Kuna maisha baada ya siasa


manzuki

manzuki

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2017
Messages
276
Likes
143
Points
60
manzuki

manzuki

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2017
276 143 60
Kwanza kabisa natoa pongezi za dhati katika Serikali ya awamu ya tano inayofanya kazi kwa uzalendo mkubwa uliotukuka wa kuwahudumia wananchi katika masuala mbalimbali ya maendeleo kama maji, elimu bure, kukomesha uzembe kazini , kudhibiti rasilimali za taifa, vyeti feki pamoja na watumishi hewa kazini.

Kwa muda mrefu nimekumbuka chama kikuu pinzani enzi za Dr. Slaa walipokuwa na agenda ya ufisadi na mambo mbalimbali huku wakisema Kikwete ni dhaifu nchi imemshinda mzee wa msoga alikaa kimya na mwisho wa siku alimaliza muda wake.

Baada ya kipyenga cha uchaguzi mkuu kilipopulizwa 2015, John Pombe Magufuli alipita ili apeperushe bendera ya CCM kugombea urais huku chama pinzani kikaamua kumpitisha bwana Lowassa ambaye walisema sana kuwa ni fisadi katika mikoa mbalimbali ,ambapo kulikuwepo operation sangara, operation fichua mafisadi na nyimbo nyingi nderemo na vifijo zilikiwa zinaimbwa za kufichua ufisadi ndani ya nchi.

Kipindi kile kilikuwa kipindi kizuri sana kwa sababu chama kilikuwa na nguvu kubwa walisamama kidete kupinga ufisadi uliokuwa unafanywa ndani ya nchi na mfano mzuri alisemwa sana Lowassa kwa kweli kwa sasa ukiangalia kwa umakini CHADEMA ya Lowassa na Dr. Slaa ina utofauti mkubwa sana,hasa unaposikia mwenyekiti wa chama bwana Mbowe anapoita waandishi wa habari na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu nchi yaani utafikiri ni tangazo la biko na tatu mzuka hakuna anachokisimamia kazi kubwa yeye nikudai demokrasia.

Kiongozi mkubwa kama huyo anasimama mbele ya wanahabari anasimama na kuongea mambo ya hovyo hasa kuhusu shambulio la mheshimiwa Tundu Lissu ambapo alivituhumu moja kwa moja vyombo vya dola bila kuwa na vielelezo vyovyote wala ushahidi ni ishara mbaya ya kuonekana kuwa yeye na washirika wake hawafai kuongoza nchi.

Kwa sasa nawaona kama kina Nassary baada ya kukosa dira na mwelekeo katika chama chao visingizio vimekuwa vingi mara maisha yao yako hatarini na mwenzake Lema walizoea siasa za kuchafuana wakapata credit kubwa kwasasa hawa na agenda yoyote yakuwambia wananchi Mrisho Gambo na Mnyeti wamejikita kuwatumikia wananchi kama ilani ya chama cha CCM na Serikali baada ya kuona kwamba wamezidiwa kete na kuona kwamba majimbo yao yako hatarini kuchukuliwa na CCM sasa hivi wamebaki wanalialia na kusema wanatishiwa maisha.

Hii yote ni kukosa cha kufanya katika majimbo yao na ukweli ni kwamba wananchi wa mkoa wa Arusha wameapa kuwaadhibu vijana hawa wasirudi bungeni 2020 baada yakuona hakuna wanachokifanya katika majimbo yao. Hii yote agenda zote walizokuwa wamezibeba Rais anazifanyia kazi moja baada ya nyingine lakini pia tukirudi kwa zitto tangu ameanzisha chama chake na kuwa kiongozi wa chama wanachama pamoja na viongozi wameamua kukihama chama baada yakuona hakuna agenda yoyote chama kinasimamia na hata hivyo ni kuona Zitto anaongoza chama kihuni juzi wazee wa Kigoma walimkemea baada yakwenda na majina ya kihuni ya mitaa katika jimbo analoliongoza akataka mitaa ipewe majina aliyokuwa nayo ya kihuni uongozi wa mkoa pamoja na wazee wa mji huo walimpiga stop ndipo alipokimbilia Dar es Salaam kujificha huko baada ya muda wanachama na viongozi walikihama chama baada ya kupoteza dira na mwelekeo.

Kudhihirisha hayo hata Mbowe alishaona jimbo lake la Hai ana wasiwasi linaweza kuchukuliwa 2020 hata Zitto kashaona hvo kwamba uwezekano wa kurudi bungeni ni mdogo akiwemo Lema na Nassari ,ndiyo maana wanalialia kila kukicha mara wanatafutwa na watu wasiojulikana mbona Mbilinyi,profesor Jay na wengine hawalalamiki lalamiki kama wao. Kama umeshindwa kutimiza ahadi ulizoziahidi katika jimbo lako wananchi wana haki ya kukuadhibu kwenye box la kura na kutoka.

Mjue kwamba kuna maisha baada ya siasa, ameingia Rais mzalendo anayetekeleza wajibu wake kwa sasa mtalia lia sana, angalieni chama cha CUF eti CUF ya Maalim Seif na CUF ya Lipumba ukiangalia hivo mpiga kura wa kawaida anayeipenda CUF anakuwaje(lazima akose mwelekeo)
 
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Messages
29,917
Likes
37,161
Points
280
GENTAMYCINE

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2013
29,917 37,161 280
Mkuu ulisoma na kuielewa vizuri kabisa Communication Skills huko Shuleni au Chuoni Kwako ulikopita? Tuanzie hapa Kwanza manake duh!!!!!!!
 
T

treborx

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,515
Likes
2,079
Points
280
T

treborx

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,515 2,079 280
Hebu tupe takwimu za maji na umeme. Watanzania wangapi wamepata maji safi na salama, na umeme wa uhakika tangu mwaka 2016??
 
chibalangunamchezo

chibalangunamchezo

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
1,525
Likes
2,586
Points
280
chibalangunamchezo

chibalangunamchezo

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
1,525 2,586 280
Kumbe sometimes, mnapataga akili, zitawakaa sawa tu cdm hakuna kitu ni wakurupukaji.
 

Forum statistics

Threads 1,235,814
Members 474,742
Posts 29,236,883