Ben Zen Tarot
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,177
- 7,301
Kuna mchezo unaendelea kwenye mitandao ya kijamii, na hasa facebook. kwangu mimi huu ni mchezo wa hatari sana kwa nafsi ya mtumiaji wa mitandao hasa wale ambao wanadhani shetani ni mpwa, shemeji, au swahina wa mwanadamu. Nitafafanua!
Mwaka jana na mwaka juzi niliwai kufundisha somo lenye kichwa "SIRI YA KUZIMU ILIYOJIFICHA NYUMA YA UTANDAWAZI"
Kwamba mitandao hii haipo tu kwasababu imeanzishwa kuunganisha watu, kama Mungu anavyoweza kuitumia na shetani vivyo hivyo. Kuna 'ma-genius' walikataa wakasimama kidete wakidhani ni hisia zangu tu, nikawaacha, nikakun'guta miguu yangu mavumbi nikawaacha waliposhupaza shingo zao, nikanawa mikono yangu.
Leo kuna kitu nataka kukisema hapa, kuna picha uwa zinatumwa kwenye mitandao, ni picha ambazo zinaweza kuonyesha mtu akiwa mgonjwa, au majeruhi, mlemavu au hata maiti kisha mtumaji atakutaka au u-like, ku-share au u-type amen.......!!
Kabla ya kufanya maamuzi hayo kuna mambo unapaswa kuyatafakari badala ya kukimbilia tu ku-like, ku-share, au ku-type amen.
1. Unapo-like maana yake umeipenda, lakini je unakuwa umeipendea nini picha iyo?
Umependa ugonjwa/majeraha/kifo/ulemavu wa mtu huyo kwenye picha?
Au je umempenda uyo mtu kwenye picha?
Usifanye jambo kabla ya kutafakari, fikiri kwanza unamaanisha nini kutoka kwenye vilindi vya moyo wako, otherwise hii ni mitego, kama huamini endelea na mwendo huo wa ku-like magonjwa, vifo au ulemavu wa wale unaowaona kwenye picha.
2. Ku-type Amen: Neno hili Amen ni neno lenye kumaanisha kukubali, Mara nyingi linatumika kuhitimisha sala au dua kuonyesha kwamba yale uliyoyaomba yawe hivyo kama ulivyoomba.
Hawa wanaosema uandike "Amen" kwenye picha ya mgonjwa, majeruhi au maiti wanatafuta nini kutoka kwako? Sio mtego huu?
3. Ku-share: kwa lugha ya ki-facebook ni kusambaza picha, video au taarifa kwa watumiaji wengine wa Facebook. Swali la kujiuliza hapa napo ni je, huyu anayekutaka usambaze iyo picha ya mauti, mgonjwa au majeruhi ni kweli lengo lake ni watu kupata taarifa? Ili iweje? Je lengo ni wewe kusambaza taarifa au usambazaji huo una agenda ingine ya siri nyuma yake???
4. Mwisho napenda uelewe kwamba kama uko makini picha nyingi za namna iyo zinahaririwa (edited), na wala sio picha halisi.
Sasa kama sio picha halisi, hawa watu wanapozituma na kukutaka wewe ku-share, ku-like au ku-type amen anatafuta nini kwako?
NIMEKUTAFAKARISHA TU , NI TAFAKURI....DUNIA INA MENGI NYUMA YA PAZIA! AKILI KICHWANI KWAKO!