Uchaguzi 2020 Kuna kila dalili huenda mwiko unaenda kuvunjika

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
2,463
2,640
Wasalam,

Pamoja na mazuri yote aliyofanya Mh magufuli bado wingu jeusi limetanda ndani ya ccm kutokana na uasi wa baadhi ya wanaccm.
Kuna kila dalili kwamba ccm inaenda kushindwa kwa fedhea ktk uchaguzi wa Oct 28.

Dalili moja mbaya ni kwamba wananchi ambao ni wapiga kura wamekata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha na wengi wameapa kuikataa ccm Oct 28, huenda Tanzania ikaandika historian kwa Rais kuongoza kipindi kimoja cha miaka5.

Dalili zinaonesha Watanzania hawana imani na CCM pamoja na rais magufuli.

Maendeleo yana vyama.
 
Kwa uelewa huu Tanzania tuna safari ndefu sana kuufuta ujinga. Hata mfano wa Maalim Seif umeusahau...tangu 2015 hadi leo hakuwahi kuwa raisi.
 
Dalili moja mbaya ni kwamba wananchi ambao ni wapiga kura wamekata tamaa kutokana na ugumu wa Maisha na wengi wameapa kuikataa ccm Oct 28,
Yaani hii njaa na dhiki ya hela ndiyo wapiga kampeni wakubwa wa Lisu. Lisu anashangiliwa na kupokelewa kwa nguvu zote kwasabb watu wako hoi kiuchumi.

Wanamuona Lisu kama mkombozi wao. Lisu atashinda kwa kimbunga, lkn watu wake hawamuambii ukweli.
 
Ninaongea kila wiki na ndugu zangu huko kijijini; hakuna wanaojua chama cha upinzani, wanasema tangu mwaka 2010 wakati CHADEMA ilikuwa imeanza kujikita hapo kijijini, leo hii hakuna chama zaidi ya CCM. Wanashindwa kutofautisha kati ya serikali na CCM; kwao huwezi kuwaambia jambo dhidi ya CCM, ndiyo maana nina uhakika kuwa CHADEMA kinacheza kujifurahisha tu, ila siyo kutafuta ushindi. Ushindi hauji kwa mtindo huu wa CHADEMA.
 
Hicho kijiji kitakuwa kiko polini sana labda ambako hata mawasiliano hakuna lakini vijijini vya siku hizi hivi ambavyo huwa tunawaomba watutumie hata picha za mashamba yetu ya miti kwa whatsapp tuone ukubwa wake wanafutilia kampeni kama kawaida na wanajadili kama tunavojadili mijini hivi hivi
 
Kwetu ni pazuri sana huenda kuliko kwenu; wako vizuri sana kibiashara, hawategemei pesa za mkato mkato ambazo ndizo zinazoliliwa na watu wengi hapa. Umewahi kuona watu wanaofanya biashara za kihalali wakililamika? Hii ya kupungua hela kwenye mzunguko ni jambo la muhimu sana kuimarisha uchumi. Mkapa aliimarisha sana mzunguko wakati wake lakini yaliyofuata ndiyo tunayokumbuka leo; kuna wakati inflation ilikuwa inapanda. Sasa hivi inflation imekuwa controlled tena kama alivyoacha Mkapa.

Sijui kama unajua kusoma graph!

1600555065381.png

Sijui kama bado unaikumbuka picha hii pamoja na vikatuni vilivyofuatia

1600555388113.png
 
Ninaongea kila wiki na ndugu zangu huko kijijini; hakuna wanaojua chama cha upinzani, wanasema tangu mwaka 2010 wakati CHADEMA ilikuwa imeanza kujikita hapo kijijini, leo hii hakuna chama zaidi ya CCM. Wanashindwa kutofautisha kati ya serikali na CCM; kwao huwezi kuwaambia jambo dhidi ya CCM, ndiyo maana nina uhakika kuwa CHADEMA kinacheza kujifurahisha tu, ila siyo kutafuta ushindi. Ushindi hauji kwa mtindo huu wa CHADEMA.
Kijiji gani??we ongelea kijijini kwenu tu mzee, huko kwenu inaelekea bado ni ulimwengu wa giza...mi nafanya projects vijijini mikoa tofati watu wameamka mnoo!!watu hawaitaki Ccm na Ccm mwaka huu inaanguka
 
Back
Top Bottom