Kuna mahali Malisa GJ amekosea

Ukiona mtu hajatoa hoja badala yake amekimbilia matusi tilia mashaka elimu yake. May be ni darasa la saba ndio maana akikaa seat moja na piece kali anaona big deal !! Shame
haaaa haaa ilikuuma sana kukaa sit moja na pisi kali? Go Malisa Go
 
Amefanyaje tena?.Amepoteza #Atlanta# yake?

Naam wanajamvi,

Leo katika pitapita zangu mitandaoni nikakutana na post ya huyu maarufu Malisa GJ ameandika mambo machache kuhusu follower wake mmoja kum block kisa ameudhika na ushabiki wake kwa Simba Sports Club. Kwahiyo huyo follower pamoja na kum-block akaongeza kuwa hata changia tena zile challenges zake(?)!

Kimsingi huyu ' follower' amekosea, Lakini Malisa GJ amekosea zaidi. Kwanini? Kuwa mnazi wa timu ya mpira au mwanamzi au bendi fulani ya mziki siyo dhambi hata kidogo. Ila alipo kosea Malisa GJ ni hapa; Kwa sasa Malisa GJ nafasi yake katika jamii ni kubwa mno! Kuna ma milioni ya watanzania wanamuona kama noble person, kifupi ana admirers wengi wadogo kwa Wa kubwa, wenye Imani za dini tofauti na wasio na Imani za dini kabisa,wanasiasa na wasio wanasiasa. Wote ni admirers wake. Kwao wao yeye ni ikon yao.

Malisa GJ ni kama mwana mfalme aliyetakiwa kuwa Mfalme at 12! Ukisha kuwa mfalme katika umri mdogo huu ni lazima uwe mkubwa ghafla. Kuna mambo utatakiwa uyaache upende usipende. Unafikiri una nafasi tena ya kusema nataka nile ujana? Huna nafasi hiyo tena. Sasa Malisa GJ, Mungu amekujalia Atlanta ya pekee katika jamii ya watanzania, wamekuamini kupindukia. Miongoni mwao wapo wanazi wa mpira, wenye akili na wasio na akili , wanaume na wanawake, wote ni followers na ni admirers wako! Ni kundi lako na wewe ndio mfalme wao. Unatakiwa uuelewe ujumbe wa aliye ku-block kuwa ukiwa mfalme hata katika umri mdogo Wa miaka 12 hutakuwa na nafasi ya kula ujana wako.

Ushauri wangu ni kwamba kamwe usipoteze follower wako hata mmoja kwasababu za kushabikia Simba au Yanga. You are now a King at 12, acha mambo mengine yapite hutapungukiwa na kitu.

Unajua baada ya Reginald Mengi kufariki na Lions club kutokuwa active enough , wewe ndio tegemeo la wenye shida mbali mbali kupitia michango ya followers wako? TAFAKARI
Hiki ndo alichoakiandika Malisa:-
Huyu ndugu simfahamu, lakini amenitext whatsapp akidai ushabiki wangu wa mpira umemkera hivyo kaamua kuniblock. Kwa maelezo yake inaonekana ni mfuasi wangu, ndio maana ameweza kuwa na namba yangu na kunitext. Naomba niseme machache;
1. Ushabiki wa mpira sio uadui. Kuna watu bado hawajui kutofautisha kati ya ushabiki/ufuasi na uadui. Yani mkitofautiana timu za mpira au vyama vya siasa anakuchukia. Anatangaza uadui. Huo ni USHAMBA na ULIMBUKENI.
Mimi ni Simba lakini familia yangu yote ni Yanga. Baba, mama na ndugu zangu wengine. Wakati wa utoto wetu Yanga wakishinda nyumba nzima inanitania mimi, Nakua mnyonge sana. Lakini Simba ikishinda mimi nawatania wote, naleta fujo nyumba nzima. Tunacheka, tunafurahi, maisha yanaendelea.
Hii ndio maana ya utani wa jadi. Lakini kumchukia mtu kwa sababu eti anashabikia timu usiyoipenda, huo ni Ulimbukeni. Tusilazimishe kutengeneza maadui bila sababu, mpira ni furaha, mpira ni starehe. Ukishinda shangilia hadi uwakere wengine, na ukishindwa vumilia kutaniwa lakini usitengeneze uadui.
2. Huyu ndugu anasema hatachangia tena challenge zangu kwa sababu eti nashabikia Simba. Huu ni utoto, na kama ni mtu mzima basi bado hajakomaa akili. Challenge za kusaidia watanzania na ushabiki wangu kwa Simba vina uhusiano gani? And infact hanichangii mimi, anachangia watanzania wenye uhitaji. Kwahiyo hanikomoi mimi, anakomoa yatima, wajane, maskini na wagonjwa wanaosaidiwa kupitia ukurasa huu. Kama anasoma ujumbe huu hapa anaweza kujiona alivyo na ujinga mwingi.
3. Maisha yetu ni mafupi sana hapa duniani. Tujitahidi kuishi kwa kutengeneza marafiki wengi watakaotulilia siku ya mwisho sio kutengeneza maadui. Adolph Hittler aliwahi kusema "ukilazimika kutengeneza adui basi hakikisha unakua na sababu za msingi".
Mtu awe adui yako kwa sababu labda alimuua mzazi wako, au alichoma moto nyumba yenu. Sio unatangaza uadui na mtu eti kwa sababu anashabikia timu usiyoipenda. Jinga kabisa.!
Maisha yana stress nyingi. Stress za kazi, stress za pesa, stress za mapenzi, halafu bado unajipa tena stress kwa sababu eti fulani anashabikia timu tofauti na wewe? Una wazimu.!!
May be an image of text that says 'TODAY Messages and calls are end-to-end encrypted. No one outside of this chat, not even WhatsApp, can read or listen to them. Tap to learn more. 1 UNREAD MESSAGE Kaka nilikua nakueshimu sana kwa kaxi kubwa unayofanya kwenye jamii lakini ushabiki wako kwenye mpira sijaupenda nakublock na challenge zako sichangii tena. 21:40'

Mimi nadhani Malisa ana maisha yake nje ya kazi anazofanya, na huyu follower atambue kuwa Malisa amekuwa asaidii wana Simba bali watanzania wote, mashabiki wa Simba, Yanga na hata wasiokuwa na timu. Kumblock kwa sababu ya kuwa shabiki wa Simba na kuapa kutasoidia watanzania wenzako ni Ulimbukeni
 
Back
Top Bottom