Kuna mahali tulikosea... you tell me where.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna mahali tulikosea... you tell me where..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 26, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tunaweza kuwalaumu, tunaweza kuwabebesha kila aina ya lawama na pia tunaweza kuwabeza, kuwakejeli, na kuwanyoshea vidole. Ukweli utabakia kuwa yawezekana siyo kosa lao peke yao; ni kosa letu pia.

  Kuna mahali tulipopotea njia, au mahali ambapo tulikwepa kufanya tulichotakiwa kufanya na matokeo yake tupo hapa tunarushiana maneno, madongo na kila aina ya lawama. Yawezekana ni rahisi kumtaja mtu mmoja na kusema huyu ndiye anawajibika kwa kupotea njia, au kutaja kikundi kimoja cha watu na kusema "wale" ndio wanawajibika kwa sisi kujikuta hapa tulipo.

  Hata hivyo yawezekana kabisa kuwa mzigo huu wa lawama unatakiwa kubebwa na watu wengi kama siyo Taifa zima. Kuna kitu hatukifanya tulipotakiwa kufanya na hivyo leo hii tunalipia gharama yake.

  Kuna kitu ambacho nchi tulizokuwa nazo sawa na ambazo bado zina mambo mengi ya kuwakera zimekuwa zikifanya vizuri na kuanza kufuata njia sahihi. Iran, Indonesia, Malaysia, South Korea, India, na sasa Liberia, Rwanda, Congo, Angola na South Afrika..

  Je yawazekana mgongano utakaotokea mwishoni mwa juma (ceteris paribus) utakuwa ni chachu ambayo itaturudisha kwenye njia sahihi kuelekea kule tunakotaka kwenda?
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  M.M.J

  Mbona unalia? Umechapwa!!!! Kosa lako ni kuandika makala marefuuu wakati sisi tunataka tujue JOTI ametembea vipi kule TBC1.

  Hebu andika MPOKI amefanya nini kwenye makala zako kama hutasifiwa na kununuliwa
   
 3. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2008
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Je yawazekana mgongano utakaotokea mwishoni mwa juma (ceteris paribus) utakuwa ni chachu ambayo itaturudisha kwenye njia sahihi kuelekea kule tunakotaka kwenda?"

  Mkuu hapa umeniacha gizani, unaweza kutupa mwanga kidogo?...
   
 4. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nadhani tumekosea kwenye mfumo wetu wa elimu. Hapo tu!
   
 5. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ingawa sifahamu hicho kitakachotokea mwisho wa juma, lakini swali juu kama kuna mahali tumekosea ni kweli kuna mahali tumekosea. Ila bahati mbaya ninayoiona ni kuwa wenzetu wanayatumia makosa haya kujineemesha wao, na wala si kuyarekebisha ili tupate kwenda kama wenzetu uliowataja.
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ujamaa was the wrong foot to start with.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Wakuu hapa tusizunguke mibuyu bure, You can't be wrong and get right, hatukuwa right from the beginning ndio maana tumeishia tulipo sasa, yaani on the wrong side of the coin!

  Never before tuliwahi kuwa right, never!
   
 8. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  sure, but we want to be right now, but how? tupunguze wanasiasa tuongeze watendaji:
  a) Wizara zipungue, ziwe at most 15
  b) majukumu waliyopewa wanasiasa wapewe wataalam ie uteuzi wa gazi mbalimbali, kusaini mikataba, kuidhinisha mipango au hatua mbalimbali za utekelezaji.
  c) kuwe na kitengo maalumu kinachojitegemea cha kuchunguza uhalifu
  d) mishahara, posho na marupurupu ya wanasiasa yaangaliwe upya na kupunguzwa ili wanasiasa wawe wanajitolea zaidi kuliko malipo.
  e) watendaji wajengewe uwezo ili wajiamini na kutekeleza mambo bila kurubuniwa na wanasiasa.

  Hii ni kwa upande mmoja wa siasa na utendaji.
   
 9. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu, obvious kuna sehemu tumekosea sio bure, then what is the next step that should be the major question from su all, nafikiri tuanza kutafuta tulikosea wapi ili tuweze kulekebisha kwani naamini bila kujua tumekosea wapi hatutaweza hata kidogo kumaliza matatizo yetu.

  tukishapata tulipokosea then, the next step will be to make wrong right.

  Je tumekosea wapi?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama tulikosea toka mwanzo, kwanini hatujajirekebisha ili tuwe sahihi, au ndio tuko sahihi sasa na hatuhitaji kujirekebisha? Au twende mbele kwa mbele na mambo yatajisahihisha yenyewe mbele ya safari?
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kuna mengi yatakayotokea mwisho wa wiki ijayo.

  1. Kikao cha Bunge kuanza, masalia kupitiwa ingawa EPA halitakuwapo
  2. Maandamano ya Waislamu kuunga mkono kauli ya Bakwata kuhusu Tanzania kuwa na kadhi na kujiunga OIC
  3. Mafisadi wa EPA wanaweza kufikishwa mahakamani
  4. Operesheni Sangara kuendelea
  5. Kikwete kuenda safarini Marekani kusini
   
 12. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2008
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haswa, wakati mwingine inabidi fikira na mitazamo na maneno na matendo ya watu yakinzane ndipo ukombozi kamili utokee.

  Nawakaribisha Mashehe watoke na kauli kali kabisa dhidi ya Maaskofu, wadai haki zao za kutaka mahakama ya kadhi na kujiunga na OIC ndipo pengine tuone kuwa huu Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar unatakiwa kuvunjwa na kila nchi iwe huru kisha tushirikiane tu kama tufanyavyo kwa Kenya na uganda n.k

  Justification.
  Inaeleweka wazi (hakuna haja ya utafiti hapa) kuwa Zanzibar Waislam ndio majority na hivyo wanastahili kabisa kujiunga na OIC na hata kuunda hayo mahakama ya Kadhi huko na hata kusema kuwa serikali ya Zanzibar inaongozwa chini cha Koran kama watakavyopenda.

  Huku Tanganyika (ingawa kwa kwa sasa hakuna serikali yenye jina hili ) huwezi kamwe kusema kuwa Waislam au hata Wakristo ndio majority unless unataka sensa ifanyike leo chini ya uangalizi wa taasisi ya Kimataifa itakayoongozwa na mpagani. Tanganyika itaachwa iendelee kufurahia serikali isiyoongozwa kwa msingi wa biblia wala korani.
  Pia ieleweke wazi kuwa hata matatizo kibao ya miafaka isiyo miafaka huko Zanzibar na maswali ya kama Zanzibar ni nchi au taifa au serikali au mkoa itakuwa inapata fumbuzi zake endapo wataachwa wakae huru kama nchi.

  Hivi kwa nini tunangángánia ndoa ambayo wanandoa wenyewe wanamalamiko kibao na huo muungano wao? Bora iwe sasa kabla ya siku za usoni ambapo kutakuwepo na ubishi mkubwa sana na huenda mapigano ambayo si ya lazima. Maana juu ya suala la mafuta/ gesi huko zenji watu sasa wanaanza hata kuhesabu mayai kabla ya kutotolewa vifaranga.

  Nyerere na Karume asanteni kwa kazi yenu na nia yenu nzuri na mbarikiwe sana lakini leo tutabadilika kutokana na mazingira ya sasa kwa ajili ya kuendeleza Amani na maendeleo na endeleeni kutuelewa kuwa nia yetu si mbaya na mtubariki tu kwa hilo. Period!

  Mh. Kikwete usikae kimya, inapokuja katika mijadala moto na yenye utata ambayo inaweza hata kuyumbisha mihimili ya Taifa hapo ndipo Maraisi wote au Wafalme wote au Mawaziri wakuu wote hutakiwa kusimama pasi kusitasita mbele ya vipaza sauti dakika hiyo na kukemea kauli za kupotosha na kueleza msimamo wa Serikali ya sasa ambapo kamwe huwezi kuruhusu waziri wako aeleze kuwa TZ ya leo kujiunga na OIC ni sawa na aendelee kuhalalisha mapokezi ya msaada wowote hata kama una ndoana ambazo kwazo unapingana na Katiba yetu au unatulazimisha sote tukubaliane na matakwa ya watoa msaada! Hapo ndipo utawaambiwa waliokuweka Ofisini kuwa 'hayo yalikuwa mawazo binasfi ya Membe na siyo Waziri katika Serikali yako'.
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Yes, bado tunakunywa mivinyo ile ile....na watu ni wale wale waliokuwa addicted na mivinyo tuliyoikosea tangu awali..........

  ....solution tubadilishe wale watu waliokuwa addicted na mivinyo ile iliyotuweka hapa na inayoendelea kutuongoza huko tuendako............

  ......mivinyo kama ile ya akina Mkuchika tuifutilie mbali......tuitafute na tuinywe ile mivinyo bora ya kutuletea afya mwilini.....period
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hata kama Muungano utakufa... sisi Waislaam wa bara tunataka kujiunga na OIC na swala la kadhi lishughulikiwe!... sasa twambieni sisi sio raia wenye haki sawa na nyie..Imekuwa ujinga sasa hvi, au mnataka tuanzishe vyama vya upinzani wa kidni ndio mjue kumekucha!
   
 15. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Mkuu Bob,

  Acha hasira bro, kwani CUF haitoshi?
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu haitoshi naona ipo haja kubwa ya kuunda chama cha waislaam maanake umekuwa upumbavu mtupu... watu tunakosa kujadili mambo ya maana yanayoturudisha sisi sote nyuma tunatafuta kuona wengine wamevaa nini.... yaani mambo ya kike... sorry bob lakini kuna mambo mazito sana kama vile serikali kutaka kununua generators za Richmond kwa bei pengine kubwa kuliko ambayo tunaweza kuagiza generator mpya za General Electric(GE) toka US na guarantee juu yake.. zikafika nchini baada ya mwezi mmoja tu.. Haya ndio maswala mazito, leo Tunakuja zungumzia vitu ambavyo havina msingi kabisa na wala haikuwa kawaida yetu hata siku moja.
  Tumekosea wapi?.. ni pale tunapoanza Ulimbukeni wetu..
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Oct 27, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Ndivyo Tulivyo................
   
 18. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwa namana fulani nakubalina na mheshimiwa hapa, ingawa sifikiri kuwa hili ndio tatizo la msingi. Binafsi naamini kwa nchi changa kama yetu kukosea ni kitu cha kawaida, ila baada ya kukosea tunafanya nini? ndio tatizo. Viongozi karibu kama si wote tulionao wallikuwpo katika huo mwanzo unaousema na walionekana kukubaliana na yote, kumbe sivyo. Walikuwa waongo, TATIZO LETU NDUGU ZANGU NI DHAMIRI ZETU. Tunachokisema sio tunachoamini na hili ni tatizo kubwa na ndio maana nikasema pale mwanzo kuwa wenzetu wanafahamu kuwa nchi ina tatizo lakini wanatumia mwanya huo kujinufaisha. Jibu la tatizo letu ni kupata dhamiri safi, kama haiwezekani ni kujenga mfumo utakaowezesha kila kitu kuwa wazi. Kwa njia hii tutaweza kujua dhamira za viongozi wetu mapema kabla hawajatupeleka mbali na hapa ndio mwanzo wa nafasi ya kuweza kutengeneza yale tuliyoyaharibu.
   
 19. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wema wetu umetuponza Nyerere alikuwa na msaada mkubwa katika nchi jirani za Afrika pengine hilo ndilo limesababisha tukawa na maisha magumu lakini pia ndio nadhani Tanzania inabaki kuwa kisiwa cha amani kwa namna mja au nyingine. Kingine ni ile dhana ya fulani kujua zaidi like zidumu fikira za fulani wakati kila mtu ana uwezo wa kufikiri. Psychologically that made all of us Dumbs until now when people began to wake up like you EXellency MMKJJ.
   
 20. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Point ya muhimu ambayo tunatakiwa kuangalia ni kuwa ni nini kifanyike.
  Possibly now we have the worst president ever,ambaye 2 years ago wengi walijua probably atakuwa the best president ever!
  It seems kuwa yeye mwenyewe kama rais hajui kaenda kombo wapi na hata kama akijua sidhani kama kuna lolote ambalo litafanyika,kwa sababu waliomzunguka wanampa habari ambazo yeye anataka kuzisikia.
  Tulipokosea mimi naona ni 1995.Ule uchanguzi wa kwanza wa vyama vingi ulitakiwa kuleta mabadiliko makubwa sana na labda kuwafungua macho wananchi ambao walikuwa wanahitaji hivyo.
  Hawa wakima Mbowe,Slaa,Zito ndio walitakiwa kuwepo wakati ule with Mrema,Marando,Lamwai na lile kundi lote.Matokeo,wale wotehawapo na sasa kuna wengine,na inaelekea itaendelea hivohivo.Sasa hivi kulitakiwa kuwe na upinzani thabiti,kiasi cha kufanya hata vijana wa sasa iwe ni rahisi kwao kuingia kwenye upinzani sio kwa sababu mtu anaichukia tu CCM au anajua hawezi kuendelea akiingia CCM,bali kujua kuwa anaweza kuleta maendeleo kwa nchi yake kupitia upinzani.
  Tutasema hapa kuwa ujamaa was wrong,lakini wengi huko nyuma ukisoma wanasema ujamaa was right,lakini implemetation was wrong.
   
Loading...