Kuna kitu kinakufurahisha zaidi ya tendo la ndoa?

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,270
Kwa lile pila la yanga, leo sijala siku nzima

Wakuu aliwahi kusema mtu mmoja "Genius is someone who has discovered something more funnier than sex".sidhani kama Kuna neno moja la kiswahili linaweza kutafsiri ili neno genius kwahiyo ntaendelea kulitumia hivyo hivyo "Genius".

Tukisema genius ni neno pana sana, Kwa ufupi genius ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana Kwenye kulifanya jambo fulani ukilinganisha na binadam wengine wanavolifanya, hapa ni katika nyanja zote mpira,mziki, elimu, dini, utawala au falsafa, watu kama Lionel Messi, Albert Einstein,Tupac Shakur, Jesus Christ, Caesar na Prato Kila mmoja wao ni genius Kwenye field yake.

Turudi Kwenye nukuu yetu pale juu "Genius is someone who has discovered something more funnier than sex", kwamba genius ni mtu aliyegundua kitu kinachompa furaha zaidi ya tendo la ndoa, yani huyu mtu anashiriki tendo la ndoa na analifurahia lakini kuna kitu hicho yeye ndo kinampa furaha zaidi ya tendo la ndoa.

Historia inatuonyesha watu wengi sana waliofanikiwa katika historia walikuwa na "Mission" wanaipambania na walitumia Kila rasimali waliokuwa nayo kufanikisha hilo, baadhi walioa,kuolewa au kuwa na mahusiano ambayo Kwa ujumla hawakuyapa kipaumbele kama hiyo "Mission" wanayoipambania.

Hapa tunaongelea watu kama Prophet Muhammad, Jesus Christ, Alexander the great, Sir Isaac Newton, Albert Einstein, Mahatma Gandhi, Mother Terresia, Queen Elizabeth I,Thomas Edison, Nicola Tesla na watu kama hao, Kumbukumbu zinaonyesha Sir Isaac Newton alikufa bikraaaaaa.

Kwenye hii dunia yetu ya leo tunaishi kana kwamba mwisho wa siku tufanye mapenzi, tu-date, uwe na pisi Kali, utoke na mubaba, upate lishangazi, manzi apate sugar daddy,,like what the hell guys??what's wrong??

Yani tunaishi ila central purpose ya maisha yetu ni mahusiano ya kimapenzi, angalia harakati zetu za Kila siku alafu angalia mwisho wa hizo harakati ni nini utakuja kugundua ni mapenzi, ndo maana leo wanajichibua, wanachonga shape, wanakuza makalio, tunauziana dawa za kuongeza nguvu za kiume, mwanaume anapambana apate hata kagari ili aanze kuvuta pisi Kali, guys whats wrong, there is a lot to accomplish out there!!!!

Mapenzi ndio lengo kuu la kuvunja jasho, vijana wengi wa kiume Kwa wakike tunapambana Kwa hali na mali ila hayo mapambano yetu mwisho wa siku ni mapenzi, yaani mapenzi yamekuja kuwa ndio lengo kuu la maisha yetu,, don't you see something is wrong?

Mtu anajiuwa kisa mapenzi, yani mungu alikuumba na kukuweka tumboni mwa mama ako miezi tisa leo unakuja kujiua kisa mapenzi??, Kwa kifupi ulikuja kuishi Kwa sabab ya mapenzi kwakua leo hayo mapenzi umeyakosa basi na wewe huna sababu ya kuishi si ndio?.

Leo tumearibiana sana, wanawake wamewaaribu wanaume na wanaume wamewaaribu wanawake kisaikilojia, leo mwanamke akiwa amekonda Hana tako basi anatamani ata kufa akipita uko mtandaoni, kakiwa kafupi ndio kabisa hakana raha wanaume nao Kuna vibamia na nguvu za kiume, yani wanawake wanataka performance ya kiwango cha wacheza video za ngona unless otherwise huna nguvu, wanataka mjegeje ulefu mithiri ya jembe unless otherwise una kibamia, ukiangalia Kwa upana hamna Cha maana tunatesana kisaikilojia na tukiangalia sababu za msingi hatuzikuti.

Bora wanawake wanaweza kuishi bila "MISSION" kwenye haya maisha au mission yake ndio ikawa hiyo "MAPENZI" ila mtoto wa kiume

YOU SHOULD HAVE A MISSION TO ACCOMPLISH, kitu ambacho kinakufanya Kila siku husilale, kitu ambacho unaamini hata ukizeeka leo ukiangalia nyuma kutakuwa na kumbukumbu za kufurahisha, kitu ambacho hata ukifa leo chenyewe kitaishi milele.

Kitu ambacho kina kupa furaha kuzidi tendo la ndoa, kitu ambacho kitakufanya hata uachane na mapenzi kama yakiwa ni kikwazo katika kukifanikisha.

Legacy, something extraordinary, kama unataka kutuletea kiwanda Cha kwanza Cha simu Tanzania fanyia kazi ndoto yako sio unalialia na mapenzi Kama mtoto wa kike, kama unataka ujenge hospital za private Kila mkoa kama aga Khan wekeza nguvu kwenye ndoto zako mpaka zitimie.

Sijasema husiwe na mpenzi, sijasema husifanye MAPENZI,sijasema husioe, oa,,,nimesema mapenzi yasiwe central purpose ya Maisha Yako, pambania ndoto mapenzi yawe ni kama hitaji la kibailojia na la kiroho ila yasiwe central purpose katika maisha yako.

Kama usiku hupati usingizi basi iwe ni kwasabab ya ile kampuni unayopanga kuijenga na sio mapenzi, kama una stress ziwe za kupoteza 500M sio umeachwa, kama unamsongo wa mawazo ni iwe ni kwasabab ya maaana na sio mbususu, kujenga nyumbaza watoto ya yatima na sio kupigia magoti mtoto wa watu.

Yani Kuna kitu kikupe motisha yakuyafurahia haya maisha ukiachana na mapenzi, uwe na kitu Cha maana unachokifanya kwenye uso wa hii dunia ukiachana na mapenzi, kitu ambacho upo tayari kufa, kwenda jela, ulale na njaa, uwe maskini ili kikamilike, A MISSION TO ACCOMPLISH!!!!!!!

Kama unaye mpende, mjali na mthamini na kama huna mtafute, ukimpata mpende, mjali na mthamini ila hasiwe kipaumbele Cha maisha yako, hasiwe MISSION yako, there is a lot to accomplish, a lot to explore, let her be by your side while you're enjoying your journey.


#OneDayYouWillBeGone
Dr Criminal






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee umeandika point tupo, japo herufi "h" imetumika sana pasipostahili lakini umetendea haki contents za uzi wako.

Na nadhani wanaume tulimbwa tuwe hivyo yaani skanganga na sio legelege kwenye mapenzi.

Kujiua kisa mapenzi ni ulofa na upumbavu mkubwa sana.
 
Upo sahihi kabisa idadi yetu ya watu inatoa tafsri kabisa asilimia kubwa ya akili zetu zipo kweny mapenzi na ngono haiwezakani mwaka 2012 tuwe 40 million ila 2022 tuwe 60 ndani ya miaka kumi tu wameongezeka watu zaidi ya Milioni 18 na hii yote ni matoke ya kufanya ngono sex ni method ya reproduction ila sio starehe.
 
Upo sahihi kabisa idadi yetu ya watu inatoa tafsri kabisa asilimia kubwa ya akili zetu zipo kweny mapenzi na ngono haiwezakani mwaka 2012 tuwe 40 million ila 2022 tuwe 60 ndani ya miaka kumi tu wameongezeka watu zaidi ya Milioni 18 na hii yote ni matoke ya kufanya ngono sex ni method ya reproduction ila sio starehe.
Exactly mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom