Kuna maneno ya kiswahiki yananitatiza wanalugha nisaidieni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna maneno ya kiswahiki yananitatiza wanalugha nisaidieni

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by mbelege, May 11, 2012.

 1. m

  mbelege Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wataalamu wa lugha ya kiswahili naombeni mnisaidie. Kuna baadhi ya m,aneno katika lgha ya yanapotamkwa mzungumzaji hutakiwa kuanza na ashakum, hasa kwa maneno ambayo yanaweza kudhaniwa kuwa ni matusi.(yaani mzungumzaji huanza kwa kusema ashakum si matusi), Sasa sijui ni kukua kwa lugha au ni nini kwa sababu siku hizi maneno mengi ambayo hapo mwanzo yalionekana kuwa ni ya kawaida lakini kwa yanaonekana kuwa ni matusi, hivyo naomba msaada kuwa je kuna haja ya kutumia ashakum kwa maneno kama; kuchomeka, kuingiza, kutoa,chomoa, panua, sugua, tanua,tao, chapa, gonga. Kwani maneno haya ninapoyatumia nashangaa watu hunielewa tofauti.Nisaidieni wataalamu wa kiswahili.
   
 2. tabibumtaratibu

  tabibumtaratibu JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 2,297
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  Haina haja coz maneno hayo ni ya kawaida sana ila wa2 wanafikiria vbaya.
  Nawasilisha
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hayo maneno mbona yakawaida sana makuu na nimazuri tuu!
  kama utaomba msamaha kwa hayo sema utaweka maneno gani badala yake!
   
 4. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wewe Mbelege ninahisi umri wako ndio tatizo katika matumizi ya maneno uliyayataja. Maana ninaambiwa ninyi vijana wadogo ni mabingwa wa kubadili matumizi ya maneno ya kawaida kwa lengo la kupiga chuku hasa katika mazingira ambamo mnahisi mnahitaji faragha ya peke yenu. Sasa hayo usituulize sisi. Sana sana nikukumbushe tu kwamba hizo maana mlizozipindisha katika maneno yote uliyoyataja, hazifahamiki kwa jamii pana ya watumiaji wa lugha. Maneno hayo yasemwapo mbele ya mmilisi wa lugha awaye yote hutaona panaleta maana ya kukera.
   
 5. r

  rununu Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa maneno hayo sioni ubaya wowote ila tu watu wamepanua maana na maana zipo katika fikra zao tu, wala hakuna ubaya wowote, ashakum/hashakum maana yake ni, "niwie radhi kwa nitakayosema"
   
Loading...