Kuna kila dalili za CCM kuhujumu uchaguzi mkuu wa 2015. Ni nini kifanyike sasa?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna kila dalili za CCM kuhujumu uchaguzi mkuu wa 2015. Ni nini kifanyike sasa?!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Jun 10, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  ..Wakati vyama vya upinzani(haswa CDM)wakipambana kuleta mabadiliko ya kifikra kwa watanzania kujua haki zao za msingi dhidi ya watawala wao...wao chama tawala CCM wanaonekana kwa kasi hiyo hiyo kuzuia vuguvugu hili la mabadiliko kwa watanzania....Badala ya kujikita kwenye kutatua matatizo ya msingi kwa watanzania..tunaona CCM wakitumia nguvu nyingi kwa gharama yoyote kwenye hila...fitna ..hujuma...kejeli...matusi.. etc etc kwenye chaguzi ndogo...mikutano ya kulazimisha kimagumashi...na hata tetesi za kushiriki kuwaua/kuwapiga wapinzani (CDM)....

  Way forward (nini kifanyike):


  • Wapinzani(CDM) kutumia gharama yoyote kuzunguka nchi nzima kutoa elimu ya uraia kwa watanzania haswa wa vijijini ili waweze kujua haki yao ya msingi ya kujiletea mabadiliko kwa njia ya sanduku la kura ifikapo 2015....na haswa kuwafanya wajue kuwa haki haipatikani kwa kupewa chakula,nguo na fedha..Pia kuwafanya watanzania hawa wajue umuhimu wa kulinda kura zao hapo 2015 kwa gharama yoyote kwa manufaa ya mabadiliko ya maisha yao(kama walivyofanya arumeru) ..Pia kuwafanya watanzania hawa wajiandikishe kwa wiingi kwenye daftari la wapiga kura ili wapate fursa ya kupiga kura kwa ajili ya mabadiliko ya maisha yao....
  • Ni kwa kufanya hivi tu wapinzani wataweza kupambana na hata kuwashinda watawala kwenye sanduku la kura....Kinyume na hapo nadiriki kutabiri kuwa come 2015...kuna hatari kubwa sana kwa CCM kufanya hujuma/kupora uchaguzi/matokeo kwa gharama yoyote....Hii ni kutokana na trend ya matendo ya CCM tokea vuguvugu la mabadilko lianzishwe na CDM...Kitakachofuata baada ya CCM kupora matokeo sijui...lakini sote twajua yaliyotokea kenya.......Nasisitiza...CDM piteni vijijini kuanzia sasa...haswa mikoa ya uswahilini....Pwani..Morogoro..Tabora...Dodoma etc etc...kama mnavyofanya Mtwara na Lindi...
  RIP mzee Bob Makani....
   
 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ukweli wa mambo unajidhihirisha katika maisha ya watanzania.Udanaganyifu is no more.Siyo enzi za kudanganyana hizi.
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hawa magamba wepesi saana,wasikupe homa
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  watanzania wa leo wameamka
  wameshaelewa umaskini wao unatokana na ufisadi wa chama tawala
  wanaelewa wanaokitetea chama ni wale walio na maslahi na wezi wakubwa serikalini
  wanaelewa chama kinawalea mafisadi hata kuwapa nafasi nyeti kama Chenge,lowassa nk
  HAKUNA ATAKAEPOTEZA MUDA WAKE KUKIPA KURA 2015
  watu wanataka mabadiliko.
  muda sasa umefika kwa wengi kusema liwalo na liwe ni heri kufa kutetea haki kuliko kuishi kwa woga ukifa maskini
   
 5. B

  Bob G JF Bronze Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ukijua kutakua na hila umeshinda coz utachukua tahadhari. Mi nina IMANI kubwa na VIONGOZI wangu wa CDM wameliona hili watalipa umuhimu na watachukua tahadhari ya kutosha. Hata hivo ccm hawana chao tena everywhere wanataka MABADILIKO, hata wale waliokuwa wanawasaidiana nao hawako upande wao tena, Chunguza CCM imekuwa ya viongozi na wale wanao vizia vyeo bila kusoma nyakati, Vimada, wapambe, watoto wao na famili zao na wachache wanaoishi kwa hofu ya Mabadiliko. hata JK Nyerere alivotangaza kuachia ngazi watu walilia sana wakiamini ndo mwisho wa Tanzania kumbe sivo nchi bado ipo, nae ameiacha na Maisha yanaendelea. JUKUMU LA KULINDA USHINDI NI LETU SOTE WAZALENDO na TULIOCHOSHWA NA UFISADI WA ccm
   
 6. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  acha ushabiki mtandaoni kwel nimeamini vijana wa sasa ni .com.
  Hebu fanya kupambanua mambo,uoni kama unahukumu kabla siku ya kiama ijatimia ni navyo jua kila binadamu ajakamili kwanini uamini kwamba hao viongozi wako wa CDM hawawezi kueleta umaskini mkubwa Tz.

  Nashangaa Watanzania wamesahau kauli moja inayosema :->A GOOD LIAR SHOULD HAVE A GOOD MEMORY:-"
   
Loading...