Kuna hujuma shule za sekondari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna hujuma shule za sekondari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Mar 4, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kumekuwa na taarifa mbalimbali za kuungua kwa Shule za Sekondari kama ilivyokwisharipotiwa siku za nyuma juu kuungua Shule ya Sekondari Machame na Shule ya Sekondari Shauritanga zote za Kilimanjaro.Leo imeripotiwa na TBC Taifa juu ya kuunguzwa kwa Bweni katika Shule ya Sekondari Singe iliyopo Singida.Bweni hilo limeungua wiki moja baada ya bweni lingine kuungua moto.Inadaiwa limeunguzwa kwa petroli wakati wanafunzi wako darasani.Shule nyingine iliyopo Arusha,katika Wilaya ya Monduli,Shule ya Sekondari Moita iliunguliwa bweni Mwaka jana na Mwaka huu tena bweni lingine limeungua.Kinachoshangaza ni kuwa bweni hilo halikuwa na umeme kwa hiyo huwezi kuhisi hitilafu ya umeme.Tetesi zilizopo ni kwamba inaweza kuwa hujuma za Mkuu wa Shule aliyeondolewa wakati hakutaka kuondoka kutokana na manufaa aliyokuwa anayapata na kusahau majukumu hivyo wazazi kumkataa.

  Sijui serikali kupitia Wizara ya Elimu imechukua hatua gani kuhusu hujuma hizi kwani zinarudisha nyuma juhudi za serikali za kuandaa nafasi zaidi kwa wanaomaliza shule za msingi.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasaidia wahanga wa mioto hiyo hivyo kuwafanya wasome kwa shida au wengine kushindwa kabisa kutokana na kuunguliwa vifaa vyao.Hata matengenezo ya sehemu zilizoungua huchukua muda au kutokuwepo kabisa na juhudi za kurejesha hali zao za awali.

  Haya nimeyapata kutokana na utafiti wangu mdogo,wenye maelezo zaidi wayatoe ili zisaidie mamlaka husika katika kuchukua hatua.
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Saa ingine watoto eti wakipata chakula kibovu wako tayari kuchoma shule moto!

  Naona ni ukosefu wa uzalendo na maadili zaidi ya hujuma!
   
Loading...