Kuna kila dalili ya kujitokeza mipasuko mikubwa CCM itakayokiweka pabaya 2015

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Points
170

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 170
Moja ya strength za ccm kihistoria ni mshikamano wake. Lakini kuanza miaka mitano iliyopita, na hasa mwaka huu kumejitokeza dalili za wazi za kuvunjika mshikamano huo hususan kipindi cha mchakato wa kura za maoni na uteuzi wa wagombea.

Inaonekana kuwa lipo kundi la miamba ambayo inapotaka kuwania nafasi za uongozi itazipata tu hata kama wana tuhuma, hili ni kundi ninaloliita MABEBERU. Na wako ambao wanachukuliwa kuwa WANAKONDOO ambao ni rahisi kutolewa sadaka kwa "maslahi ya chama" (maslahi ya wa kundi la babeberu). Kilichokuwa kinatokea wakati akina Sita wanasulibiwa hata ikaundwa kamati ya mzee ruksa ni hiki hiki. Na kama sio woga kuwa kuwaengua akina Sita kungeathiri uchaguzi uliokuwa umekaribia, leo "Sita" angekuwa "mbili", kwa kupunguzwa nguvu za kisiasa, kama sio "zero" kabisa.

Anyway, nachotaka kusema hapa ni kwamba, mwaka 2015, kwa kuwa ni mwaka ambao wanaccm watalazimika kupata mgombea mpya wa urais, makundi haya yatasigana, kiasi kwamba hapatatosha humo ccm. Kama wanaJF mnanusa mambo yaliyo mbali basi mmeshaona dalili za zanaowania uraisi huo. Mtayaona maandalizi hayo kuanzia uteuzi wa Waziri mkuu, mawaziri, na nafasi nyeti za uongozi wa ccm katika ngazi ya taifa. Mzee Mkwere atalazimika kulipa fadhila, na kuweka watakaomlinda atakapokuwa amepunzika pale Bagamoyo, na hapo ndipo moto utapoanza kuwaka. Mipasuko itakayotokea hapo kwenye chama kijani sina hakika kama itaacha jiwe juu ya jiwe. YANGU MACHO.
 

Forum statistics

Threads 1,389,890
Members 528,046
Posts 34,037,698
Top