Kuna mahali tulikosea... you tell me where..

Point ya muhimu ambayo tunatakiwa kuangalia ni kuwa ni nini kifanyike.
Possibly now we have the worst president ever,ambaye 2 years ago wengi walijua probably atakuwa the best president ever!
It seems kuwa yeye mwenyewe kama rais hajui kaenda kombo wapi na hata kama akijua sidhani kama kuna lolote ambalo litafanyika,kwa sababu waliomzunguka wanampa habari ambazo yeye anataka kuzisikia.
Tulipokosea mimi naona ni 1995.Ule uchanguzi wa kwanza wa vyama vingi ulitakiwa kuleta mabadiliko makubwa sana na labda kuwafungua macho wananchi ambao walikuwa wanahitaji hivyo.
Hawa wakima Mbowe,Slaa,Zito ndio walitakiwa kuwepo wakati ule with Mrema,Marando,Lamwai na lile kundi lote.Matokeo,wale wotehawapo na sasa kuna wengine,na inaelekea itaendelea hivohivo.Sasa hivi kulitakiwa kuwe na upinzani thabiti,kiasi cha kufanya hata vijana wa sasa iwe ni rahisi kwao kuingia kwenye upinzani sio kwa sababu mtu anaichukia tu CCM au anajua hawezi kuendelea akiingia CCM,bali kujua kuwa anaweza kuleta maendeleo kwa nchi yake kupitia upinzani.
Tutasema hapa kuwa ujamaa was wrong,lakini wengi huko nyuma ukisoma wanasema ujamaa was right,lakini implemetation was wrong.
Mtu ambaye ni rafiki na anashauriwa na G. Bush unategemea nini kutoka kwake? mwenzake kashamalize 8 yake na US ndio hiyoo.
 
Huku Tanganyika (ingawa kwa kwa sasa hakuna serikali yenye jina hili ) huwezi kamwe kusema kuwa Waislam au hata Wakristo ndio majority unless unataka sensa ifanyike leo chini ya uangalizi wa taasisi ya Kimataifa itakayoongozwa na mpagani. Tanganyika itaachwa iendelee kufurahia serikali isiyoongozwa kwa msingi wa biblia wala korani.
Pia ieleweke wazi kuwa hata matatizo kibao ya miafaka isiyo miafaka huko Zanzibar na maswali ya kama Zanzibar ni nchi au taifa au serikali au mkoa itakuwa inapata fumbuzi zake endapo wataachwa wakae huru kama nchi.

Hivi kwa nini tunangángánia ndoa ambayo wanandoa wenyewe wanamalamiko kibao na huo muungano wao? Bora iwe sasa kabla ya siku za usoni ambapo kutakuwepo na ubishi mkubwa sana na huenda mapigano ambayo si ya lazima. Maana juu ya suala la mafuta/ gesi huko zenji watu sasa wanaanza hata kuhesabu mayai kabla ya kutotolewa vifaranga.

Nyerere na Karume asanteni kwa kazi yenu na nia yenu nzuri na mbarikiwe sana lakini leo tutabadilika kutokana na mazingira ya sasa kwa ajili ya kuendeleza Amani na maendeleo na endeleeni kutuelewa kuwa nia yetu si mbaya na mtubariki tu kwa hilo. Period!

Mh. Kikwete usikae kimya, inapokuja katika mijadala moto na yenye utata ambayo inaweza hata kuyumbisha mihimili ya Taifa hapo ndipo Maraisi wote au Wafalme wote au Mawaziri wakuu wote hutakiwa kusimama pasi kusitasita mbele ya vipaza sauti dakika hiyo na kukemea kauli za kupotosha na kueleza msimamo wa Serikali ya sasa ambapo kamwe huwezi kuruhusu waziri wako aeleze kuwa TZ ya leo kujiunga na OIC ni sawa na aendelee kuhalalisha mapokezi ya msaada wowote hata kama una ndoana ambazo kwazo unapingana na Katiba yetu au unatulazimisha sote tukubaliane na matakwa ya watoa msaada! Hapo ndipo utawaambiwa waliokuweka Ofisini kuwa 'hayo yalikuwa mawazo binasfi ya Membe na siyo Waziri katika Serikali yako'.

1. Inawezekana hakuna taarifa rasmi za kiserikali kuhusu idadi ya waislamu ama wakristo lakini nijuavyo mimi ni kuwa makundi haya ya kiimani ya mitandano yao inayotumika kuwa na data hizi kila nyakati. Siku hizi kaka kuna watu wanafuatilia data hata kujua katika mwezi huu ni wakristo wangapi wamepata leseni za biashara na waislamu wangapi.....hiyo ndio Tanzania ya baada ya Mwalimu....

2. Kusema kuwa malalamiko yawe sababu za kuvunja muungano ni ufinyu wa kimawazo. taifa halijengwi, haliendelezwi na wala halilindwi kwa mtindo wa kususasusa eti malalamiko mengi. Kuna kitu cha kijamii kinachokosa malalmiko yasiyokwisha. Mfano wa ndoa ni wa kipunguani kabisa..na hili nalisema kwa wote wanaopenda kutumia mfano huu. Kama malalamiko yasiyokwisha kwenye ndoa yanakuwa sababu ya kuvunja ndoa no wonder unakuwa na jamii hivyohovyo iliyojaa chokoraa wa kipato na elimu ya daraja mbalimbali....sembuse taifa litakalokuwa likikimbilia kuvunja muungano kwa sababu ya hicho kiitwacho malalamiko yasiyokwisha..no wonder familia zetu nyingi zinabomoka kila kukicha..

3. Rais hapaswi kukurupuka kujibizana na makundi maalumu yenye maslahi binafsi yasiyotilia maanani masilahi ya nchi kwa ujumla. Kama swala la kadhi na la OIC linafanywa upeo wa kutokea kwa wenye manung'uniko yao ambayo kwa upande mmoja ama mwengine yanhusiana na URAIS wake atakuwa ni RAIS hovyo kama atakimbilia kujiingiza kwenye mfarakano huu wa kijinga bila ya kuusoma kwa umakini na kutambua wahusika, nguvu na masilahi yao katika suala hili na ni vipi uhusika wake utakavyoathiri TAIFA na URAIS wake kwa ujumla. Urais sio kazi ya kukurupuka kujionyesha kuwa upo kila pale panapofuka moshi uwepo.....

Tanzanianjema
 
1. Inawezekana hakuna taarifa rasmi za kiserikali kuhusu idadi ya waislamu ama wakristo lakini nijuavyo mimi ni kuwa makundi haya ya kiimani ya mitandano yao inayotumika kuwa na data hizi kila nyakati. Siku hizi kaka kuna watu wanafuatilia data hata kujua katika mwezi huu ni wakristo wangapi wamepata leseni za biashara na waislamu wangapi.....hiyo ndio Tanzania ya baada ya Mwalimu....

2. Kusema kuwa malalamiko yawe sababu za kuvunja muungano ni ufinyu wa kimawazo. taifa halijengwi, haliendelezwi na wala halilindwi kwa mtindo wa kususasusa eti malalamiko mengi. Kuna kitu cha kijamii kinachokosa malalmiko yasiyokwisha. Mfano wa ndoa ni wa kipunguani kabisa..na hili nalisema kwa wote wanaopenda kutumia mfano huu. Kama malalamiko yasiyokwisha kwenye ndoa yanakuwa sababu ya kuvunja ndoa no wonder unakuwa na jamii hivyohovyo iliyojaa chokoraa wa kipato na elimu ya daraja mbalimbali....sembuse taifa litakalokuwa likikimbilia kuvunja muungano kwa sababu ya hicho kiitwacho malalamiko yasiyokwisha..no wonder familia zetu nyingi zinabomoka kila kukicha..

3. Rais hapaswi kukurupuka kujibizana na makundi maalumu yenye maslahi binafsi yasiyotilia maanani masilahi ya nchi kwa ujumla. Kama swala la kadhi na la OIC linafanywa upeo wa kutokea kwa wenye manung'uniko yao ambayo kwa upande mmoja ama mwengine yanhusiana na URAIS wake atakuwa ni RAIS hovyo kama atakimbilia kujiingiza kwenye mfarakano huu wa kijinga bila ya kuusoma kwa umakini na kutambua wahusika, nguvu na masilahi yao katika suala hili na ni vipi uhusika wake utakavyoathiri TAIFA na URAIS wake kwa ujumla. Urais sio kazi ya kukurupuka kujionyesha kuwa upo kila pale panapofuka moshi uwepo.....

Ahsante mkuu wa PHDddddd, hivi Mwalimu alipokuwa anakataa tusijiunge na OIC alikuwa anatokea kundi gani kati ya hayo makundi yako?
 
Nchi INAENDELEA. Cha kujadili hapa labda ni kasi na viwango kama vinaridhisha? Maisha ya kila siku ya watu wetu yanaguswa na maendeleo haya kwa kiwango gani? Je tunaweza kufanya vizuri zaidi ya hapa tulipo? Nini kifanyike ili KUZUIA mapungufu yanayojitokeza hasa kwenye UONGOZI, UTENDAJI na USIMAMIZI wa MAFANIKIO kidogo tuliyoyapata? Tatizo hasa liko wapi; watu wetu? uongozi wetu? sera zetu?
 
Kwa namana fulani nakubalina na mheshimiwa hapa, ingawa sifikiri kuwa hili ndio tatizo la msingi. Binafsi naamini kwa nchi changa kama yetu kukosea ni kitu cha kawaida, ila baada ya kukosea tunafanya nini? ndio tatizo. Viongozi karibu kama si wote tulionao wallikuwpo katika huo mwanzo unaousema na walionekana kukubaliana na yote, kumbe sivyo. Walikuwa waongo, TATIZO LETU NDUGU ZANGU NI DHAMIRI ZETU. Tunachokisema sio tunachoamini na hili ni tatizo kubwa na ndio maana nikasema pale mwanzo kuwa wenzetu wanafahamu kuwa nchi ina tatizo lakini wanatumia mwanya huo kujinufaisha. Jibu la tatizo letu ni kupata dhamiri safi, kama haiwezekani ni kujenga mfumo utakaowezesha kila kitu kuwa wazi. Kwa njia hii tutaweza kujua dhamira za viongozi wetu mapema kabla hawajatupeleka mbali na hapa ndio mwanzo wa nafasi ya kuweza kutengeneza yale tuliyoyaharibu.
Nilikuwa sijamaliza nikapata kajidharula.
Jingine ambalo nahisi kuwa ni kusa kubwa tulilifanya ni kuamini mtu badala ya System(mfumo), mwanzoni hatukuona kuwa ni tatizo kwa kuwa tuliyemwamini alikuwa ni mtu wa kuaminika. Lakini sasa tatizo linaonekana wazi, ingekuwa ni mfumo ingekuwa rahisi. Tunaangalia watu tumekosea tunarekebisha tunaenda mbele, lakini kwa kuwa imani yetu tulijenga juu ya watu kuwarekebisha ni ngumu kweli. Hasa ukizingatia kuwa wanajua wanachokifanya, na wanajua hakuna mfumo wowote uliopo kuwazuia wasifanye, hii ni ngumu sana. Hakuna nchi ambayo imeweza kupiga hatua vizuri bila ya kuwa na systems zinazofanya kazi vizuri, zenye kuweza kuwachunga hata wale waliopewa dhamana. Na uzuri ukijenga imani juu ya system na si mtu ni rahisi kutathmini hatua unazopiga, ili kujua kama uongeze kasi au urekebishe nini.
 
Hivi karibuni Kenya imeunda tume ya "Ukweli na Maridhiano" ili kuangalia historia yao na kuona ni wapi walienda kombo hadi kusababisha matukio ya Disemba mwaka jana.. Je Tanzania inahitaji tume ya Historia au kitu kama hicho ili ipitie historia yetu na kutoa majibu ya maswali mengi ambayo watu wanayo kwa mfano kuhusu Mapinduzi, Uasi wa Jeshi, n.k ? Je tutaendelea kuikimbia historia yetu mpaka lini?
 
Mtajiuliza weee....mtafanya kila kitu....mwisho wa siku....sisi Ndivyo Tulivyo na hakuna lolote la maana litakalotokea. I'm sad to say it but it is true and y'all know it's true.....
 
Wajamani,
Mie kila siku nimekuwa nikisoma haya malalamiko ya Muungano. Nafikiri Wazenji na Wailsma ni kama watu wa East Timo. Hata mkipata u mkivunja Muungano, milele hamtaendelea. Watakuja akina dr. Salimin Amour (komandoo??) na kuanza kula hela zenu kama kazi. Mtaendea kuuwa Muungano wa Zanzibar yaani Pemba na Unguja. Nasikia eti kisa Wa-Unguja hawataki watu wa Pemba kuingia madarakani ni sababu kuwa "wakati wao wanapigania uhuru, Wapemba walishirikiana na Sultan". Ukweli leo twaujua kuwa SI KARUME aliyepigania Uhuru wa Zenji ila M-Uganda John Okello. Mkumbuke milele kuwa uhuru wenu umeletwa na John Okello na si ABEID AMMAN KARUME.
Sasa kwa Zanzibar ambayo misingi yake imejengwa kwa kudanganywa, milele watanganywa. Mmoja kataka kuwa RAIS wa NCHI, anafikiria heri nivunje Muungano. Anaanza kampeni za kuwa Eti wao wananyanyaswa katika Muungano. Huko Zenji hamna kitu kwa sasa zaidi ya utalii. Heri watu wa Tarime walalame maana kwao wana madini. Ila hawa hawajasema wavunje Muungano. Kama Tabora ingelikuwa kisiwa, na mie ningelisema kuwa tuvunje Muungano maana serikali yetu haijafanya kitu cha chochote Tabora, zaidi ya NSSF kujenga jengo ambalo liligeuzwa kuwa DISCO na kuuwa watoto 20. Ukifika Tabora mjini ndiyo utajua ninasema nini. Mita kadhaa kutoka kituo cha bus kuna nyumba zimechoka hata Sikonge kuna nafuu. Au na sisi Tabora tuingie umoja wa Waislam? Tuanzishe mahakama ya kadhi? Tuingie EU? Tuvunje Muungano na tuanzshie taifa la Tabora? Tutangaze autonomy kama wanavyotaka Tarime?
Tatizo la Wazenji ni kuwa nyie mkifika Dar, mnafikiri mmeshaona bara nzima. Malizieni homework. Njooni Sikonge, nendeni Tarime, nendeni Kigoma na ndipo muanze kulinganisha Bara na Zanziba. Malalamiko mengi ya kuvunja Muungano yamekaa kaa kama watu WAVIVU wanaoona wakivunja Muungano na wao watakuwa akina SOMEBODY kwenye nchi mpya ya Zenji. Na miezi sita baadaye kutakuwa na nchi ya Unguja na Pemba. Ni UVIVU na tu unatusumbua Watanzania kwa ujumla. Ukiongeza na UJINGA ndiyo inakuwa kama kwenye BIBLIA kuwa neno "tuvunje Muungano" linaangukia kwenye udongo mzuri na ukisema "tubadilike na tuongeze juhudi" unakuwa umeangusha maneno kwenye MWAMBA wa jiwe. Ndege watakuja na KUYALA.

WHAT TO DO:-
1. Tuvunje BUNGE. Wabunge hakuna chochote cha maana wanachokifanya. Wapo hapo kama picha tu huku tukipoteza mamilioni ya fedha kuwalisha wao na vimada wao. Muome Komba alivyonona. Hata Wangwe aliongeza mke wa pili.
Sheria zote za Tz ziwe zinaandikwa na "KITENGO CHA KATIBA" ambacho kitaundwa na Majaji, mahakimu, wanasheria na Waalimu wa sheria wa vyo vikuu.

2. Mawaziri wachaguliwe NJE ya BUNGE. Wawe ni watu Profesional. Ikiwezekana watume maombi ya kuwa WAZIRI na THE BEST wachaguliwe. Wakubali kuacha kazi zao zote na wawe wanashughulikia uongozi tu. Akiendelea na biashara zake basi anakuwa anavunja MAKUBALIANO na adhabu kali ichukuliwe. Hawa walipwe vizuri ili wasiwe na tamaa ya kuiba. Akivunja miiko adhabu yake iwe kali sana.

3. Madaraka mikoani. Wakuu wa Wilaya ndiyo wafanye kazi kama wanavyofanya kazi Wabunge. Boss wao ya RC ndiyo awe msimamizi wao. Wote hawa wachanguliwe na wananchi. Tanzania tuna watu wengi sana wanaenda chooni kwa ghalama za walipa kodi kwa kutofanya kazi yoyote. Mishahara yao isiwe ya ajabu.

Rais achagulie kutoka hawa ma-RC au DC. Kiongozi mzuri ni yule ambaye kwa bidii yake na mawazo yake, ameleta maendeleo katika walaya au Mkoa wake. Hiki kiwe kipimo kwa wananchi. Ila kama alipendelewa na Waziri wa fedha, achunguzwe mara mbili. Hapa iangalie kipi kipya alikileta bila msaada wa Mawaziri.

- Wabunge hata mwaka mmoja hawajapinga bajeti. Kila mwaka wanaipitisha kwa 100%. Ina maana hakuna wabunge kupinga. Sheria ndiyo hizo zimezorota. Hata Kikwete mwenyewe anasema wazi kuwa rais ana madaraka makubwa sana. Wabunge wamelala kabisaa. Wizi wa pesa si kazi ya bunge. Leo tunamuona Mwakyembe na wenzie mashujaa ni kutokana na UOZO wa system. Ilitakiwa Hosea na UWT wafanye kazi. No more TUME. Mazeruzeru wanakufa, hakuna mtu anakamatwa. Hadi inaandikwa CNN na BBC ndipo Muungwana anakubali kupokea Maandamano ya Ma-Albino. Serikali iko wapi?

Yangu kwa leo ni HAYO.
 
Hata kama Muungano utakufa... sisi Waislaam wa bara tunataka kujiunga na OIC na swala la kadhi lishughulikiwe!... sasa twambieni sisi sio raia wenye haki sawa na nyie..Imekuwa ujinga sasa hvi, au mnataka tuanzishe vyama vya upinzani wa kidni ndio mjue kumekucha!

Kuna manufaa yoyote mtapata mkijiunga na OIC? au ndio bendera fuata upepo, mnaweza kufanya mnachotaka kama waislamu ila tafadhali msiburuze na wengine wasiohusika...kumbuka kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
 
Tonga,
Mkuu sizungumzi na watu wanaotanguliza nenoi MKI-JIUNGA na OIC kama vile sisi ni uchafu fulani ktk nguo zenu...Hili ndilo tatizo kubwa -THEM as if nyie mna nafuu fulani... Hapa ndipo tulipokosea!
Wakuu jifunzeni kuzungumza pamoja na chuki zetu ambazo zinajitokeza sana siku hizi.. na hakika hii ni ishara moja kubwa ya NDIVYO TULIVYO....Mnapenda sana kuzungumzia chupa badala ya content yaani kwenu Cocacola ni chupa yake, sabuni ya kufuria ni OMO, Vacuum ni Hoover, Magarine ni Blueband na kadhalika..Ukimuuliza mtu ingredients za kitu hata kimoja wapo hakuna mtu anayefahamu wakati shule mmekwenda!..
Ndivyo tulivyofundishwa na ndio elimu tunayojivunia leo wakati imetujaza ujinga mtupu..Hizo dini zenyewe hatujui kitu zaidi ya kuzungumzia maisha ya Yesu na Muhammad..(Chupa nyingine)
kiasi kwamba tunasubiri Yesu ama Muhammad watuongoze peponi utafikiri kundi la kondoo!..Akili ya kitumwa - That time is gone my brother!
Kuzungumzia waislaam hivi ama vile wakati hufahamu kitu kuhusu Uislaam isipokuwa jinsi unavyomuona Juma jirani yako ni ishara tosha ya ndivyo tulivyo.. na Nyani Ngabu hajakosea kitu kabisa!
Sisi tutakuwa wa kwanza kuingia motoni na tutajisifia kushika nafasi ya kwanza!... Ndivyo tulivyo!
 
Mkandara hapa umesema jambo moja muhimu sana na siyo sisi tu hapa kwenye mtandao bali hata kwenye taasisi zetu hizi jinsi suala la OIC linavyozungumzwa. Wakristu wanazungumzia kitu nje yao na Waislamu wanazungumzia kitu wakiondoa wengine. Utasikia wakristu wakiwataka Waislamu "wajiunge OIC" au "Waanzishe mahakama zao" na Waislamu wakiwataka Wakristu "wawaache na mambo yasiyowahusu" na kuwa "haya ni masuala ya Waislamu".

Sasa kwa mtindo huwa wa exclusion ya yule mwingine utaona kuwa kila mmoja hayuko tayari kumsikiliza mwingine kwani kuna kile kitu kinachoitwa "noise". Wakristu hawako tayari kusikiliza hoja za Waislamu, kuzipima na kuona ni kwa kiasi gani zinafaa au hazifai badala yake wanazikataa outright. WAislamu nao hawako tayari kusikiliza kwanini Wakristu wanapinga na kupima hoja hizo na kuona uzito na ukweli wake. Matokeo yake kinachoangaliwa ni "nani" kasema.

Mijadala hii itabadilika kabisa pale baadhi ya Wakristu watakapounga mkono OIC na Mahakama ya Kadhi na baadhi ya Waislamu wakapinga vitu hivyo. Ikitokea hilo mjadala ndipo utalazimisha watu kukaa chini na kuzungumza kama Taifa na siyo vijikundi vya watu wachache.
 
Kama tulikosea toka mwanzo, kwanini hatujajirekebisha ili tuwe sahihi, au ndio tuko sahihi sasa na hatuhitaji kujirekebisha? Au twende mbele kwa mbele na mambo yatajisahihisha yenyewe mbele ya safari?

Mwanakijiji,Makala zako nyingi zimekuwa kuilamu serikali yetu.Ni sawa.Lakini si sawa kwa mtu msomi(naamini wewe ni msomi) kulaumu kila wakati.Kulaumu ni ishara ya kushindwa kufikiri.Si vibaya tukilaumu,But what next after that.Nashukuru umetambua hata sisi yumkini tumechangia,Sasa,wewe kama msomi( i believe so) naomba utoe opinon kama ungepata nafasi ya kukaa na Mheshimiwa pamoja na baraza lake na wakakwambia wameshindwa kabisa wanahitaji ushauri wako na hakika wataufanyia kazi katika kuleta maziwa na asali Tanzania,ungewaambia nini? Kama umewahi kutoa opinion si vibaya ukarudia tena kwa faida ya watanzania.Thanx in advance
 
Mwanakijiji,
nakubaliana na wewe sana tu na hakika swala hili lawama zipo pande zote... sisi wananchi na serikali yenyewe..
Kuna ubaguzi mkubwa unaojengwa na chuki kati ya Waislaam na Wakristu nje ya uwezo wa serikali..tatizo mkuu wangu ni kama nilivyosema sisi sote hatutaki kujua yaliyomo ila gamba la juu ndio kitabu chenyewe..Soda ya Cocacola inatambuliwa kwa chupa na rangi yake!
Hali hii haikuwepo enzi za mwalimu, Wakristu walikuwa bega kwa bega na Waislaam ktk maswala mengi pamoja na kwamba mapungufu yalikuwepo lakini kutokana na mfumo uliokuwepo tofauti zetu hazikuwa na impact kubwa ktk maisha ya watu ya kila siku...
Leo hii dini zimekuwa na sauti kubwa sna kwa sababu nchi yetu haina dira tena, haina malengo zaidi ya kila mtu kubeba mzigo wake na dini zimechukua nafasi kubwa ya uongozi wa wananchi wake kwa kujenga dira zao ambazo kama siasa ni lazima kwanza zi Identify adui wake..Hivyo kila mmoja anajihadhali na huyo Q&Q - ADUI..

Yote haya mkuu yametokana na Ulimbukeni, ushamba na kupenda kuiga culture na Values za nje tukifikira kwamba wageni wa dhehebu ama dini zetu ndio ndugu zetu kuliko Mtanzania mwenzangu mwenye imani tofauti. Kwam kufanya hivyo tumeunda jamii mbili tofauti kati yetu, ndicho unachokiona hapa na huko nje kiasi kwamba leo hii Muislaam hawezi kufanya kitu bila kuuliza kama mwanzilishi ni Mkristu ama Muislaam na kwa maslahi ya jamii ipi.
Mwisho wa yote haya mkuu wangu kutakuja kuwepo madhara makubwa sana kati ya waumini wa dini hizi mbili ambao wote kwa mtazamo wangu hawajui dini ni kitu gani zaidi ya kutazama cover lake, kama vile tulivyozoea kuita sabuni ya kufuria ni OMO..Huwezi ku accept Uislaam bila kukubali yoliyomo na huwezi kukubali Ukristu bila kukubali yanakuja na Ukristu..
Kuzuia mojawapo kwa sababu ya imani zetu ni kupanua gap la utenganishi na mwisho wa yote waathirika ni sisi wenyewe. rwanda wameanza kuuana kwa sababu ya kutokubaliana na kupokea tofauti zao, Somalia vile vile wote wameanzia mambo madogo kabisa!..
Mimi nitawalaumu sana viongozi wa madhehebu haya mawili, Evangalist na hao Ansar Sunni kwani hawa ndio wanapandikiza mbegu mbaya sana za UDINI. Niliyasema haya toka zamani wakati wa matatizo ya Mwembechai na mkuu yanazidi kuota mizizi sasa hivi..
 
Yah, huu ni wakati wa kuangalia wapi tulijikwaa.


Tumemdharau Ajui Ujinga, Matokeo yake amemakribisha Rafiki yake Umaskini na hapa ndipo Adui huyu Umaskini akatuletea Matatizo Makubwa si mengine bali ni Adui Maradhi, tena afadhali ingekuwa maradhi ya Mwili , hasha ni Maradhi ya Akili, Ni Ugonjwa Mbaya sana ambao unatutafuna yah Maradhi ya Akili, hapa ndipo tulipokosea.

Uwezo wetu wa Kufikiria umeenda wapi jamani? Ni heri kufilisika Kimali kuliko kufilisika Kifikra, Kwamba Imefikia mahali hatuwezi hata Kuchimba shimo la choo cha shule mpaka tupate msaada! Ina maana hatujui hata nini tunapaswa kufanya juu Utajiri wote uliotuzunguka jamani? Nchi yetu imezungukwa Na Maji Kusini, Kasakazini, Mashariki na Magharibi, nhi inatiririsha maji kila kona ya Nchi, Tunahitaji watu Creative, wataoweza kuikiria mikakati ya nini kifanyike juu ya Ardhi Nzuri kubwa na yenye Rutuba, juu ya samaki waliojaa katika Maziwa na Bahari yaliyoizunguka hii nchi, juu Wanyama pori wavuatiao waliojaa katika Mbuga zetu, Juu ya Madini na vito amabvyo Mungu aliamua kuvizika ardhini kwa Manufaa ya watanzania, Juu ya PEPO kali zimumazo katika milima ya Pare pamoja na Sehemu nyingi za Tanzania. Si hivyo tu ni LAZIMA watu hao Wafikri yote hayo kwa niaba ya Watanzania na siyo Maslahi yao Binafsi.
 
Back
Top Bottom