Kuna mambo mengine hadi unawaza kama kweli tu binadamu tuliokamilika

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,627
Hivi kweli ni akili kumuona dada yako, shangazi yako, mama yako mzazi, mke au girlfriend wako akijiunga kwenye kikundi cha kulia misibani na ukaridhika kabisa kuwa ni moja ya kazi!?

Inasikitisha sana

FB_IMG_1564053792667.jpeg
 
Ng'wanapagi, Unapaswa kutambanua kuwa kila kazi inawenyewe, hivi wewe unaweza furahi kumuona baba, kaka au Mjomba anazibua mitaro ya Choo au maji machafu?.

Kila kitu kinanafasi katika Maisha, unapoona kunavikundi vya burudani ni sawa pia kuwa na vikundi nya huzuni na maombolezo.
 
Mkuu kazi ni kazi iwapo inampa mtu kipato halali pasipo kuvunja sheria. Bora hao wanaopata pesa kwa kazi ya kulia misibani kuliko wale wanaopata pesa kwa kuiba pesa za walipa kodi masikini kabisa.

By the way kazi ya kulia misibani ni kazi ngumu sana maana inahitaji watu wenye ujasili na hisia kali mbele ya umati wa watu.

OMBI LANGU: Kazi hii iwe kazi rasmi na wahusika wapewe vitambulisho vya ujasiliamali ili waanze kulipa kodi maana ni kazi halali kabisa isiyoovunja sheria za Nchi .
 
Hivi kweli ni akili kumuona dada yako, shangazi yako, mama yako mzazi, mke au girlfriend wako akijiunga kwenye kikundi cha kulia misibani na ukaridhika kabisa kuwa ni moja ya kazi!?

Inasikitisha sana

View attachment 1260867
Inasikitisha tena sana kwani ni unafiki na uchuro. Ni bora kumzika marehemu kimya kimya kuliko kujifanyisha kuhuzunika kwa mikelele hiyo.
 
Kwa hiyo watu wakilia sana, ndio inachukuliwa kuwa msiba ulifana?
 
Mhhh hapana ndugu
Mkuu kazi ni kazi iwapo inampa mtu kipato halali pasipo kuvunja sheria. Bora hao wanaopata pesa kwa kazi ya kulia misibani kuliko wale wanaopata pesa kwa kuiba pesa za walipa kodi masikini kabisa.

By the way kazi ya kulia misibani ni kazi ngumu sana maana inahitaji watu wenye ujasili na hisia kali mbele ya umati wa watu.

OMBI LANGU: Kazi hii iwe kazi rasmi na wahusika wapewe vitambulisho vya ujasiliamali ili waanze kulipa kodi maana ni kazi halali kabisa isiyoovunja sheria za Nchi .
 
hapo ndio only way kaona anaweza mudu kujitafutia maisha. Kama wew ulivyoona kazi yako ufanyayo ndio unaimudu.

Kuna wengine, wanaongelea vibaya kazi za ndugu zao huku hata kuwapa sh.1000, hawawezi.
 
Back
Top Bottom