Kuna maisha baada ya haya

babadullah

JF-Expert Member
Feb 21, 2017
508
318
Ushawahi kujiuliza ulikuwa wapi miaka elf moja,iliyopita
Na utakuwa wapi baada ya miaka buku,ijayo
Jiulize ni,kwann,umeumbwa yan ni nn lengo la kuumbwa kwako
Je baada ya maisha haya utakuwa na hali gan
Tunahimizana kutengeneza future life, ni IPI hiyo future life, Mimi nijuavyo future life ni maisha baada, ya kifo
Tu jiandae na maisha baada ya kifo kwan ndiyo ya kudumu na,ya milele
 
Hivi haiwezekani ikawa hivi:
Kwamba kama niko hivi ninavyojiona/jitambua, kama nitakufa na mara tu baada ya kufa au baada ya miaka makumi, mamia au maelfu baadae nikajikuta na umbile na mwili mpya tofauti na ule niliokufa nao huku nikiwa siwezi kufanya yale niliyokuwa nimezoea kufanya kipindi cha uhai wangu mfano kupiga mswaki, kuvaa nguo, kula, kufanya kazi za uzalishaji mali n.k. basi mimi nitakuwa siyo tena yule "binadamu wa kawaida" niliyepata kuishi miaka hiyo?

Naamini wapo watakaoelewa hoja yangu.
 
Yapo maisha jiandae na mioyo yenu kwenda Mbinguni / Peponi..... Haya ya dunia yapo tu miaka 70 au mia ni michache compared to eternity.....
 
babadullah Umeongea sense sana sema basi tena biandamu hawataki kusikia hizi habari..hawataki kusikia kifo wakati its the truest of all kwamba whether tunataka au hatutaki lakini lazma tufe tu.

Bob Marley aliwahi kuulizwa akiwa na afya nzuri tu kwamba what is your richness because we heard you have a lot of money akasema "my richness is life forever and not how much I have in my bank account.

Tujiulize utajiri wetu ni upi sisi binadamu maana we live to die rejected and alone in the tomb.
 
Maisha ni hayo uliyo nayo, roho ikitoja (kifo) inaenda kuanzisha maisha mengine kama mbwa, kondoo au kitu chochote chenye uhai kwa maisha mengine tofauti na uliyoishi. Ukiondoka umeondoka hakuna mtu kama wewe tena. Hivyo vunja mifupa bado maisha yangalipo. Kuna vitu vingi vyenye uhai na Mungu alishaumba roho za kutosha ni mzunguko tu wa kuwa na maumbo tofauti. Kwa hiyo mbinguni na motoni ni hekaya za abunuwasi
 
Kwahyo huamini uwepo wa pepo na moto baada ya kifo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom