Kuna kila sababu ya katiba mpya kuja na muundo mpya wa muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna kila sababu ya katiba mpya kuja na muundo mpya wa muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by simaye, Apr 12, 2012.

 1. simaye

  simaye JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Muungano wa Tanganyika na Zanziba uliofanyika mwaka 1964 una mapungufu mengi hasa kwa upande wa Tanganyika hasa katika mfumo wa mamlaka ya juu kabisa ya uongozi maana wanzanzibari hakuna siku watakosa kiongozi wa kuwatetea maana wanaye RAIS wa Zanzibar nawa Muungano, Watanganyika ikitokea anachaguliwa RAIS wa Muungano Mzanzibari basi wanakosa mwakilishi katika mamlaka ya nchi yaani Rais je hii ni sawa au ndio kusema hawa watu walioko madarakani hawalioni hili.Kuna kila sababu katiba ijayo kutamka wazi kuwa anapochaguliwa rais wa muungano mzanzibari basi watanganyika nao wachague rais wa Tanganyika. Hii italeta usawa na maana hali ya Muungano wetu maana kwa sasa naona kama ni vurugu maana akitokea Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Mzanzibari na wanzabari wanachagua Rais wa Zanzibar ambao eti wote wanakuwa wawakilishi wa watanganyika pia.Wadau mnalionaje hili?
   
 2. U

  Userne JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkubwa hili nalo neno!
  Ila Tg pamoja na kujifanya wanaona hawana macho! Sababu Tg haina kauli kuhusu Muungano! Kamati yeyote iteuliwayo kuhusu Muungano wazenj wanakuwa ni wengi kwenye kamati husika! mzenj atawakilisha zenj, Pia lazima awakilishe muungano na usishangae kamati zima ikawa ya wazenj kwa mtindo huo!
   
 3. m

  mharakati JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tusiongee tu tukae katika forum tofauti katika muda huu na kudai haki ya utanganyika wetu, wazanzibari wako proactive ni sisi tu huku bara kila kitu sawa..kila kitu sawa mpaka lini? huu ni wakati wa kutaka kujua huu muungano unatunufaisha vipi kimaendeleo ya kiuchumi..dunia ya sasa siyo mambo ya kisiasa yalishapitwa na wakati, uchumi na fedha ndiyo zinaongoza siasa za kimataifa na maslahi ya nchi zote.sasa sisi hatuoni hili, muungano ni mzigo kwa Tanganyika na lazima hili liongelewe kitaifa.
   
 4. l

  lum JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 343
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  zanzibar wanasema ''JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA'' shengesha badaeee .Km watanganyika hawaitaki nchi yao sio wazanzibar
   
 5. k

  kula kulala Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini na sisis hatuanzi harakati za kudai tanganyika yetu kwa kuwambia hawa ccm kwani wakatu umeshafika
   
 6. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Njia pekee ya kuidai Tanganyika na kufanikiwa kuipata ni kwa kuikataa ccm. Lakini tukiendelea kuikumbatia ccm muundo wa muungano hautabadilika na malalamiko ya watanganyika kukosa serikali yao yatakuwepo daima. Ikumbukwe kwamba muundo wa serikali 2 uko katika sera za ccm!
   
 7. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unajua hatuna wa kumlaumu coz kama sasa tumeelewa kuwa kuna tatizo na hatuchukui hatua za haraka kulirekebisha, basi tumeridhika na hali halisi ya kunyang'anywa haki zetu kama watanganyika. Tunatakiwa tuwatoe viongozi wenye nidhamu ya uwoga ya muungano bubu, kila kiongozi utasikia anasema muungano ulioletwa na baba wa taifa tuudumishe. Huu ni upuuzi mtupu, hatuwezi kudumisha kitu kisichokua na faida kwetu. Labda kwa wakati huo kulikua na faida ila sasa hautekelezeki na hatuutaki. Ni kama sera za ujamaa zilivyokatalia na zikafa kifo cha asili. Sisi tuamke, hakuna wakumlaumu, labda tujilaumu wenyewe kwa kuchagua viongozi wenye nidhamu ya uwoga. Fursa hii imekuja ya marekebisho ya katiba, tujitokeze tutoe maoni yetu, tudai tanganyika yetu, la sivyo muungano wa nchi moja sio muungano, coz zenji ni nchi huru kabisaa, inayosemwa kuungana ni tanganyika, sijui na nchi gani, ikazaa Tanzania. Ndiyo mana hata kwenye kuchanganya udongo wa nchi Mwl Nyerere alikua peke yake. Kwa hiyo alitudanganya tu, hapakuwepo na muungano bali kulikuwepo una ubadilishaji wa Jina la nchi kwa mgongo wa muungano kivuli/bubu, ndiyo mana zanzibar ina bendera yake, rais wake, mamlaka yake n.k. Ila sisi watanganyika tuna nini? Tuamke, tudai haki zetu watanganyika.
   
Loading...