incredible terminator
JF-Expert Member
- Aug 1, 2016
- 2,229
- 3,524
Habari Wakuu, kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu, Nimejikuta nimekuwa mlevi wa kufuatilia mada za kiroho hasa zinazohusiana na masuala ya kishirikina huwa napenda kusikiliza na kujua mambo yakishirikina yanafanyikaje,
Zaidi nimejikuta hadi naingia YouTube kutafta simulizi za kusisimua na za kutisha ambazo zina ukweli zinazohusisha shuhuda za watu mbalimbali ambao waliwahi kutumika au kutumia nguvu za kichawi na kishetani na baadae wakaacha, huwa napenda kusikiliza simulizi hizo maana huwa wao wanasimulia mambo mengi sana,
Yaani nimekuwa mlevi wa simulizi za aina hizi hadi kuna marafiki zangu huwa wananikataza kuwa naweza kujikuta nakuwa mchawi kwa kufuatilia sana habari za kishirikina, huwa ninatabia ya kuingia YouTube natafta simulizi nyingi na kuzisave offline alafu nikimaliza nazima data naweka headfone nasikiliza kuanzia asubuhi hadi jioni, lakini licha ya kusikiliza simulizi nyingi na zakutisha ila cha ajabu huwa siogopi wala kushtuka hata nikiwa peke yangu, hakika huwa nafurahia sana hasa ninaposikia wakisimulia namna walivyokutana na nguvu ya mungu, kuna mda huwa napata nguvu na mawazo ya kutamani kumtumikia mungu huku nikiamini kwa mungu nitakuwa sehemu salama lakini cha ajabu kila nikipanga kwenda kanisani nashindwa, Kibaya nimeenda mbali zaidi katika simulizi hizi nimejikuta kulingana na mambo ninayosikia kupitia simulizi inanisaidia kujua baadhi ya hali flani ambazo sio za kikawaida hasa nikikutana nazo huwa ninahisi kulingana na baadhi ya simulizi nilizowahi kusikia baadhi ya watu wakielezea namna ya kutambua MTU ambae si wa kawaida na MTU ambae ni wa kawaida, lakini zaidi kinachonipa wasiwasi nimejikuta naanza kuogoa kila mzee anaekatiza mbele yangu huwa napata picha flani inajengeka kichwani mwangu ya mambo ninayoyasikia katika simulizi mbalimbali,
Nimejitahidi sana kuacha kusikiliza simulizi za namna hii na kufuatilia machapisho yanayohusu ushirikina lakini nimeshindwa kabisa yaani nikikaa bila kusikiliza huwa naskia hali ya msukumo inanituma nitafte simulizi za shuhuda za mambo ya kutisha nisikilize,
Ninachoomba kujua kwa wazoefu vipi kuna madhara yotote ninaweza kupata? Au ni namna gani naweza kuepuka huu uraibu?
Hizi ni baadhi ya simulizi nilizowahi kufuatilia