Kuna la kujifunza kutoka kwa wadada wa kazi ( dini na maeneo wanayotoka iko nyuma kielelimu)

Status
Not open for further replies.

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Sina nia mbaya!
Lakini kwa muktadha wa nadharia!

Asilimia 40%-55% ya nyumba nyingi mijini zina dada wa kazi!
Hivyo katika kila nyumba 100 maana yake kuna wadada wa kazi 55 majumbani!

Hivyo katika makazi 10000 ya mji mmoja! Maana yake wapo wadada wa kazi takribani 55000 Hawaijui kesho yao kielimu na kimaisha!

Nataka kusema nini! Ni kwamba matokeo ya watoto hawa, ni malezi kutoka katika jamii walizotoka kuanzia Iman yao na mikoa yao kushindwa kuwaendeleza kielimu!

Je, ni dini gani hasa inaongoza kutoa wadada wa kaz majumbanii? Hapo utagundua lipo tatizo la mafundisho ya imani kiasi cha kuwatelekeza watoto kimalezi!
Pili iko mikoa inayoongoza kutoa wadada wa kazi, hili nalo ni tatizo la kikanda iko shida katika utoaji elimu kanda hizo!
Mila na destuli pia ni changamoto!

Lakini naomba kuishauri serikali Ione namna ya kuisimamia vyema ile sheria ya child labour ikiwezrkana iboreshwe ili kupunguza tatizo!

Kwa kuweka kipengele cha kuhakikisha watoto hawa wanaendelezwa! Pia mafundisho ya imani yasisitize pia elimu dunia!

Tuige mfano wa mkoa wa Kilimanjaro! Ingawa nako bado shida iko kidogo wilaya ya Rombo!

Kwasababu ukiona mdada wa kazi anatoka Kilimanjaro basi wengi wao hutoka Rombo/Tarakea na baadhi ya maeneo ya kishumundu
 
Kwanza nianze kwa kuonyesha masikitiko yangu kwa mtoa maoni wa kwanza, sanjali na hilo naomba niombe msamaha kwa yeyote atakayeumimzwa na maoni hayo.

Mkuu umeandika vema sana, umepangilia hoja zako vema na kwa mantiki nzuri, kwa kifupi umeonyesha uwezo wako mkubwa wa kufikiri na kuchambua mambo.

Binafsi naungana nawe kwa asilimia kubwa sana hasa kwenye upande wa baadhi ya kanda kujisahau sana ktk suala la kuwaendeleza watoto kielimu. Ni dhahiri kabisa kuna kanda ambazo wafanyakazi za ndani wengi hutokea. Nadhani sababu kubwa ni jamii kutoshiriki kwa pamoja ktk kuhimiza na kuendeleza watoto kielimu. Nakiri kabisa hili kwani naliona waziwazi hasa ktk ukanda naotokea mimi.

Mfano wa mkoa wa Kilimanjaro ni kweli kabisa jamii ya watu wake wanamwamko mkubwa kielimu na wanamuungano ktk kuendeleza watoto kielimu.

Upande wa dini, binafsi sina uhakika sana kwani kwa mtazamo wangu naona kama wafanyakazi kazi wa ndani wanatoka dini zote. Kwa hili nachelea sana kulitolea maoni.

Mwisho, naomba uzi wako uwe chachu kwa kila atakayeusoma, aone kabisa kwamba suala la malezi ya watoto ni suala la jamii nzima siyo familia tu. Binafsi sijisifii lakini nimejitahidi kuwawezesha watoto kadhaa kijijini napotokea kuendelea na masomo ya sekondari. Kama kila mmoja akimsaidia mtoto mmoja, basi tutajikuta tatizo hili tunalipunguza kama siyo kulimaliza kabisa.
 
Wadada wa kiislam hawapendi kutumikishwa,bora achome vitumbua au mandazi ila sio kuwa house girl,pili wadada wa kiislam sio rahisi kufanya kazi kwa wakristo wakihofia kulishwa kitimoto.familia nyingi za kiislam hazijitaji house girl maana wamama wengi wa kiislam ni house wives,wazanzibari na waarabu pekee ndio huweka house girl sababu .......wao,kuhusu ukanda,ukikuta mhaya amekuwa house girl ni nadra sana,wahehe wanamudu hiyo kazi sababu ni wavumilivu,mwisho wa yote dada wa kazi pia ni kazi kama zingine,tuwaheshimu
 
Kazi za ndani ni kazi kama zingine na inaweza kupewa heshima yake inayostahili na nadhani hicho ndo muhimu.

Kuipa hadhi na heshima. Domestic Managers( Househelps) are not lesser human beings.
 
Hata wakenya wamejaa Gulf countries kufanya kazi za ndan kwa waarabu mi sion kma Ni suala la kikabila wala dini ni umaskini wetu tu hakuna anaependa kuwa mtumwa kwenye makazi ya watu
Issue ni kuwa huko wanafanya kazi watu wazima huku watu wanachukua watoto.
 
Mwarabu alipokuja Tanganyika alijenga misikiti tu.

Mzungu alipokuja alijenga Kanisa na Shule.

Kamwe hao watu walioishi hapo hawawezi kufanana.
Ni kusahihisha, mwarabu alipokuwa Africa, Africa ilikuwa na nguvu kiuchumi, kijeshi na hata ki elimu. Mwarabu hakuondoa utawala wala kuingilia uongozi wa ki Africa

Mzungu kaja kuku kukufundisha umtegemee yeye, elimu ya Ki tegemezi, Africa iwe mzalishaji wa Raw material yeye atengeneze Bidhaa, kiongozi hawi mzuri hadi awe puppet na mengineyo.
 
Sina nia mbaya!
Lakini kwa muktadha wa nadharia!

Asilimia 40%-55% ya nyumba nyingi mijini zina dada wa kazi!
Hivyo katika kila nyumba 100 maana yake kuna wadada wa kazi 55 majumbani!

Hivyo katika makazi 10000 ya mji mmoja! Maana yake wapo wadada wa kazi takribani 55000 Hawaijui kesho yao kielimu na kimaisha!

Nataka kusema nini! Ni kwamba matokeo ya watoto hawa, ni malezi kutoka katika jamii walizotoka kuanzia Iman yao na mikoa yao kushindwa kuwaendeleza kielimu!

Je, ni dini gani hasa inaongoza kutoa wadada wa kaz majumbanii? Hapo utagundua lipo tatizo la mafundisho ya imani kiasi cha kuwatelekeza watoto kimalezi!
Pili iko mikoa inayoongoza kutoa wadada wa kazi, hili nalo ni tatizo la kikanda iko shida katika utoaji elimu kanda hizo!
Mila na destuli pia ni changamoto!

Lakini naomba kuishauri serikali Ione namna ya kuisimamia vyema ile sheria ya child labour ikiwezrkana iboreshwe ili kupunguza tatizo!

Kwa kuweka kipengele cha kuhakikisha watoto hawa wanaendelezwa! Pia mafundisho ya imani yasisitize pia elimu dunia!

Tuige mfano wa mkoa wa Kilimanjaro! Ingawa nako bado shida iko kidogo wilaya ya Rombo!

Kwasababu ukiona mdada wa kazi anatoka Kilimanjaro basi wengi wao hutoka Rombo/Tarakea na baadhi ya maeneo ya kishumundu

umekosea sana kusema dini !

kama umefika vijijini hii mada yako usingeongea !

kuna watu wanamaisha magumu utazani mungu kachukua ipod kusikiliza miziki kuliko familia za watu.

ukiwa unataka kujifunza pitia ndani ya ndani ya vijiji.

natembea sana mpaka nje ya nchi hata ulaya kuna watu ni maskini na unaweza kuoa mzungu au kuwa mfanyakazi wako na hapa tz wakashangaa kuwa ni house girl wako.

hata huyo mwarabu,mchina,mzungu na asia
 
Sina nia mbaya!
Lakini kwa muktadha wa nadharia!

Asilimia 40%-55% ya nyumba nyingi mijini zina dada wa kazi!
Hivyo katika kila nyumba 100 maana yake kuna wadada wa kazi 55 majumbani!

Hivyo katika makazi 10000 ya mji mmoja! Maana yake wapo wadada wa kazi takribani 55000 Hawaijui kesho yao kielimu na kimaisha!

Nataka kusema nini! Ni kwamba matokeo ya watoto hawa, ni malezi kutoka katika jamii walizotoka kuanzia Iman yao na mikoa yao kushindwa kuwaendeleza kielimu!

Je, ni dini gani hasa inaongoza kutoa wadada wa kaz majumbanii? Hapo utagundua lipo tatizo la mafundisho ya imani kiasi cha kuwatelekeza watoto kimalezi!
Pili iko mikoa inayoongoza kutoa wadada wa kazi, hili nalo ni tatizo la kikanda iko shida katika utoaji elimu kanda hizo!
Mila na destuli pia ni changamoto!

Lakini naomba kuishauri serikali Ione namna ya kuisimamia vyema ile sheria ya child labour ikiwezrkana iboreshwe ili kupunguza tatizo!

Kwa kuweka kipengele cha kuhakikisha watoto hawa wanaendelezwa! Pia mafundisho ya imani yasisitize pia elimu dunia!

Tuige mfano wa mkoa wa Kilimanjaro! Ingawa nako bado shida iko kidogo wilaya ya Rombo!

Kwasababu ukiona mdada wa kazi anatoka Kilimanjaro basi wengi wao hutoka Rombo/Tarakea na baadhi ya maeneo ya kishumundu
Kwamba Wachaga hawafanyi kazi za ndani sababu wamesoma? mbona wapo kibao wameajiriwa kulisha nguruwe!!
 
Iringa, Dodoma na Singida tunaongoza kwa kutoa mabeki tatu. Tunaomba mabosi muwalipe vizuri dada zetu.
Kazi mnawapigisha, mishahara hamuwalipi na matusi juu, siku wakiwafanyia tukio msianze kulialia kwenye vyombo vya habari.
 
Ametoa takwimu vizuri ila hii aliisahau, muhimu kukumbushana.
Tanzania waislam ni wengi kuliko wakristo, Kama umeishi kwenye baadhi ya majiji makubwa kma
Dar,Arusha, dodoma utagundua yamejaa sana waislam misikiti ipo kila mtaa, mtaa mmoja una misikiti hadi minne.
Kwahyo n lazma utakuta sample yao kila sehem japo watu wataangalia zaid katika udhaifu ambao kila binadam hajakamilika
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom