Kuna maajabu kwenye undugu. Niko kijijini, Bibi yangu ananisimulia jinsi anavyomzimia Bujibuji wa JF

Hapana!
Ni mimi, lakini hiyo ID ilipotea baada ya zile emails za Yahoo kupata mushkeli miaka fulani. Bahati mbaya na email yangu ilikuwa mojawapo.
Nilifungua ID mpya ya Gwamahala Jr/GwamahalaJR.
I also like Bujibuji. Nami pia I hail from Mbeya but nimekulia usukumani kama Bujibuji tu, kijiji cha Iyengamulilo kisha baadaye Iparamasa.
 
Weekend oyeee (rejea kuku oyeee, jogoo oyee)

Leo nipo kijijini kwetu Garijembe, Mbeya vijijini. Nimekuja huku kumsabahi Bibi yangu na kuadhimisha maadhimisho ya Baridi la Taifa yanayofanyika kitaifa hapo Upoloto Namba Wani.

Baridi ni Kali Sana na leo tunachaeza na 2.1°C. Bibi yangu na miaka Yake 81, you buheri wa Afya njema na anaendelea vyema na kazi zake za kilimo, ufugaji na ufumaji wa masweta kwa kutumia sindano za tanitani.

Bibi yangu ni Mwalimu mstaafu na muda wake wa ziada huwa anabarizi kwenye mitandaoni mbalimbali ya kijamii ambako ame subscribe.

Miongoni mwa mitandao hiyo Ni pamoja na JamiiForums, Facebook na Twitter. Instagram haipendi kabisa anasema ana account huko lakini hainjoi.

Leo baada ya kupata mlo wa mchana, nikaona niingie mtandaoni, nikawa nacheka, akauliza. Gwamahala (ndilo jina langu halisi) unacheka Nini?

Nikamjibu Mambo tu ya mtandaoni yananichekesha, JF Kuna mtu anaomba ushauri, paka wake hadaki panya anaingiza tu madume ndani

Akaungana na Mimi kwenye kucheka, akasema, hebu tafuta comment ya Bujibuji kwenye uzi huo. (Hamna ndugu yangu yoyote anayejua kuwa kwamba Mimi ni Bujibuji, kwani hili jina lilikuwa la Mwalimu wetu enzi zile nasoma Nyambitilwa, Magu)

Nikamwambia Bujibuji hajachangia, akanitolea macho huku akifoka, huo uzi una kurasa zaidi ya mbili, IWEJE unasema Bujibuji hajachangia wakati hujapitia kurasa zote? (Nilikuwa najua ninachokiongea kwani sikuchangia neno kwenye uzi huo)

Nikaendelea kumsomea comments za watu mbalimbali Hadi uzi ukaisha. Akaanza kunipa story mbalimbali za Bujibuji, kwamba huwa anamchekesha Hadi wakati mwingine hutokwa na machozi ( kweli kabisa sijawahi maishani mwangu kujua au kuhisi kuwa comments zangu zinaweza kumfanya mtu kuwa follower wangu)
Akanielezea mengi hasa visanga, visa na Mikasa mbalimbali ya kwenye thread za Bujibuji.

Akaniambia anatamani Sana aje kukutana na Bujibuji ana kwa ana afanye naye mahojiano na wanywe chai ya maziwa ya kienyeji na mafufu na makatapera (ndizi mbivu za kuchoma na maparachichi)

Kwa namna nilivyo mpole na mkimya, nikamwambia Bibi, Mimi ndiye Bujibuji umsemaye.
Bibi huwa tunapenda kumwita Bishdo, akagoma kabisa, akaniambia wewe ulivyopooza hivyo utafikiri supu ilikosa ndimu, pilipili na chumvi huwezi kuwa Bujibuji.

Bujibuji anaonekana Ni mtu mwenye mahela Yake, ana magari, anakaa Dar Masaki, sio wewe umepanga kwa Ali MBOA Yombo.

Akanizodoa weee Hadi nkaanza kuboreka. Nikamuaga, nikamwambia naenda kuchuma mahindi nichome nichangamshe mdomo.

Hiyo ndio Kali ya Leo ya Bujibuji na Bishdo wake.
Ninayoijua mie ni Galijembe, hiyo Garijembe ni ipi?
 
Back
Top Bottom