Kuna Manufaa Kitaifa Tundu Lissu na Rais Samia kukutana?

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Moja ya mambo ya kipaumbele wakati rais Samia Suluhu anaapishwa kushika madaraka ilikua ni kudumisha umoja wa kitaifa.

Ingawaje baada ya muda matarajio hayo yalikosa Imani kutoka kwa baadhi ya wananchi na wadau wa siasa nchini hasa baada ya mashtaka dhidi ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kufunguliwa kwa tuhuma za ugaidi.

Si hilo tu kitendo cha rais Samia kupiga danadana kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani ilitajwa kuwa moja ya sababu ya kufifia kwa matumaini ya kurudisha umoja ndani ya taifa.

Nataka kusema nini? Kwa namna yoyote ile utakubalina na mimi kuwa hayati Magufuli alifanikiwa katika baadhi ya mambo lakini kwenye hili la Siasa Safi na umoja wa kitaifa alifeli Sana na ndipo utengano huu na siasa chafu ilipoanza.

Magufuli aliwaaminisha viongozi wote wa serikali hasa wale wa chama tawala kuwa wapinzani sio watu wenye nia njema ndani ya taifa hili na sio watu salama kwa kuwachagua au kuambatana nao kwa namna yoyote ile.

Unakumbuka baada ya Tundu Lissu kupigwa risasi, Lazaro Nyarandu akiwa mbunge alimtembelea Lissu hospital Kule Nairobi nini kilifuata?

Unakumbuka zile kauli za Magufuli kuwa penye kiongozi wa upinzani sileti maendeleo?

Huu ni mzizi ulio pandwa na kupaliliwa ndani ya miaka mitano Rais Samia ana deni la kuung'oa na kupanda mti wa neema ambao kivuli chake kitakuwa na manufaa kwa wote.

Licha ya kwamba muda umeenda yakaribia mwaka Sasa tangu Samia atoe kauli ya kuliponya taifa bado ana nafasi ya kufanya mengi yenye manufaa kama hili la kukutana na makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu huko Brussels nchini ubelgiji.

Baadhi ya watu wanachukulia kitendo hiki kuwa cha kwaida na hakina manufaa kwa taifa.

Je watu hawa wanajua nguvu ya siasa na wanasiasa kwa ujumla au wanasema ili kufurahisha nafsi zao?

Ngoja nikupe mchapo kidogo hivi karibuni mwaka 2018 pale nchini Kenya kwa majirani lilitokea jambo.

Kwa mara ya kwanza rais wa Kenya Uhuru Kenyetta na aliyekuwa kiongozi wa chama cha ODM na Waziri mkuu mstaafu Raila Odinga walikutana ikiwa ni muda mrefu tangu machafuko ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Baada ya kukutana hadharani na kusalimiana Odinga na Uhuru walifanya mazungumzo kisha kupanga safari ya kikazi kwenda china kisha ulaya.

Mkutano huu ulitazamwa kwa sura mbili, sura ya kwanza Makamu wa rais William Ruto na wafuasi wake waliona kitendo kile ni usaliti na sura ya pili wakenya walishangilia kwa kuona kile kitendo ni kudumisha upendo na utaifa.

Kwanini Ruto na wafuasi wake hwakupenda, ilikua ni mawazo yao kuwa watakufa kisiasa kwakua ulikwepo mpango kuwa Uhuru akitoka madarakani basi ampambanie Ruto aingie.

Kwahiyo maslahi binafsi ya kisiasa ndiyo yaliyo wapa hofu wafuasi wa Ruto na sio maslahi kwa taifa la Kenya.
Tuachane na hayo je bado kuna mtu anahoji manufaa ya mkutano huu wa rais na mwananchi wake ambaye ni mhanga dhidi ya taifa lake?

Kwa mujibu wa Lissu mwenyewe baada ya mkutano huu mambo mbalimbali yanaweza kutokea kama vile Lissu kurudi nchini iwapo atahakikishiwa Usalama, weje na Lema kurudi nchini kwa hali hiyohiyo, kuangalia mambo mbalimbali ya kitaifa ikiwemo suala la Mgogoro wa uhalali wale wabunge 19 ndani ya bunge na mambo mengine.

Mtu anae pinga maslahi ya mkutano huu aje na hoja zenye mashiko zisizo endana na ile simulizi ya Ruto na wafuasi wake pale nchini Kenya.

Mimi Binafsi ntakuwa mtu wa mwisho kusema ule mkutano haukuwa wa manufaa.
Kwa hisani ya Mtandao.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa na jamii.

IMG-20220216-WA0006.jpg
 
Siasa zetu huwa siyo za kushabikia matokeo ya on the spot, you needs wait to catch the product.

Vinginevyo yatakuwa sawa na yale au haya ya anaupiga mwingi. Never trust politicians at any word.
 
Jibu ni ndiyo. Siasa siyo uadui! Tulizoe kuona wanasiasa wakishindana kwa hoja! Ila kuanzia 2017, mambo yalibadilika kabisa!

Ni vizuri tukarudi kwenye utaratibu wetu wa zamani. Ubaguzi, ubinafsi, na utengano wa aina yoyote ile! Hauwezi kutusaidia chochote.
 
Sasa hapa ana tofauti gani na Zito aliyeenda kwenye kikao kuomba Mbowe aachiwe?

Tulishasema siku nyingi huyu jamaa ni mbinafisi sana, akifanya yeye sawa ila wakifanya wengine kosa
Zitto alitumwa na nani?
Kama Mbowe na chama chake hawakutaka kuwepo kwenye ule mkutano wa kimichongo kati ya vyama vya kiCCM na Rais Samia, Zitto alienda kuwasemea wakina nani?
 
Kuna faida ya kuoga? Naandika page 4, alafu najiita mchambuzi blah blah blah. Rubbish
 
Back
Top Bottom