Walinzi wa shule za msingi hulipwa mshahara kutokana na michango ya wazazi,sasa kuna kila dariri zinazoashiria walinzi hao kuacha kazi mara shule zitakapofunguliwa Januaari/11/2016.Hii inatokana na tangazo la ELIMU BURE BILA MALIPO mwanzoni mwa mwezi Oktoba hivyo kusababisha wazazi kutochangia michango tena.Tangu tangazo hilo litolewe matokeo yake tangu mwezi Novemba walinzi hao hawajalipwa mishahara yao hadi leo hii.Hali hii inadhihirisha kuwa Serikali haikujianda na sera ya ELIMU BURE BILA MALIPO ingawa inadhamira njema kwa wananchi.Ombi langu kwa serikali iandae utaratibu shule zitakapofunguliwa walinzi walipwe mishahara yao yote.Tayari walinzi wameshaanza kuwasumbua walimu wakuu kuhusu mishahara yao na kutishia kuacha kazi hiyo ya ulinzi kwani wanashindwa kumudu maisha yao.