali katika kuhudumia mishahara zimeongezeka kwa Sh78 bilioni kwa mwezi, ambalo lilianzia bungeni kwa hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, Dk Magufuli hakulitolea ufafanuzi mzuri, aliliacha lielee kana kwamba ni hoja ya kisiasa tu.

Kuhusu Tanzania ya Viwanda, hili ni eneo ambalo Rais Magufuli alipaswa kulizungumzia kwa wigo mpana kwa sababu ndiyo alama ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa jinsi alivyofanya kampeni na alivyojinasibu baada ya kushinda.

Angeweza kujipamba kuhusu hatua ambazo ameshapiga kuijenga Tanzania ya Viwanda, vilevile mikakati yake katika miaka yake minne iliyosalia kwenye huu muhula wake wa kwanza. Swali liliulizwa lakini hakulinakshi jawabu lake kama ilivyokuwa kwenye utumbuaji wa majipu

Chanzo: Maandishi Genius
 
Hongera kwa ufafanuzi wako na rejea ya mkutano wa Rais wa 4 November 2016 na Wahariri ukumbi ws Ikulu.

Ushauri wangu kwako mtoa mada pamoja na kuiweka mada JF lakini itume Ikulu kama reference kupitia kitengo cha mawasiliano maana mada yako ina mambo muhimu kwa Rais inpersonal.

Rais alitoa ufafanuzi wa maswali mengi yaliyoulizwa na Wahariri kwa kadri ya ilivyowezekana.

Na siyo majibu yote yatawafurahisha watu wote kwani Rais mwenyewe amesema yupo ktk vita ya kimaslahi ktk sehemu kubwa na yeye anapambana kuhakikisha nchi inarudi ktk mstari wake.

'Let's give him time and support for his effort'
 
huwezi kuweka nchi sawa wakati Polisi ni corrupt huwezi kuweka nchi sawa wakati jeshi ni corrupt huwezi kuweka nchi sawa wakati mahakama ni corrupt huwezi kuweka nchi sawa wakati taasisi zote ni corrupt hivyo nikusema kama wewe unataka kuwa dikteta tu maana yoote hayo source ni tume ya uchaguzi bila kuweka sawa tume ya uchaguzi huna kuweka sawa zaidi ya kuendeleza ama udiktaka au zaidi ni corruption ivi utashindaje uchaguzi kama tume ya uchaguzi sio corrupt au ndio utafuta uchuguzi mpaka nchi iwe total ni ccm
 
Jaji wa mahakama kuu anateuliwa na rais.
Spika anateuliwa kutokana na mapendekezo ya kamati kuu ya chama tawala ambacho mwenyekiti wake ndiye rais.
Halafu hapo hapo mnasema hii mihimili ipo sawa .
Serikali inakusanya fedha halafu inapeleka mapendekezo ya bajeti za mihimili mingine inapanga tu hawa tuwape hiki wale tuwape hiki bunge likileta fyoko fyoko rais anaweza kulivunja.
Hii mihimili ipo sawa kwenye katiba tu ila kiuhalisia haipo sawa.
 
Back
Top Bottom