Kuna jinsi ya kumfanya mwanaume huyu amhudumie mtoto wake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna jinsi ya kumfanya mwanaume huyu amhudumie mtoto wake?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mom, Jun 28, 2010.

 1. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni walipendana sana na kupeana ahadi za ndoa, ikaja tokea dada akapata ujauzito ambao mwanaume alishauri atoe na dada alikataa, akamwacha na kumwambia si mimba yake maana yeye alishakuwa diagnosed kuwa hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba.

  Mwanaume hakuwahi kuokea mpaka mtoto alipozaliwa na kufikisha miezi5 na kama Mungu alitaka kumuumbua mtoto amefanana nae kama copy and paste!

  Alipomwona mtoto akaoma msamaha, lakini kwa kuwa dada alishatendwa alimuambia labda wafunge ndoa otherwise hahitaji uhusiano nae tena. Ikaja kutokea dada akapoteza kazi aliyokua nayo na mtoto anahitaji matunzo ikiwemo pesa ya kuhudhuria clinic ya ngozi kila mwezi kutokana na kuwa allergic,

  Shida baba hataki kutoa matunzo ya mtoto na mama akilalamika sana na kutishia kumwachia mtoto ndio anapewa pesa kidogo ambayo haitoshi kutokana na mahitaji ya mtoto kuwa makubwa.

  Je kuna sheria yoyote inaweza kumfanya mwanaume huyu atoe matunzo ya mtoto na mtoto aendelee kuishi na mama yake? Mtoto ana umri wa miaka miwili sasa.
   
 2. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  [FONT=arial,helvetica][FONT=arial,helvetica]Do not put such unlimited power into the hands of the husbands. Remember all men would be tyrants if they could
  d
  Hii signature yako kiboko, nimeipenda lakini inaonekana Mom wewe unawachukia sana wanaume. yaani umefika mahali unaamini wanaume wote wangependa kuwa tyrants? On the other side wat about women.(sorry off topic)
  [/FONT]
  [/FONT]
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  akimfungulia mashitaka bila ya shaka mahakama itamlazimisha alipe ............ila viwango atakavyolazimishwa alipe na mahakama ni vidogo sana. mahita aliambiwa alipe laki tu kwa mwezi, sasa huyo wako aweza pata labda laki na nusu tu na ndo uhasama na baba mtoto ukawa ndo wa moja kwa moja.

  bora awashirikishe wazee kutatua suala hilo
   
 4. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwenye birth certificate aliandikisha jina la nani? (Father)... kama alikubali kama mtoto wake na akakubali mtoto wake aandikwe kwa jina lakini i think she should have rights to ask for a child support... sijui sheria za TZ vipi lakini huku the court can order up to 20% of the fathers' net income as a child support...

  Having said that, premarital sex is totally condemned in our society, kama msichana got pregnant out of wedlock she and the father of the child will either have to face 2 yrs jail sentence or they should get married and they are free to get divorced later but the father will be forced to provide a child support...labda ahame nchi...
   
 5. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  si wachukii kihivyo! changia topic basi
   
 6. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  aliandika jina halisi la baba kwa sababu kwa uelewa wake hakuona sababu ya kuandika jina tofauti na baba yake mzazi.
  naona wenzetu wameendelea kumbe kuna sheria inawalazimu kwenda jela au kufunga ndoa?
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Sheria zipo. Anachotakiwa ni kutoa uthibitisho (mahakamani) kuonesha kuwa huyo mtoto ni wa huyo mwanaume (akikataa kuna DNA!). Ikishathibitika kuwa ni mtoto wake, suala la baba kutoa matunzo halina mjadala merefu kwani sheria ipo wazi (labda kama huyo mwanaume hana uwezo kabisa).

  Lakini huyo dada ni lazima ajue kuwa haki inakwenda na wajibu vilevile. Kama baba atatoa malezi kwa mwanae, then atakuwa na haki fulani juu ya huyo mtoto (kumwona, au pengine hata kumchukua akifikisha miaka 7).
   
 8. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  gaijin huyu dada anabahati mbaya sana maana hata mama mzazi wa mwanaume likua anaamini mwanae hana uwezo wa kumpa mtu mimba kutokana na walivyoambiwa na doctor. sasa hata ile kuja kumwona mtoto alileta mashoga zake ili waje wamsute dada na bahati mbaya ndio wakakuta mtoto wao kwa sura! yani wakaondoka kwa aibu na hawajawahi kutaka kujua tena. kwa hsida za huyu dada hata wakimlazimu kulipa laki ni kidogo ila inatosha.
   
 9. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kumchukua? hapo kweli haitakiwi maana dada hatakubali kumwacha mtoto akalelewe na baba especial baada ya kumkataa mimba. apart from DNA atatakiwa kutoa ushahidi kivipi? mtoto kafanana na baba ndio ushahidi wake au atatakiwa kueleza nn kingine?
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hii sheria ya premarital sex kuwa na kifungo cha miaka miwili iko wapi?
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280

  Nakumbuka kuna mahali niliwahi kuishi miaka ya tisini mwishoni. Sasa kulikuwa na mtoto anafanana na mimi sana na watu wengi walikuwa hawasiti kunambia hivyo. Ilikuwa bahati tu yule mtoto alikuwa mkubwa (i.e. alizaliwa maiaka kama mnne kabla mimi sijafika maeneo yale), otherwise ningesingiziwa kutembea/kuzaa na mke wa mtu!

  So kufanana tu sio ushahidi wa kutosha ingawa unaweza kumshawishi hakimu! Kama ulifuatilia ile kesi ya Mahita unaweza kuelewa nazungumzia nini. Ushahidi utakuwa muhimu endapo baba anakataa kuwa mtoto sio wake lakini katika case hiyo unaindicate baba alikataa mwanzao lakini baadae alikubali. Ni muhimu suala hilo la malezi likawa wazi na formal zaidi ili kutoa uhakika kwa mustakabali wa mtoto (hasa hilo suala la matibabu!).
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Wote wana makosa, lakini hawakumbuki anayeathirika ni mtoto. Kama kuna mwenye busara kwa pande zote mbili awakalishe chini wakubaliane tofauti zao ila wafanye yale yaliyo na manufaa kwa huyo mtoto.
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mom kama mama ngoja nikae kitako nifikirie nini cha kufanya
   
 14. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni SMU kuna kule kufanana japo si ndugu. shida ya dada ni garama za kumpeleka mtoto kupata matibabu, wakati mwingine anashauriwa kumbadilishia diet ili kuweza kujua nini kinamuaffect inakua ngumu sana kwa mtu asie na ajira ya uhakika kama isingekua hizi cost za hosp dada angeweza kujitahidi ahangaike na mtoto mwenyewe mpaka apate ajira.
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mwambie aende Ustawi wa Jamii... wanashughulikia hii maneno
   
 16. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sio premarital sex nawewe hujasoma vizuri nimesema mimba... halafu ukisoma location yangu utapata clue ya swali lako
   
Loading...