Kuna kila dalili wachambuzi Wasafi FM wamemchoka Maulid Kitenge

Kumekuwapo na sakata siku mbili hizi kati ya msemaji wa Simba, Haji Manara na mtangazaji wa Wasafi FM, Maulid Kitenge.

Hii ni baada ya Kitenge kupost kwenye page zake kwamba kuna ugomvi kati ya Morrison na kocha wake Gomes, na ndio maana Morrison aliachwa Dar safari ya Khartoum, madai ambayo Manara aliyakanusha na kumuonya Kitenge aache uzushi.

Leo katika kipindi cha michezo asubuhi, amehojiwa CEO wa Simba, akakanusha kuwapo ugomvi huo na akadai ni waandishi tu wanaotafuta followers kwenye pages zao ndio wanazusha hilo. Pia akahojiwa kocha Gomes kama ana ugomvi na kwa nini alimuacha Dar, akasema taarifa hizo si za kweli na Morrison ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa ambaye atawasaidia sana Simba, na akasema alimuacha Dar kwa sababu za matatizo ya kifamilia.

Pamoja na ufafanuzi huo wa CEO na kocha mwenyewe, lakini bado Kitenge akawa anamlazimisha Zingizi aongelee ugomvi ili kuhalalisha habari yake ya mitandaoni, na wakati wakizungumza hayo, wachambuzi wengine wa soka akina Musa, Ambangile nk waliamua kupiga kimya kuwaachia Kitenge na Zingizi wakifarijiana kuwa CEO na kocha wamekanusha tu ila kuna habari wao wanazo, hadi ikafikia hatua ya Ambangile kuvunja ukimya na kuanzisha habari nyingine mpya.

Kitendo cha wachambuzi wenye akili zao kuamua kukalia kimya ushawishi wa Kitenge ili wasiwaamini CEO na Gomes kimenifanya nipate picha kuwa huenda waliona watajiondolea heshima kujadili kitu ambacho kimeshakanushwa, tena mmoja wa wakanushaji nihuyo huyo Gomes anayehusishwa na ugomvi!

Hongera Musa Kawambwa, George Ambangile na wachambuzi wote mliokuwapo studio kwa kumuachia Kitenge alibebe zigo lake, wala asiwasumbue, mpeni makavu!
Unaona Simba wapo sahihi kwa hili au umeandika ili ujaze page tu
 
Fabrizio Romano huwa anasema, wachezaji wamegombana na kocha?
Mara kagere ampiga kichwa kocha Sven?
Hivi hizi ni tetesi au lengo kuu ni kuwatoa watu mchezoni? Hasa katika ardhi yetu ya Tanzania ambapo kila kitu ni mtandaoni.
Mkuu,
Kuhusu hilo la mchezaji kugombana na kocha ni mara ngapi umewahi kusikia tetesi juu ya jose mourinho kugombana na wachezaji wake??? Mfano ndani ya chelsea 2016 ilisemekana kulikuwa na mgohoro..juzi lampard kaondoka lkn inasemekana kulikuwa na mgogoro..tetesi zipo..hazikwepeki..watu wenye weledi wanajua jinsi gani ya ku deal na tetesi

Iwe simba iwe yanga tetesi hazikwepeki..cha muhimu ni jinsi ya ku deal nazo lkn si kutishia waandishi wa habari
 
hv unategemea kabisa Babra au Gomes wangekubali kua kuna ugonvi? halafu hili swala baadhi ya mashabiki wanalikuza tu, hizo Kitenge alizosema ni tetesi tu, na mbona hata Ulaya kusemwa semwa kutokuelewana kati ya coach na player ni jambo la kawaida sana? inakuaje hiii inakua ishuuuu wakati ni jambo la kawaida tu katika soka? Kite na Haj seems wana mambo yao binafsi wao kama wao, sema teams zinatumika tu kujifichia
Wewe unawaza kama mm.. sioni cha kuwatoa mate wale jamaa.

Tetesi za kitenge zisitupotezee muda.
 
Kitenge hajawahi kuipenda Simba...

Kitenge na Haji wanajuana hao, mambo yao waachieni wenyewe...
 
Siwezi kubishana na mtu anajiita Chizi,kama unaelimu yoyote ada imepotea bure tu,kama Kaze ni kocha kweli kwenye situation ya 1-1 na zimeongezwa dk 2 na unataka matokeo huwezi mwinua mchezaji sub aingie.......yaani 91+ unamwingiza mchezaji kwenda kufanya nini ? Kwahiyo kupiga mbele tu ndiyo unaona mpira? Mechi zote, Coastal na Police tumecheza kama underground sijui wa wapi.......yes tuna average players kwa baadhi ya position ila siyo kwa mpira ule wa piga mbele wala huoni goli linatengenezwa kupitia wapi........
Sasa huo ndo mpira wa Yanga miaka yote. Its our philosophy. Na wachezaji wenyewe ndo hao hao...kwa sasa wachezaji wa maana hawazidi 4 wachezaji ndo uwezo wao. Huku kocha wa ngapi tunafukuza.
 
Naifananisha yanga na binti aliyekuwa anaringa ujanan akitaka kiolewa na wenye pesa matokeo yake kaishia kuwa single mother na uzee ndio huo unapiga hodi anabak kuringia uzur wa ujanani kumbe umr ushamtupa

mfanano umekaa vyema sana huu
 
Nyie huyo kanjibay wenu anajua nn kuhusu soka litimu lenu linashakua la familia ya mo
Ulishawahi kuona Mo anasafiri kwenda kufuata mchezaji nje ya nchi? Ulishawahi kuona Mo amebebwa juu juu kwenye kiti eti amewezesha usajili? Ulishawahi kuona washabiki wa Simba wanashangilia usajili badala ya ushindi?
 
hv unategemea kabisa Babra au Gomes wangekubali kua kuna ugonvi? halafu hili swala baadhi ya mashabiki wanalikuza tu, hizo Kitenge alizosema ni tetesi tu, na mbona hata Ulaya kusemwa semwa kutokuelewana kati ya coach na player ni jambo la kawaida sana? inakuaje hiii inakua ishuuuu wakati ni jambo la kawaida tu katika soka? Kite na Haj seems wana mambo yao binafsi wao kama wao, sema teams zinatumika tu kujifichia
Wewe unawaza kama mm.. sioni cha kuwatoa mate wale jamaa.

Tetesi za kitenge zisitupotezee muda.
Kitenge kwenye taarifa yake hakusema Tetesi, yeye ameandika kama shahidi namba moja.

Hii ni mbaya sana, kwasababu hakuna sehemu amesema chanzo cha habari, lazima kuwe na mashaka kwenye taarifa yake.

Hivyo huenda nia yake ni kuleta taharuki Simba SC, kwahivyo lazima apewe Onyo Kali Sana!
 
Sio kweli mkuu bali ni hivi..kitenge amewameza wale madogo mle ndani yaan jambo analo tqka yeye ndilo lizungumziwe ukibishana nae itakupasa ukae kimya tu.

Na shida ya kitenge ni Unanzi wa kuipenda yanga. Binafssi nilimsikiliza shafii dauda leo ktk Hili game shafii alipasua JIPU leo na ule ndio ukweli. Shafii amesemaa wazi kabisaa wadhamini wale wa herufi tatu ndio shida maana wao ndio wana ratibu kila kitu ktk club ile na shafii alisema wazi ata maamuzi ya kumfukuza kocha M/kiti wa club na Makamu wake wote hawakuwepo.

Lwambano akaongezea akasema ndani ya club ya utopolo kuna wajanja wachache ambao wanaendesha maisha yao kupitia club ile wamejificha kwa mgongo wa mdhamini wa herufi tatu

Sasa kuamini hili binafsi huwa najiuliza iv ina kuwaje sponsor anaingia ktk vikao vya kuongoza club tena wao sio main sponsor mbona wale michezo pesa hawa play part kama mdhamini wa herufi 3
Anachofanya mo simba anatofauti gani na hao gsm tuacheni unafki watanzania,
 
Back
Top Bottom