Salama wakubwa wa JamiiCheck?
Katika pitapita zangu mitandaoni kuna mtu nimeona akishauri kuwa ni vizuri kumnyoa mtoto mchanga nywele alizozaliwa nazo ili mtoto akue vizuri.
Amedai kuwa mtoto asiponyolewa nywele hizo anaweza pata madhara ya ngozi ya kichwa, ukuaji duni lakini mwisho ni mambo ya kiimani.
Binafsi nipo njiapanda maana nimekuwa nikiona watoto wengine wakinyolewa ndani ya wiki moja baada ya kuzaliwa, lakini wengine hawajawahi guswa nywele zao mpaka wanakuwa wakubwa.

- Tunachokijua
- Nywele ni nyuzi za protini zinayokua kutoka kwa follicles iliyopatikana kwenye ngozi. Nywele ni moja ya sifa zinazoelezea wanyama. Mwili wa binadamu, mbali na maeneo ya ngozi ya glabrous, hufunikwa kwa follicles ambayo hutoa terminal nyembamba na velusi nzuri nywele. Nia ya kawaida ya nywele imezingatia ukuaji wa nywele, aina ya nywele na huduma za nywele, lakini nywele pia ni muhimu sana hujumuisha protini, hasa alpha-keratin.
Kumekuwa na taarifa zinazodai mtoto mchanga akizaliwa lazima anyolewe nywele alilozaliwa nazo, na asiponyolewa nywele hizo anaweza pata madhara ya ngozi ya kichwa, ukuaji duni nk
Je, ukweli ni Upi?
JamiiCheck imemtafuta Dkt. Remigius Thadeo, Registrar Idara ya Watoto Muhimbili National Hospital ambaye amekanusha kuwa hakuna madhara yoyote anayoweza kuyapata mtoto iwapo asiponyolewa nywele alizozaliwa nazo.
"Suala la mtoto kuzaliwa kisha iwe ni lazima kunyolewa nywele hilo ni suala la imani tu hakuna ushahidi wa kisayansi wowote ambao unaeleza kuwa suala hilo linatakiwa kufanyika.
Mtoto anaweza kuzaliwa na akaishi maisha yake vizuri bila kunyoa nywele, suala hilo lilitumiwa labda na watu wa Jamii fulani au imani fulani kwa sababu zao na siyo sababu za kitaalam"
Aidha, kupitia machapisho mbalimbali nayo yameunga mkono kuwa hoja zinazodai ukiacha kumnyoa mtoto mchanga nywele alizozaliwa nazo atapata madhara hazina ukweli, wengi wanodi hivyo wanakuwa na mtazamo w kiimani na hakuna uthibitisho w kisayansi kuhusu kuwepo kwa madhara yoyote yale iwapo nywele hizo zikiachwa zikue bila kukatwa.