Kuna maana yeyote kubadili jina kwa mwanamke??

gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,274
20,670
Wanajamvi,
hivi kuna maana yeyote kwa mwanamke kubadili jina lake la ubini na kuitwa kwa jina la ubini wa mume??
je kwakufaya hivyo inamaana kwamba wzazi wa watoto wa kike hawana sifa waipatayo kwa mafanikio ya watoto wao??

sijui kama nimeeleweka lkn kimfano iko hivi mimi gfsonwin nilizaliwa nikaitwa gfsonwin Massawe, sasa leo nimeolewa na Kaizer niitwe gfsonwin Kaizer. je inamaana yyte kuitwa hivyo?? na kama ndio je huko si kuwanyima wazazi wa mtoto wa kike haki yao ya kumili huyo mtoto??
 
Last edited by a moderator:
kaulize kwa nini mwanaume hafanyiwi sendoff?au kwa nini hatolewi mahari?na kwa nini watoto wenu hawatumii jina la ubini wa mwanamke??

sasa wataa kusema sendoff ndio sababu au kutolewa mahari?? je inamaanisha india ambako wanawake ndio hutoa mhari basi wanaume waitwe kwa ubini wa kike??
lkn kama nilishaitwa kwa ubini wa baba yangu why shld i change now eti kisa ni mke wa mtu??
 
Binafsi sijaona sheria inayolazimisha hayo. Nadhani ni tamaduni tu katika kuifanya iwe familia moja na sioni kama kuna ubaya. Au wewe hupendi?
 
maana? ipo......
wewe sasa unakuwa mke wa ........, kwa hiyo unavyobadili jina unatoka jina la usichana wako na kuitwa mke wa fulani.
na ndo maana kama unatumia jina la mume, officially inatakiwa liazwe na Mrs. na siyo kuanza jina tu.
Ila kwa upande wangu mimi naona ni ngumu kidogo kubadili jina la ukoo. kutokana na mazingira ya kazi na kusoma, sawa kuna mambo ya kisheria yanazingatiwa lakini kuna kausumbufu fulani kanaendelea.
Jana nilimsoma staa mmoja alikuwa anatangaza sasa ameshabadili surname yake na kurudia ya usichana wake na yupo tayari kuolewa na mume mwingine, lol! hapo sasa. ndoa za siku hizi ni za siku 3, umebadilisha kila kitu chako unaitwa Mrs fulani, kesho mmeachana unahangaika tena mahakamani kurudisha jina lako na kupata jina la mume mwingine...... inasumbua sana.
Mimi nilikaa na mume wangu tukaongea na hatukuona sababu ya mimi kubadilisha jina. Ingawa watu wooote hata ofisini wananiita kwa jina la Mrs fulani, lakini officially natumia Ms fulani. mambo yanaenda, na najijua kuwa mimi ni mke wa fulani.
 
Ni sawa kuitwa gfsonwin Massawe na pia kuitwa hivyo lina maana yake.

Kipindi ukiwa bado haujaolewa uliitwa Gfsonwin Massawe kwasababu ulikuwa kwenye himaya ya Massawe(yaani ulikuwa chini ya mamlaka ya baba yako) na sasa unaitwa gfsonwin Kaizer kwasababu upo kwenye himaya ya Kaizer(yaani mumeo).
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi,
hivi kuna maana yeyote kwa mwanamke kubadili jina lake la ubini na kuitwa kwa jina la ubini wa mume??
je kwakufaya hivyo inamaana kwamba wzazi wa watoto wa kike hawana sifa waipatayo kwa mafanikio ya watoto wao??

sijui kama nimeeleweka lkn kimfano iko hivi mimi gfsonwin nilizaliwa nikaitwa gfsonwin Massawe, sasa leo nimeolewa na Kaizer niitwe gfsonwin Kaizer. je inamaana yyte kuitwa hivyo?? na kama ndio je huko si kuwanyima wazazi wa mtoto wa kike haki yao ya kumili huyo mtoto??

Ni muendelezo wa mfumo dume Duniani, na sidhani kama Rasimu ya katiba imegusia hili pia!!!
 
maana? ipo......
wewe sasa unakuwa mke wa ........, kwa hiyo unavyobadili jina unatoka jina la usichana wako na kuitwa mke wa fulani.
na ndo maana kama unatumia jina la mume, officially inatakiwa liazwe na Mrs. na siyo kuanza jina tu.
Ila kwa upande wangu mimi naona ni ngumu kidogo kubadili jina la ukoo. kutokana na mazingira ya kazi na kusoma, sawa kuna mambo ya kisheria yanazingatiwa lakini kuna kausumbufu fulani kanaendelea.
Jana nilimsoma staa mmoja alikuwa anatangaza sasa ameshabadili surname yake na kurudia ya usichana wake na yupo tayari kuolewa na mume mwingine, lol! hapo sasa. ndoa za siku hizi ni za siku 3, umebadilisha kila kitu chako unaitwa Mrs fulani, kesho mmeachana unahangaika tena mahakamani kurudisha jina lako na kupata jina la mume mwingine...... inasumbua sana.
Mimi nilikaa na mume wangu tukaongea na hatukuona sababu ya mimi kubadilisha jina. Ingawa watu wooote hata ofisini wananiita kwa jina la Mrs fulani, lakini officially natumia Ms fulani. mambo yanaenda, na najijua kuwa mimi ni mke wa fulani.

ukweli ni kwamba kwa waajiriwa kubadili ubini naona kama ni njia ya kupata stahili zako tu like hela za likizo na uhamisho nk. jambo ambalo nafikiri hata bila kubadili jina lako unaweza kupatiwa so long as una evidence i.e certificates

sasa linakuja swla pale ambapo prestige imeongezeka mzazi wako ama mume yupi utakaye mpa priority?? mfano leo hii FP ni Ms. lakini kesho keshokutwa umekuw Dr... je utaitwa kwa ubini upi?? kuna mdada mmoja hapa ofsn kwetu anapata wakati mgumu sana hadi nikamjibu ajiite jina tofauti kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Ni muendelezo wa mfumo dume Duniani, na sidhani kama Rasimu ya katiba imegusia hili pia!!!

sina hakika manake hata rasimu yenyewe sijaipitia vyema ila tu mimi nimeangalia kutoka kwenye mfumo ambao niliajiriwa nao.
 
Wanajamvi,
hivi kuna maana yeyote kwa mwanamke kubadili jina lake la ubini na kuitwa kwa jina la ubini wa mume??
je kwakufaya hivyo inamaana kwamba wzazi wa watoto wa kike hawana sifa waipatayo kwa mafanikio ya watoto wao??

sijui kama nimeeleweka lkn kimfano iko hivi mimi gfsonwin nilizaliwa nikaitwa gfsonwin Massawe, sasa leo nimeolewa na Kaizer niitwe gfsonwin Kaizer. je inamaana yyte kuitwa hivyo?? na kama ndio je huko si kuwanyima wazazi wa mtoto wa kike haki yao ya kumili huyo mtoto??

Katika haki za binadamu unauhuru wa kutumia jina unalolipenda wewe, hata kama umeolewa na hutaki kutumia ubin wa mume wako. Kwa upande mwingine, ukiwa umeolewa na mume let say anaitwa 'Mr Kinyago', wewe kuwa Mrs Kinyago na watoto wenu Ally Kinyago, Beatrice Kinyago, Maajabu Kinyago ni inarahisisha kuiaddress familia ya Mr Kinyago. Kwa mfano tu mnaomba visa kama familia ni rahisi familia kuwa addressed.

Waganda hawatumii ubin wa baba, inatokea watoto wa famili moja lakini kila mtoto anaubin wake. Rafiki yangu mganda nilisoma nae UK, alitaka kumwalika kaka yake aje kumtembelea, alikataliwa visa na ubalozi wa UK Kampla kwakuw hawakuamini kuwa hawa watu ni ndugu. Alipewa baada ya kuapeal.

Sijatoka nje ya mada lakini ninaelezea in a different angle.
 
Hata kama ni kutaka haki sawa sasa naona mnataka kuvuka mipaka kabisa!!!!

Hapo sasa dada gfsonwin naona mnataka kufanya watu wote waonekane ni ma-liberal.

Mfano ukute mtu anaitwa Juma Halima Mwanahamisi undhani litakuwa linaleta maana au mtu huyo ataoneana ndivyo sivyo?

Muda mwibgine tuache tu mambo kama yalivyokuwa, ninyi kutoka ubavuni kwetu isiwe sababu.

kaka yangu saudari mimi sijasema watu waitwe kwa ubini wa kike la hasha manake hiyo ni topic nyingine ila sasa nataka tu kujua mantiki ya kubadili jina kama ipo yaani kutoka kuitwa jina la baba yangu hadi kwenda kuitwa jina la mume wangu.
 
Last edited by a moderator:
Katika haki za binadamu unauhuru wa kutumia jina unalolipenda wewe, hata kama umeolewa na hutaki kutumia ubin wa mume wako. Kwa upande mwingine, ukiwa umeolewa na mume let say anaitwa 'Mr Kinyago', wewe kuwa Mrs Kinyago na watoto wenu Ally Kinyago, Beatrice Kinyago, Maajabu Kinyago ni inarahisisha kuiaddress familia ya Mr Kinyago. Kwa mfano tu mnaomba visa kama familia ni rahisi familia kuwa addressed.

Waganda hawatumii ubin wa baba, inatokea watoto wa famili moja lakini kila mtoto anaubin wake. Rafiki yangu mganda nilisoma nae UK, alitaka kumwalika kaka yake aje kumtembelea, alikataliwa visa na ubalozi wa UK Kampla kwakuw hawakuamini kuwa hawa watu ni ndugu. Alipewa baada ya kuapeal.

Sijatoka nje ya mada lakini ninaelezea in a different angle.
ok sasa nimekuelewa ila naona kama bado kuna ugumu sana ambao unatulazimisha indirect kuitwa kwa ubini wa mume.
turudi hapo hapo ninamaanisha kwamba mimi gfsonwin Massawe nikitaka kupata passport nikamtembelee Kaizer mume wangu lazima niwe ninasomeka kwamba ni Mrs gfsonwin Kaizer??

kwanini vyeti vya ndoa visisimame kuhakiki hilo??
 
Last edited by a moderator:
ukweli ni kwamba kwa waajiriwa kubadili ubini naona kama ni njia ya kupata stahili zako tu like hela za likizo na uhamisho nk. jambo ambalo nafikiri hata bila kubadili jina lako unaweza kupatiwa so long as una evidence i.e certificates

sasa linakuja swla pale ambapo prestige imeongezeka mzazi wako ama mume yupi utakaye mpa priority?? mfano leo hii FP ni Ms. lakini kesho keshokutwa umekuw Dr... je utaitwa kwa ubini upi?? kuna mdada mmoja hapa ofsn kwetu anapata wakati mgumu sana hadi nikamjibu ajiite jina tofauti kabisa.
hapo kwenye RED siyo lazima ubadili ubini.
unachotakiwa kufanya ni kupeleka cheti cha ndoa na vyeti vya watoto kwa ajili ya kupata stahili za watoto.
mimi sijabadili ubini ila cheti cha ndoa nilipeleka kwa hiyo huwa napata stahili za mume wangu kila likizo.
prestige? yaani wajibebe kwa mgongo wangu? lol!
kama nilivyosema tangu mwanzo tulikubaliana nitabaki na jina la ubini wangu, kiofisi. ingawa hata sasa ukifika kwa ofisi yangu ukaniulizia kwa ubini wowote (wangu au wa mume wangu) unanipata. kwa watu napenda kujitambulisha naitwa fulani binti fulani, au mrs fulani, kwa hiyo utakaloona linakupendeza kuniita I am fine. Ila kwenye ma-document ndo utakuta ubini wa babangu
 
Katika haki za binadamu unauhuru wa kutumia jina unalolipenda wewe, hata kama umeolewa na hutaki kutumia ubin wa mume wako. Kwa upande mwingine, ukiwa umeolewa na mume let say anaitwa 'Mr Kinyago', wewe kuwa Mrs Kinyago na watoto wenu Ally Kinyago, Beatrice Kinyago, Maajabu Kinyago ni inarahisisha kuiaddress familia ya Mr Kinyago. Kwa mfano tu mnaomba visa kama familia ni rahisi familia kuwa addressed.

Waganda hawatumii ubin wa baba, inatokea watoto wa famili moja lakini kila mtoto anaubin wake. Rafiki yangu mganda nilisoma nae UK, alitaka kumwalika kaka yake aje kumtembelea, alikataliwa visa na ubalozi wa UK Kampla kwakuw hawakuamini kuwa hawa watu ni ndugu. Alipewa baada ya kuapeal.

Sijatoka nje ya mada lakini ninaelezea in a different angle.
sijui balozi nyingine zinaangalia nini, lakini sijawahi pata hiyo shida.
wakati mwingine mume wangu anaposafiri au mimi nikisafiri kikazi huwa tunapenda kwenda pamoja.
hapo mtu ambaye ndo safari yake ya kiofisi anapata visa kirahisi kabisa, msindikizaji ndo lazima uelezee huyu ni mke/mume ananijoin. tuna surnames tofauti, lakini tunalindwa na cheti cha ndoa. Jina langu la kwenye passport yangu na jina la mume wangu kwenye passport yake ndo majina yetu kwenye cheti cha ndoa, kwa hiyo hatujawahi wala hata kuulizwa kwamba hatutumii surname moja
 
ok sasa nimekuelewa ila naona kama bado kuna ugumu sana ambao unatulazimisha indirect kuitwa kwa ubini wa mume.
turudi hapo hapo ninamaanisha kwamba mimi gfsonwin Massawe nikitaka kupata passport nikamtembelee Kaizer mume wangu lazima niwe ninasomeka kwamba ni Mrs gfsonwin Kaizer??

kwanini vyeti vya ndoa visisimame kuhakiki hilo??
siyo lazima, nisome post # 15
 
hapo kwenye RED siyo lazima ubadili ubini.
unachotakiwa kufanya ni kupeleka cheti cha ndoa na vyeti vya watoto kwa ajili ya kupata stahili za watoto.
mimi sijabadili ubini ila cheti cha ndoa nilipeleka kwa hiyo huwa napata stahili za mume wangu kila likizo.
prestige? yaani wajibebe kwa mgongo wangu? lol!
kama nilivyosema tangu mwanzo tulikubaliana nitabaki na jina la ubini wangu, kiofisi. ingawa hata sasa ukifika kwa ofisi yangu ukaniulizia kwa ubini wowote (wangu au wa mume wangu) unanipata. kwa watu napenda kujitambulisha naitwa fulani binti fulani, au mrs fulani, kwa hiyo utakaloona linakupendeza kuniita I am fine. Ila kwenye ma-document ndo utakuta ubini wa babangu

umenikumbusha miaka ile naanza kazi, nilijiita kwa ubini wa baba sasa ikaja wakati wa kulipwa subsistance allowance nikapata shida sana kwamba sijaolewa na kama ndio basi niitwe kwa jina mume........... aisee niligoma nilichofanya nilijiita majina yote yaani majina yangu mawili incluiding la ubini nilikozalika na la ubini wa mume sasa shuhudia hiyo mixed grill hapo utachoka lkn maisha yanenda
nakubali kuitwa Mrs fulan lakini siyo fulani binti ubini wa mume lol!
 
Wanajamvi,
hivi kuna maana yeyote kwa mwanamke kubadili jina lake la ubini na kuitwa kwa jina la ubini wa mume??
je kwakufaya hivyo inamaana kwamba wzazi wa watoto wa kike hawana sifa waipatayo kwa mafanikio ya watoto wao??

sijui kama nimeeleweka lkn kimfano iko hivi mimi gfsonwin nilizaliwa nikaitwa gfsonwin Massawe, sasa leo nimeolewa na Kaizer niitwe gfsonwin Kaizer. je inamaana yyte kuitwa hivyo?? na kama ndio je huko si kuwanyima wazazi wa mtoto wa kike haki yao ya kumili huyo mtoto??
Huwezi ukaitwa mrs massawe, sio? Utaitwa mrs kaizer. Kwa kiswahili mama kaizer... Automatically utajikuta mwenyewe ukijitambulisha kama mrs kaizer, na ukiambiwa taja mawili, utajikuta unasema gfsonwin kaizer... Hii inaapply zaidi kwenye utambulisho usio rasmi, lakini vyeti vyako, kazini kwako na sehemu nyingine rasmi utaendelea kuitwa dk massawe...lol
 
umenikumbusha miaka ile naanza kazi, nilijiita kwa ubini wa baba sasa ikaja wakati wa kulipwa subsistance allowance nikapata shida sana kwamba sijaolewa na kama ndio basi niitwe kwa jina mume........... aisee niligoma nilichofanya nilijiita majina yote yaani majina yangu mawili incluiding la ubini nilikozalika na la ubini wa mume sasa shuhudia hiyo mixed grill hapo utachoka lkn maisha yanenda
nakubali kuitwa Mrs fulan lakini siyo fulani binti ubini wa mume lol!
walikuonea, kwani hukupeleka cheti cha ndoa?
kwa nini wakulazimishe kutumia ubini ambao hujauandika?
 
Huwezi ukaitwa mrs massawe, sio? Utaitwa mrs kaizer. Kwa kiswahili mama kaizer... Automatically utajikuta mwenyewe ukijitambulisha kama mrs kaizer, na ukiambiwa taja mawili, utajikuta unasema gfsonwin kaizer... Hii inaapply zaidi kwenye utambulisho usio rasmi, lakini vyeti vyako, kazini kwako na sehemu nyingine rasmi utaendelea kuitwa dk massawe...lol
Point of correction: ataitwa mke wa Kaizer, siyo mama Kaizer..... Kaizer ana mamake ambaye siyo GFs
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom