Kuna Kitu kinaendelea kwenye Media za Tanzania

mzee wa liver

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
81,403
423,245
Kaka yangu,

Dotto Bulendu.

2015 Vyombo vya Habari hususani TV viliweka utaratibu mzuri wa namna ya kuandika na kutangaza Habari za Kisiasa hususani uchaguzi mkuu kuanzia hatua ya mchakato ndani ya vyama mpaka Siku ya kutangazwa Kwa mshindi.

TV zilivipa vyama vyote hadhi Na haki Sawa ,ilikuwa ukifungua taarifa ya Habari ya TV,Kama leo stori ya kwanza ni CCM itakayofuata itakuwa ya Chama shindani,na kesho stori ya kwanza itakuwa ya kwanza ya Chama shindani inayofuatia CCM.

Mfano Mmoja wapo walikuwa ITV, walipeleka waandishi upande wa UKAWA Na Upande wa CCM,Na kama leo Kwenye taarifa ya Habari CCM wakitengeneza Habari kuu,basi kesho itakuwa zamu ya Kambi ya vyama shindani.

Mwaka huu imekuwa tofauti kidogo,Jana nilitazama Kwa wakati mmoja taarifa za Habari za TBC,Azam(UTV),Star TV,na ITV ambapo hiyo jana vyama viwili vya upinzani vilikuwa vimeanza Vikao vyao vya juu vya kupitisha majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na upande wa Zanzibar.

Nilichoshuhudia kilikuwa tofauti kabisa Na zile Siku ambazo CCM ilikuwa inapitisha majina ya wagombea Uraisi,CCM Kwa Siku zote ilitawala maudhui ya Vyombo vya Habari ,Karibu Taarifa ya Habari zote ,stori ya kwanza ilihusu mchakato ndani ya CCM.

Ila kwa Jana, ni Azam (UTV) pekee Kwenye taarifa ya Habari ndiyo waliotoa uzito Kwenye matukio ya Vikao vya vyama vya Chadema Na ACT,Azam waliipa kipaumbele stori ya Chadema Kwa kuifanya Kuwa stori namba Moja Na waliipa Karibu dakika 6,ikafuatiwa na ile ya ACT,Stori ya Chadema Na ACT ilikwenda karibu dakika 12 Kwa uzito ule ule ambao waliupata CCM.

ITV Kwenye taarifa yao ya Habari ya saa mbili stori Hii haikuwa Habari kuu,iliruka baada ya dakika 20,Yaani saa mbili Na dakika 20,Na ilirushwa Kwa mfumo wa kifurushi ambacho hakikuzidi dakika 2 Na sekunde 45 ,Kwenye Uandishi Habari kuwekwa hapo maan yake haina uzito.

Star TV wao waliirusha baada ya dakika 18,Yaani saa mbili Na dakika 18,Na stori hiyo haikuwa Na sauti za wagombea wala taarifa za matokeo ya Kura za wawania ridhaa ndani ya Chama,stori hakikuzidi dakika Tatu Na ilikuwa ni kirufurushi.

Je, leo Chadema Na ACT wataweza kupenya Na kutengeneza Habari kuu Kwenye taarifa za Habari za saa mbili Usiku Na saa Moja Usiku Kwenye TV za Tanzania?ama watawekwa Kwenye kundi la Habari za kawaida?
 
Uliyoyaandika yalifanyika Kenya miaka ya 2000 uko kilichofuata Moi akapigwa chini, Yalifanyika Sudan Leo Bashir yuko wapi!?

Yalifanyika majuzi Ethiopia Leo Ethiopia imebadilika kabisa

Yalifanyika south Africa,Gambia, Malawi ila leo kote ni hisoria

Nchi inaenda kuandika historia mpya na kubwa Sana katika Taifa letu.
 
Mimi naliangalia hili kwa jicho la tatu...

When it comes to Habari / Media Tanzania imerudi nyuma kwan kiwango kikubwa sana..., na impact yake itaendelea miaka mingi sana..., Kazi nzuri zilizofanywa huko nyuma za kuifikisha habari hapa ilipofika imeharibiwa kwa kasi sana...

Yaani hizi sio habari tena bali ni propaganda.....
 
Mi nishasema mwandishi wa habaei akifa msiende kumzika akiwa na harusi msimchangie Hawa watu inabidi wawe dealt with individually.

Sjaelewa unamaanisha nini, nanibwasiende kumzika, chadema au wananchi,
Weww unadhani kila mwananchi ananufaika na vyombo vya habali
 
Uliyoyaandika yalifanyika Kenya miaka ya 2000 uko kilichofuata Moi akapigwa chini, Yalifanyika Sudan Leo Bashir yuko wapi!?

Yalifanyika majuzi Ethiopia Leo Ethiopia imebadilika kabisa

Yalifanyika south Africa,Gambia, Malawi ila leo kote ni hisoria

Nchi inaenda kuandika historia mpya na kubwa Sana katika Taifa letu.
Mkuu bado umelala? Naona bado unaota!
 
Dawa yao hawa wamiliki wa vyombo vya habari,kutonunua bidhaa zao,tuyang'oe madishi yao ,tutafute habari kwenye mitandao,
Eti ITV habari ya kwanza inakuwa 8 8
 
Na huyo Bwana MC aka Msema Chochote akiwaropokea hao watu wa media ndo hata taarifa ya habari asahau.
 
Back
Top Bottom