Kuna maisha baada ya uchaguzi kupita, tuwekeni akiba ya maneno na vitendo

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,289
12,582
Hata iweje maisha yataendelea baada uchaguzi kumalizika na bila kujali matokeo ya Uchaguzi yatakuwaje.

Wadau wote wa uchaguzi, yaani Wanasiasa, wagombea, ofisi ya msajili, Tume ya Uchaguzi, Askari, wasimamizi wa uchaguzi, wahesabu kura, mawakala na wapigakura tukumbuke muda wote kuweka akiba ya maneno na vitendo vyetu ili vitusaidie kuendelea na maisha baada ya uchaguzi kumalizika. Miaka 5 ya baada ya uchaguzi Ni mingi Sana kuliko muda wa mchakato wa uchaguzi Hadi kutoa matokeo. Kuna kesho nyingi baada ya uchaguzi kuliko wakati wa uchaguzi.

Wahenga wetu kutokana na uzoefu wao wa kuishi kwingi na kuona mengi walikuja na misemo ya "majuto Ni mjukuu, mdomo unaponza kichwa na baada ya kisa mkasa"

Kila mtu anayafahamu maneno na vitendo vya kuudhi, maneno na vitendo visivyovumilika, na maneno na vitendo ambavyo Ni matusi kwa mujibu tamaduni zetu.

Tutumie maneno na vitendo ambavyo vitaibakiza Tanzania ikiwa salama, amani na tulivu.

Haki iwe ndiyo msingi wetu katika hatua ya Uchaguzi. Maana hata mtoto anaweza kukutukana Kama utampa pipi moja wakati watoto wenzake umewapa pipi tano tano mbele yake. Kama hatakutukana basi atalia Sana au kufanya vitendo ambavyo utalazimika kumuongezea pipi au kumpiga.

Viongozi wa dini bila kupepesa macho Wala kumung'unya maneno yetu hubirini zaidi haki itendeke katika kila hatua ya Uchaguzi kuliko Jambo lolote. Haki ndiye mzazi wa amani na utulivu. Hata Mungu lazima ampeleke peponi na kumjalia zaidi Yule anaemcha Mungu kuliko asiyemchaMungu, Kama atafanya kinyume chake atakuwa hajatenda haki na hakutakuwa na mchamungu Tena. Kiongozi wa dini kukemea lugha za matusi bila kukemea vitendo vinavyonyima haki Ni kuidhalilisha na kuiondolea umuhimu makanisa na misikiti yenu kwenye jamaa. Itaonekana Kama vile hamjui mnachokisema na mtendalo.

Baada ya uchaguzi maisha mitaani, misikitini, makanisani, ofisini, kwenye madaladala lazima yaendelee.

Wadau tusaidiane kwenye hili
 
Back
Top Bottom