Kuna mambo katika kuongoza Taifa hayafanyiwi majaribio, ukijaribu unajijaribu

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,188
11,219
Unajua ndugu zangu, niwaambie ukweli kabisa yapo mambo unapo ongoza Taifa hupaswi kuyafanyia majaribio au mzaha maana mambo hayo ukiyafanyia majaribio au mzaha basi mwisho utajitekenya mwenyewe na kucheka peke yako wakati watu wakikucheka na kukusanifu ndipo unakuja ule msemo "ukipenda kushangiliwa basi usisahahu kuna kuzomewa."

Dunia imebadilika sana kuliko wakati mwingine wowote ule yani kitu unakiona nikidogo sana kina lipuwa taifa zima mpaka unashangaa how come mbona imekuwa hivi? Kama kuna wakati watawala wanapaswa kuwa makini na maamuzi na kauli zao basi nikatika zama hizi za sasa.

Hongereni sana viongozi mnao kimbia kamera nakufanya kazi zenu kwa weledi maana siku zinakuja kamera hizi na picha hizi mnaona zina wapaisha kwa mkuu mtatamani zisingechukuliwa wala kuonwa maana zimekuwa kovu na huzuni ktk kazi zenu na hata muktadha wa safari yenu ya kiuongozi. Watanzania wanyonge wanawasubiri siku nao wawaulize kama mlisoma sheria au laa? Itakuwa siku ngumu sana kwenu.

Yapo mambo kama kiongozi hupaswi kujaribu kamwe ktk historia haya mambo hayajaribiwi uwa yanaongozwa na sera na sheria zilizopo.

Katiba huu ni msaafu tena msaafu wenye muongozo wakuwaongoza wanan nchi. Ukicheza na katiba una cheza na bomu kwenye sehem ya moto yani kulipukiwa asilimia ni 99%. Historia inatukumbusha watawala walio cheza na katiba mwisho walichezewa mchezo ule ule walio ucheza ktk katiba yani walijikuta wanajitekenya na kucheka wenyewe. Yani usicheze na katiba wala usije kamwe mshangilia kiongozi anacheza na katiba ya nchi yake nakwambia mnaweza angamia wote kama hatotokea mwerevu nakuwashitua hayo mnayafanya ni hatari kwa ustawi wa taifa.

Uchumi wa taifa lolote ndio nguzo ya kule wanaeleka. Ukichezea uchumi kwa ajili ya sifa na kuonekana wewe ndio kidume wanao kishangilia ndio watakuja kukuzoea. Nenda kamuulize Hayati Mugabe alipo amua kutwaa mashamba ya wa zungu kwa chuki binafsi wakati akijuwa kabisa hawana uwezo wakulima nini kimelikumba taifa umasikini na hasara ambayo watalipa vizazi na vizazi. Nenda hapo Libya Ghadaffi akachukua visima vya mafuta kinguvu kwenye uwekezaji ambao hakutia hata cent mwisho akajifanya anapesa na wananchi mwisho wakamtanguliza mbele ya haki wakikataa mungu mtu. Uchumi hauchezewi wala kujaribiwa.

Uchumi wa taifa ni kama yai hauwongozwi kwa jeshi wala mtutu wa bunduki ila unalindwa na jeshi na vyombo vya usalama wa taifa. Ukiona lugha ya watawala ktk uchumi ni yakibabe na nguvu nyingi ya kijeshi basi juwa taifa hilo linakoelekea inajuwa lenyewe. Mara nyingi ukiushikia uchumi bunduki utakusanya kiasi fulani ila baada ya muda makusanyo yanashuka ghafla why? Uchumi ni sawa na Ng'ombe wa maziwa ili upate maziwa shurti umlishe vizuri umpe pumba na mashudu majani mazuri basi jion unapata maziwa mengi tu. Uchumi wa taifa unalindwa kwa kuweka sera nzuri wawekezaji wazipende na sio hivyo tu kauli za watendaji ziwe na munyu sio vitisho na fedhea mara sijuwi akaunti zimefungwa utegemee mwekezaji huyo atafanya vizuri never on earth.

Wananchi wako ndio mtaji hakuna kitu kibaya kama ku miss treat raia wako. Ambaye ndio nguvu kazi ya taifa . Mwana nchi anahitaji upendo wala niwaambie wananchi hawafurahi kuona mnafukizana kama mbwa hiyo ni dalili ya mismanagement huwez mfukuza mtu like dog as if hukumsomesha na kumuajiri haya yanaleta hofu na kuona serikali yao nikatili isio jali watu wake.

Kauli nzuri kwa unao waongoza nalo sio jambo lakubeza. Kauli za kejeli, ubabe na kujiona mimi ndio mimi mara nyingi zimeziangusha serikali embu ona kauli za Trump zilivyo mkosesha urais awamu ya pili na zinavyo mgarimu kuondolewa madarakan before time. Viongozi tuangalie kauli zetu maana zina weza zuwa jambo.

Respect your citizens.
 
Back
Top Bottom