Kuna madhara yoyote ya kutokudhibiti bei ya vyakula kupanda?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,267
33,871
Kuwaachia wakulima na walanguzi kuuza vyakula kwa bei zinazowapendeza wao, kuna madhara yoyote kiuchumi ama kijamii kwa Taifa letu kiujumla?
 
Lakini inasemwa kutesa kwa zamu na leo ni zamu ya wakulima kutesa!!
Consumer hasa wanapokuwa masikini wana tabia ya kupunguza consmption vyakula vinapozidi bei kwa hiyo atatoka milo 3 mpaka 2 au milo 2 mpaka 1 au mlo 1 mpakanusu mlo kwa siku. Matokeo yake season inayofata wanakuwa wameshajiwekea kuwa hiyo ndiyo routine yao as a result mauzo yanapunguwa. Wakulima mazao yanawaozea.
 
Consumer hasa wanapokuwa masikini wana tabia ya kupunguza consmption vyakula vinapozidi bei kwa hiyo atatoka milo 3 mpaka 2 au milo 2 mpaka 1 au mlo 1 mpakanusu mlo kwa siku. Matokeo yake season inayofata wanakuwa wameshajiwekea kuwa hiyo ndiyo routine yao as a result mauzo yanapunguwa. Wakulima mazao yanawaozea.
Kuna soko kubwa sana la Mahindi Rwanda, Burundi na Kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuruhusu mbolea za viwandani, madawa na zana za kilimo kupanda bei kupelekea gharama za mkulima kupanda then tunataka bei ya mazao yake isipande, madhara makubwa sana kwa mkulima wakidhibiti bei ya mazao ya chakula kupanda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini inasemwa kutesa kwa zamu na leo ni zamu ya wakulima kutesa!!
Hakuna mkulima anaenufaika na bei ya sasa kama wapo ni wachache sana hawafiki hata 30% ya wakulima. Wanaonufaika kwa sasa ni wafanyabiashara wanaoweka vyakula mfn mchele, mahindi na maharage katika maghala na kuuza kipindi hiki cha upungufu wa chakula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika aina mbalimbali za uchumi, swala la kumlinda mlaji, mzalishaji na mfanyabiashara ni la muhinu sana.
Serikali kazi yake ni ku regulate mfumo mzima wa shughili zozote za kiuchumi zinazofanywa na watu.
Swala la Bei ya mazao au bidhaa muhimu katika Inchi ni lazima ziwe regulated na Serikali ili kuwe na hali ya usalama Inchini.
Wanafalsafa husema " You win the people through their stomack"
Unaweza kuwapata na kuwaongoza watu wakiwa wameshiba vizuri.
Watoto wako wanaweza kuwa wanalala njaa lakini hawasemi ila siku ukiwa huna nguvu nao watakusuta na kukuambia kuwa ulikuwa unawashindisha na njaa.
Inchi kama za ujamaa hutoa pesa ili kumlipa muuzaji apate kuwauzia wanainchi bidhaa kwa pei ya chini (subsidize) .
 
Na bado mkuu Allen ! Bei hii unayoiona inapanda itafika Siku utakuta hapo iringa kwenye soko la magarimabovu au mashine tatu anayeweza kununua mboga ya magulumeru ni ASAS tu ! Kuna kitu sio cha kawaida kinaendelea katika masoko ya mazao yaani wanapokutana mzalishaji,muuzaji na mnunuaji. Chama cha mafisi Wacha watuchezee sisi mafala kwenye mabox ya kupigia kura Ila wasicheze na wafanya biashara wanaakili sana hao! Na kuhakikishia kabla ya uchaguzi mkuu hii sirikali ya fisiemu itabweka tu kilio cha mbwa mwizi.Mimi Kimenikera sana kile kibwanyenye bashe kinawaambia Jirani zenu hapo iringa watu wa Njombe eti kinasema ukiona unga unapanda bei nenda kapike wali au chips . kuna Siku itafika sio muda mrefu kuanzia sasa Allen wanafisiemu wakiona fuso imepakia hata nyanya watashangilia na kusema awamu ya tano inatekeleza na fuso hiyo ya nyanya ikifika sokoni mwenye ubavu Wa kununua hiyo nyanya kama huko DSM atakuwa mo au,manji tu
 
Kwani n lini wakulima walikuwa wanapangiwa bei!!? Navofahamu n kwamba bei huwa inajipanga yenyewe sokon...formula n simple tu kwamba ukiwepo upatikanaj mwing wa kitu bei hushuka yenyewe na ukiwepo uhaba bei hupanda sa hayo mambo ya mkulima kupanga bei yanatoka wap!! Mazao yenye bei elekezi n machache mnoo mfno pamba n.k
Kuwaachia wakulima na walanguzi kuuza vyakula kwa bei zinazowapendeza wao, kuna madhara yoyote kiuchumi ama kijamii kwa Taifa letu kiujumla?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom