Kuna "kakikundi" ambako Rais Magufuli alikuwa nako pale TANROADS na anakatukuza sana, kulikoni?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Haka ni kakikundi ka watu ambako Rais Magufuli alikuwa nako pale Tanroads na amekuwa akikatukuza sana. Imefika hatua hata wakitumbuliwa huku wanapelekwa kule. Aidha wengine nimeona wakipewa hata utukufu usio wa kawaida.

1. Mhandisi John Kijazi.
Huyu alikuwa pale ujenzi kama boss na Rais Magufuli alipoukwaa urais tu akamtoa kwenye ubalozi muda mfupi baada tu ya kudumu hapo sasa yupo naye ikulu kama katibu mkuu kiongozi. Hawa walikuwa maswahiba wakubwa pale ujenzi

2. John Mfugale.
Huyu ni mtendaji mkuu wa Tanroads ambaye jina lake limepewa hadhi na Rais Magufuli kuwa jina la daraja la juu la TAZARA. Hii ni ya kwanza kufanywa na mkuu wa nchi yetu na ni ya aina yake. Bila shaka akitoka pale Tanroads anaweza kuukwaa ubalozi.

3. Alphayo Kidata.
Huyu naye aliwahi kupita pale Tanroads. Rais Magufuli akamteua kuwa kamishina mkuu wa TRA, akamrudisha kwenye ubalozi akamvua hadhi ya ubalozi na wengi tulitarajia kitakachofuata ni mashitaka dhidi yake ila sasa ni RAS.

4. Charles Kicheere.
Huyu naye alikuwa na Rais Magufuli pale Tanroads akateuliwa kuwa kamishina wa TRA, akatumbuliwa na sasa ameteuliwa kuwa CAG baada ya kutokea huko kwenye u RAS.

Aidha nimeona leo wahandisi wawili wakiukwaa ubalozi na u RAS na hawa pia wamezungua zunguka kwenye vyeo na walikuwa pale Tanroads na Rais Magufuli.

Naona kuna kitu wanazunguka naye nacho na hawa hawatumbuliki bali wanahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Kulikoni? Hii kweli ni sahihi?
 
Acha uongo na kuongea usiyoyajua.

Alfayo kidata alikua katibu mkuu ardhi enzi ya JK mpaka JPM anaingia madarakani.

Kijazi alikua katibu mkuu ujenzi kabla yakupewa ubalozi. Kijazi alipewa ubalozi na JK sio Magu.

Inatia kinyaa sana kuongea usiyoyajua.
 
CAG amestaafu kwa mujibu wa sheria

Kama wapinzani wanampenda wamwajiri maana kila mwaka wanapata upotevu wa pesa
Kuna billion 250 zilihishwa kutoka mfuko wa barabara Tanroad hazijulikani zilikokwwnda na hazijatolea maelezo, Luna vivuko hakuna mawlezo, kuna nyumba za serikali zilizouzwa hakuna maelezo maana mhusika ndio huyooo kashikilia kila kitu sasa.. Hakuna duty of responsibility kwa aliyofanya na ukikaribia anga zake unatumbuliwa kabla ya Muda..
 
Amepiga sana tanroad na hao ndio walio na siri zake zote..

Ila kijazi hakupelekwa ubalozi na maguguli.. ila magufuli alipo.pigwa chini uwaziri wa ujenzi na JK Kijazi naye alipigwa chini ukatibu wa wizara ya ujenzi .
 
Acha uongo na kuongea usiyoyajua.

Alfayo kidata alikua katibu mkuu ardhi enzi ya JK mpaka JPM anaingia madarakani.

Kijazi alikua katibu mkuu ujenzi kabla yakupewa ubalozi. Kijazi alipewa ubalozi na JK sio Magu.

Inatia kinyaa sana kuongea usiyoyajua.
Good!
 
Hao ni wabwekaji wanaotumika na Mabeberu

Tutawanyoonsha kuanzia mtandaoni hadi mtaani
Acha uongo na kuongea usiyoyajua.

Alfayo kidata alikua katibu mkuu ardhi enzi ya JK mpaka JPM anaingia madarakani.

Kijazi alikua katibu mkuu ujenzi kabla yakupewa ubalozi. Kijazi alipewa ubalozi na JK sio Magu.

Inatia kinyaa sana kuongea usiyoyajua.
 
Dadavueni
IMG-20191103-WA0022.jpeg
 



Anayefahamu kazi zote na nani anafaa ni Zito Kabwe peke yake. Je, atatolea ufafanuzi maswali ya hapo juu?​
 
Back
Top Bottom