Zanzibar 2020 Kuna kijungu kinapigwa Visiwani, ni Uchaguzi wa hatma ya Zanzibar

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Tunaendelea kuwapeni habari zetu za tathmini. Bado timu iko visiwani ikitupatia tathmini mbali mbali za kisiasa na kijamii.

Huko visiwani kuna kijungu chapagwa.

Picha halisi ilioyoko huko ni kuwa baada ya CCM kumteua Dkt Hussein Mwinyi, kwenye jamii kuna fundo la chini chini. Mara HII KAMPENI NI RAHISI MNO KWA WAPINZANI , Tayari huko kuna sauti zinavuma,

"Hatma ya Zanzibar" Hili neno lipigiwe mstari sana, Wenyewe wanasema ulioitwa ukoloni sasa unaelekea kutaka kurasimishwa na kuimaliza Zanzibar

Ujio wa Dkt Mwinyi si tu kwamba ulikataliwa ndani ya CCM kindaki ndaki kwa wenyeji wa Zanzibar, lakini unatafsiriwa ndio unataka kuhitimisha uwepo wa Zanzibar katika ramani.

Watafiti fuatilieni. Zanzibar kuna hofu iliyofichwa na wenyewe wanaambizana. " uchaguzi wa 2020" umebainisha mengi , Ni vita ya CCM asili Zanzibar na CCM kutoka bara. huo ukweli hausemwi.

Katikati ya hilo kuna upinzani wenye nguvu ambao wenyewe unajitosheleza. Mjadala unaendelea kuhusu hatma ya ZANZIBAR na ujio wa Dkt Hussein Mwinyi.

Siasa za Muungano na Maslahi ya Zanzibar yanatajwa sana na kuingizwa nasabu za watu na asili zao.

Hii misemo ipo na kuna tahadhari kubwa inachukuliwa na makundi mbali mnbali ya kisiasa na kijamii.

Kazi ipo kweli kweli. Tunasubiri upepo wa kampeni uanze tuweze kuwajuza zaidi.

Kishada
 
Jecha bado yupo hai na keshazalisha kina Jecha juniors kibao hata Maalim akishinda kwa 99% ni Mwinyi atatangazwa mshindi, kiukweli siasa ya Zenjibari inatia aibu sana!!

wapinga muungano wakae vikao ardhini majini kwenye mashua na jahazi na mawinguni hakuna shida!! hatma ya Zenjibari na Rais wake tayari vilishaamuliwa Idodomya!! Goli la mkono Zenjibari ni njia pekee kuzuia Upinzani.

Hizo zingine mbwembwe tu!
 
Ni Dhahiri shahiri kuwa haya ni maneno ya wapinzani wa CCM huko Zanzibar wakijificha chini na ndani ya kichaka cha UTAFITI NA UCHAMBUZI. Fumbo mfumbie mjinga yahe mwerevu atalibaini tu.

Tumeshabaini rongo rongo na choko choko zenu wapinzani, kwa vile hamna pa kutokea, sasa mnataka kujikita ndani ya ubaguzi wa kitoto, wa huyu Mzanzibari Asili na huyu siyo au huyu Mpemba na huyu Mzanzibari na MZANZIBARA! Tunazijua hizo zote na kama wasemavyo TCRA, Mjanja Haingizwi Chaka!
 
huyo ni mtanganyika huyoo, shauri zenu wazanzibari yaani mtaendelea kuchaguliwa raisi na watanganyika adi lini?
 
Husein Amekataliwa na Wazanzibar wote ! huyu jamaa ana mkosi mkubwa sana !
Sio kweli wajumbe wa nec ccm Zanzibar jumla yake 68. 33 kati ya hao wamempa kura Dk Hussein. 35 wamegawana Dk Khalid na Mh Nahodha Kwa hiyo Dk Hussein Mwinyi amepata nusu ya kura za wajumbe wa nec kutoka Zanzibar.

Watu wasiokuwa na nia safi wanaopenda mifarakano na kuendeleza siasa za chuki na ubaguzi Kwa maslahi wanayoyajua wao ndio wanaoeneza hizo propaganda. Lazima tuwapige vita watu wa aina hii Kwa mustakbali wa taifa letu.
 
Zanzibar ni kisiwa kwa minajili hiyo Zanzibar hakuna mzawa usidanganyike. Wale wanaojihita waunguja ni wanzanzibara wazaramo, Wamakonde, Wanyamwezi, wangoni nk.

Na wale Wapemba ni masalia ya kiarabu kutoka kwa surutani. Leo natoa hofa pale Zanzibar kama unaweza kukuta kabuli la babu yake babu, au baba babu yake kabuli lake pale Zanzibar hakuna.

Wote historia yao hama isome bara kwa baba na mama au isome bara mama na baba ajulikani kama alivyo maalim seif sharif Hamad mwambieni awaonyeshe kabuli la baba yake pale Zanzibar au ndugu zake baba yake makabuli yao thubutu.

Kila siku unasikia hapa bara mbowe kafiwa na kaka yake, magu kafiwa na dada yake, kikwete nk, lini umesikia maalim seif kafiwa na ndugu yake pale Zanzibar jibu hana ndugu Zanzibar.
 
Muelimishe huyo kilaza wa CHADEMA hajui lolote
Sio kweli wajumbe wa nec ccm Zanzibar jumla yake 68. 33 kati ya hao wamempa kura Dk Hussein. 35 wamegawana Dk Khalid na Mh Nahodha Kwa hiyo Dk Hussein Mwinyi amepata nusu ya kura za wajumbe wa nec kutoka Zanzibar. Watu wasiokuwa na nia safi wanaopenda mifarakano na kuendeleza siasa za chuki na ubaguzi Kwa maslahi wanayoyajua wao ndio wanaoeneza hizo propaganda. Lazima tuwapige vita watu wa aina hii Kwa mustakbali wa taifa letu.
 
Je, kuna hasara gani kuwa na nchi moja na kuwa na viwango sawa. Watanzania wawezekuishi popole bila hila
 
Back
Top Bottom