Kuna kila sababu Jumuiya za kimataifa kuingilia kati suala la haki za binadamu nchini, kama serikali

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,380
2,000
Kuna kila sababu Jumuiya za kimataifa kuingilia kati suala la haki za binadamu nchini, kama serikali yetu imeshindwa kuzilinda. Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja matukio yafuatayo yametokea:

1. Kupotea kwa mwanaharakati, mwanasiasa chipukizi, na mwanafunzi wa shahada ya uzamivu (PhD) Chuo kikuu cha Maastrich Uholanzi Ndg.Ben-Rabiu Saanane

2. Kuokotwa kwa miili ya watu 7 huko Bagamoyo katika eneo la mto Ruvu ikiwa ndani ya mifuko ya sandarusi, na baadhi ikiwa na majeraha.

3. Kuchomwa moto kwa mtu mmoja huko Moshi eneo la Uru, na kuteketea kabisa kiasi cha kushindwa kutambulika. Mtu huyo anadaiwa kuvaa nguo zinazofanana na sare za magereza. Bado haijajulikana kama ni mfungwa au lah.

4. Kupotea kwa watu wanne wa familia 4 tofauti ambao ndugu zao hawajui walipo. Jeshi la Polisi mkoani limepokea taarifa kutoka familia 4 tofauti zikidai kupotelewa na ndugu zao. Haijulikani kama watu hao ni miongoni mwa wale 7 wa mto Ruvu, au ni huyo mmoja aliyechomwa huko Moshi.

Katika matukio yote hayo serikali imekaa kimya kana kwamba hakuna lolote lililotokea. Ni ajabu akifa Waziri, Mbunge, RC, DC etc watu watalia na kuomboleza, lakini watu maskini wakipoteza ndugu zao, wakifa/kuuawa kwa kuwekwa kwenye sandarusi au kuchomwa moto hakuna anayejali.

Hata familia zinapoomba kupima vinasaba vya miili ya waliokufa/kuuawa zinapuuzwa. Wanaambiwa miili imeharibika sana haiwezi kupimwa vinasaba. Lakini maiti ya Faru inafukuliwa na kupimwa vinasaba, kwa sababu nchi hii faru ana thamani kuliko binadamu. Amelaaniwa yeye amsujudiaye mnyama.! [HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]

Malisa GJ
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom