Kuna madhara gani kuweka kitu cha moto kwenye friji

NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
917
1,198
Hususan chakula kama wali au chai ili ipoe kidogo? Maana yake ndio zangu kama nina haraka. Kuna madhara gani kuweka kitu cha moto kwa friji?
 
Hususan chakula
Kama wali au Chai ili ipoe kidogo.

Manake ndo zangu kama nina haraka.

Kuna madhara gani kuweka kitu cha moto kwa friji.?
Haitaharibika ila matumizi ya umeme yatakuwa makubwa bure. Ndio sababu kubwa, nyingine ni uwezekano wa joto kupanda ndani ya friji na kusababisha vitu vingine vilivyomo kupata joto.
 
Kwanza kitu cha moto kinaongeza joto ndani ya friji na kusababisha ile sensor ione joto lipo juu na na kusababisha compressor izunguke muda mrefu na kuichosha comoressor na kula umeme mwingi.

Kitu cha moto kinatoa mvuke mwingi ambao unasababisha unyevu mwingi sana ndani ya friji ambao matokeo yake inasababisha barafu nyingi sana.
 
Kwanza kitu cha moto kinaongeza joto ndani ya friji na kusababisha ile sensor ione joto lipo juu na na kusababisha compressor izunguke muda mrefu na kuichosha comoressor na kula umeme mwingi.

Kitu cha moto kinatoa mvuke mwingi ambao unasababisha unyevu mwingi sana ndani ya friji ambao matokeo yake inasababisha barafu nyingi sana
Asante
 
Back
Top Bottom