Kuna kitu kinanitatiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna kitu kinanitatiza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kwaminchi, Jan 19, 2008.

 1. K

  Kwaminchi Senior Member

  #1
  Jan 19, 2008
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi ni Muislamu na Mwenyezi Mungu amenijaalia nimewahi kuhiji pia. Alhamdulillah.

  Siku moja nilimuuliza Sheikh, "masharti ya mtu kuwa Muislam ni yapi?" Akaniambia ni kukiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah peke yake na Muhammad SAW ni mtume na mjumbe wake.

  Sharti jingine ni kufuata yote yaliyoamrishwa na Mwenyewe Subhanahu Wataala na kuyaacha yaliyokatazwa Naye. Subhanallah!

  Nikamuuliza, "ni hayo tu?" Akanijibu, Naam, ni hayo tu. Nikamuuliza, "jina je, ni lazima nipewe jina la Kiislamu?" Akaniambia, hakuna jina la Kiislamu. Haya majina tuyatumiayo ni majina ya Kiarabu. Kuna Waarabu wasiokuwa Waislamu wanaitwa majina hayo hayo. Unamkumbuka Tariq Azizi? akaniuliza, nikamwambia ndio namkumbuka. Akaniambia, "hakuwa Muislamu yule.

  Sasa nikaanza kutatizwa hivi kwa nini sisi Waafrika tunaacha kutumia majina yetu ya Kiafrika, tunayapenda ya Kiarabu tukiwa ni Waislamu na ya Kizungu tukiwa ni Wakristo. Hii maana yake ni nini?

  Kwani Alhaj Kipesile Mwaitobo hawezi kuwa Muislamu au Reverend Kitogo Mazengo hawezi kuwa Mkristo? Mara nyingi ni sisi tu Waafrika. Wagiriki wana majina yao ya kigiriki na Wataliano wanatumia ya kwao ya kitaliano. Kwanini sisi mpaka tuwe George au Abdallah ndio iwe uthibitisho wa imani zetu za kiroho?
   
 2. mtuwawatu

  mtuwawatu Senior Member

  #2
  Jan 19, 2008
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  you i really hate my European name, i will change in the time to come
   
 3. M

  Mtu JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2008
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umenifurahisha sana kwa kuliona hilo
   
 4. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Yaani ndugu yangu kwa hili umenifurahisha sana. Nimekuwa nikiwanasihi wengi kuwa hakuna majina ya kikristo wala ya kiislamu, basi wao hunikatalia katakata. Nawauliza "ukisikia mtu anaitwa Gift Mlakunde utajua dini gani?" Wanajibu harakaharaka "Mkristo huyo!" Nashangaa, jamani mwislamu haruhusiwi kumwita mwanawe jina hilo (zawadi)? "Na akiitwa Abdullah je?" Najibiwa "mwislamu huyo!" Ama! Sasa mkristo wa Tunisia, Misri, Saudia, Iraq akitaka kumaanisha mwanae ni "mtumishi wa Mungu" atamwitaje? Na kuna watu wana kasumba kwamba mtu akiitwa "Silvester" basi ni mkristo zaidi kuliko "Songoro", au "Nassoro" ni mwislamu zaidi kuliko "Nkwabi". Tunatakiwa tujikomboe kwenye hali hii. Tumekubali imani, sawa, lakini sidhani kama Mungu alitaka tutupilie mbali kila kilichokuwa chetu (kwanza ni yeye mwenyewe Mungu aliyetupatia lugha na tamaduni mbalimbali). Haya mambo ya kuona kuwa vitu pamoja na majina yetu ya asili ni vya "kishenzi" ni wakoloni waliotupandikizia ili watutawale vizuri. Wazungu wakaamua mtu yeyote ambaye si mkristo wala mwislam ni "mpagani", makusudi tu ili kutudhalilisha. Nasi kwa unyonge wetu tukakubali na kuchukua majina yasiyo ya kipagani, ndio haya ya kiarabu na kizungu. Hatuitani majina ya kichina wala ya kihindi ingawa tunao wengi miongoni mwetu, tunajiita majina ya "mabosi" wetu ili tuwe karibu nao zaidi. Nikijitambulisha kwa mzungu najikoki "Hi, I'm Brian!". Siku moja uso ulinishuka mmoja alipotaka kujua jina hili lina maana gani kwangu. Hata mimi kwa kweli nitakuja badili hili jina, nasubiri tu nimalizie hiki cheti cha sasa hivi, nabadili once and for all!
   
 5. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kurudi kwenye majina ya kiasili ni vyema tukaanza kwa watoto zetu
  kwani suala la kubadili jina ukubwani itabidi uwe na cheti kingine kinachounganisha wewe wa jina jipya na yule anayeonekana katika vyeti vingine kwa mfano kuzaliwa,ndoa, elimu, ubatizo (kwa wale wamisheni) nk.

  lakini mobutu alifanya hivyo kwa nchi yake kwa kuanzia yeye joseph desire mobutu na kuwa mobutu seseseko kuku wa zabanga
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kubadili jina na kuwa la asili si kazi kubwa ni kwenda mahakamani..labda watu wa mahakama watueleze taratibu zikoje. ndio maana sie wengine tukachukua majina ya asili ya chuma...sio iron smith..!!!!
   
Loading...