- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Mbali na sababu za kiimani, Ni kweli kuna bahari ambazo zina maji ya rangi tofauti ndani ya bahari moja na maji hayachangamani japokuwa yanagusana?
- Tunachokijua
- Bahari ni eneo kubwa lenye maji ya chumvi. Kwa maana ya kijiografia bahari yaani maeneo makubwa ya maji ya chumvi ambayo ni kama yanauzunguka uso wa Dunia. Bahari kuu ya dunia inafunika asilimia 71 za uso wa dunia.
Kwa mujibu wa huduma ya taifa ya bahari ya nchini Marekani (National ocean service) inaeleza kuwa Licha ya kuwa dunia kuwa na bahari moja, sehemu ya yenye maji ni asilimia 71 duniani, huku ikiwa imegawanywa kulingana na majina ya maeneo husika. Inaelezwa kuwa mipaka katika maeneo mbalimbali imekuwepo katika vipindi tofauti vya kihistoria, utamaduni, kijiografia na sababu za kisayansi.
Kihistoria zinajulikana bahari nne ambazo ni Antantiki, Pasifiki, Hindi, na Artic hata hivyo nchi nyingi ikiwemo Marekani zinatambua bahari ya Antartic na kufanya bahari hizo kuwa tano.
Kumekuwepo na taarifa na hata picha zinazoonesha kuwa maji ya bahari hutengana na kutokuchangamana, mfano mzuri ambao umekuwa ukitumiwa ni bahari ya Pasifiki na Atlantik
Uhalisia wa jambo hili upo vipi?
JamiiCheck imepitia maandiko mbalimbali ya kisayansi ambapo si kweli kwamba maji ya bahari hayachangamani bali huchangamana taratibu kwa namna isiyoonekana kwa wepesi, Kwa mujibu wa tovuti ya Geologyin Maji ya Bahari ya Pasifik na Atlantik ambazo hazikutanishwi kwa mpaka wa moja kwa moja unaoonekana lakini ni sehemu ya muendelezo wa maji ya bahari ambayo maji yake huchanganyikana lakini si kwa urahisi kutokana na sifa zinazotofautiana mfano joto la maji, kiwango cha chumvi pamoja na hali ya maji kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.
Kwa mujibu wa tovuti ya MariTimes post Bahari ya Pasifiki kwa kawaida ina joto zaidi na ina chumvi kidogo kuliko Bahari ya Atlantiki. Hii ni kwa sababu Bahari ya Pasifiki inapokea mwanga wa jua zaidi na ina kiwango kidogo cha uvukizi kuliko Bahari ya Atlantiki. Tofauti katika joto na chumvi kati ya bahari hizi inaunda kizuizi ambacho kinazuia maji yake kuchanganyika kwa urahisi.
Utofauti wa ‘density’, joto, na chumvi, katika pande mbili za bahari unasababisha maji hayo kutokuchanganyika kwa urahisi, ambapo Hii ni zaidi kwenye tabaka la juu la bahari, ambapo utofauti katika ‘density’ ni mkubwa zaidi.
Aidha, sababu zinazowezesha maji ya bahari kuchanganyika ni pamoja na mawimbi, upepo na mkupwa na kujaa kwa maji baharini kunakosaidia maji kujichanganya mpaka maji yaliyo kina kirefu zaidi.