Kuna kidada cheupe pale TANESCO Mbezi Beach Afrikana nani anakipa jeuri namna ile?

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,457
2,000
Kama mwezi hivi umepita!

Baada ya kusikia bei ya umeme imeshuka, Nilimtuma mdogo wangu kuomba umeme pale afrikana Tanesco!

Kwasababu nyumba ile anaishi mdogo wangu, hivyo nikamwambia aingize umeme kwa jina lake!

Dogo alipofika pale ili kuchukua fomu, Alikikuta kidada cheupe hivi kina nywele nyingi kichwani, kikamwambia dogo atoe hela ili kimpige picha ya passport! Dogo kwasababu kilimwambia picha alokuwa nayo haifai! (Hakijasema haifai kivipi)

Dogo akakubali kupigwa hiyo picha, Hicho kidada kikampiga picha dogo kwa simu pale dirishani na kuisafisha mle mle ndani ya ofisi ya umma!

Dogo alipoomba kupewa ile fomu, kile kidada kikamwambia atoe hela ya picha kwanza!

Dogo akatoa pesa pale dirishani lakini hakupewa listi yoyote ya ile pesa,
Baadae akanipigia simu kunielezea ilivyokuwa nikashangaa! Inakuwaje mfanyakazi wa umma anakuwa na ujasiri wa kiwango kile!

Nikamwambia dogo aulizie namba ya meneja pale ili nipate kumuuliza vyema,

Nikabahatika kumpigia simu yule meneja, lakini ajabu akasema wazi malalamiko ya hicho kidada hata yeye yanamkera kashakionya Mara kadhaa lakini yanajirudia!

Nikauliza mbona nimetozwa pesa ya picha katika ofisi ya Tanesco hapo afrikana pasipo kupewa lisiti? Yule meneja akasema atalifanyia kazi,

lakini ajabu hadi Leo sikupewa taarifa yoyote na malalamiko nilimfikishia!

Sasa nikajiuliza, kama mambo kama hayo kile kidada kimenifanyia Mimi hivyo.
Je ujasiri huo wa kupiga picha kwenye ofisi ya umma kimewafanyia watu wangapi?
Ina maana kinafanya biashara ndani ya ofisi ya umma?
ujasiri ule nani anakipatia?

Pia kama meneja alinijibu kuwa taarifa na malalamiko ya huyo mfanayakazi ni mengi na kashamuonya Mara kadhaa lakini haachi, je hicho kidada kinapewa jeuri hiyo na nani?

TANESCO YETU embu fuatilieni mtuambie hicho kidada cheupe chenye nywele nyingi pale mapokezi Tanesco mbezi beach afrikana kimewekwa pale na nani hadi kiwe jeuri namna hiyo?

Kinafanyia hivyo watu wangapi?
Huyo uliyeongea naye ndiye anayempa ujasiri, au jeuri, vyovyote utakavotaka kuita. kakutoa pembeni tu kuwa atafuatilia, wote wananufaishana kwa vitendo vya huyo dada.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom