Kuna Kila Dalili Uchaguzi Mkuu 2015 Hautakuwa Halali wala wa Haki

Mfikirishi

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,492
8,537
Tanzania si nchi ya kwanza kutumia mfumo wa BVR.

Kote ambako teknolojia hiyo imetumika na hasa barani Afrika tayari tumeshuhudia matatizo mengi sana. Uzoefu unaonesha kuwa matatizo mengi hutokea siku ya upigaji kura na makusudi kabisa kipindi cha kuhesabu kura ili kumpata mshindi.

Na mara nyingine tumeona matokeo yakiamuliwa mahakamani.

Hapa kwetu Tanzania changamoto zimeanzia hatua ya uandikishaji ambapo watu pamoja na kuwa na sifa bado wanaandikishwa kwa mafungu - yaani mpaka muda uliopangwa eneo fulani unaisha wapo walioandikishwa na wasioandikishwa.

Kwa maelezo ya wahusika kwenye uandikishaji ni kwamba pamoja na walioandikishwa kupewa kadi kuna uwezekano majina yao hayatakuwa kwenye mfumo hadi baadaye sana... Hapa napata mashaka makubwa... Hii ni Afrika; makosa ya makusudi yanaweza kuhalalisha uhalifu....(fursa ya uchakachuaji).

Itoshe tu kusema kuwa tusipokuwa makini BVR itatuvurugia nchi yetu. Wapo wengi watakao achwa bila kuandikishwa lakini vile vile wapo watakaofika kwenye vituo vya kupiga kura wakiwa na vitambulisho lakini hawatakuta majina yao.
HAKI ITAPORWA HAPA.

Lakini bado changamoto zitakazokuja wakati wa kuhesabu kura ambapo UHALALI WA MATOKEO UTATILIWA MASHAKA.

Kabla hayajatufika makubwa ni busara wanasheria wangekimbilia mahakamani kupinga matumizi ya BVR hadi hapo NEC itakapojipanga sawa sawa.

Maarifa na busara hii itusaidie la sivyo wengi wataangamia!!
 
Back
Top Bottom