Kuna hujuma kubwa kwenye ujenzi wa Uwanja wa Ndege Iringa

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
572
356
Kwanza niipongeze kwa kuupanua uwanja wa ndege wa Nduli Iringa kuwa wa kiwango cha kimataifa. Kwakweli mwanzaoni hata mimi sikuona haja lakini huu mradi ni muhimu sana kwa utalii nyanda za juu kusini. Mkandalasi anajitahidi kuujenga uwanja huu kwa kasi kubwa ambapo kazi inafanyika usiku na mchana.

Nimeona kuna wimbi kubwa la wizi wa mafuta ya diesel unaofanywa na wafanyakazi wa mradi huo wakishirikiana na boda boda wa mitaani ambapo utaona makundi ya vijana wamepakia mdumu ya mafuta kwenye pikipiki na baiskeli na kisha kuwauzia wenye mabasi wanaopita barabara ya Iringa Dodoma. Kweli wizi ni mkubwa na wa kutisha kiasi kwanza unaweza kuathiri ujenzi wauwanja huu kwa kiwango kilichokusudiwa.

Ushauri kwa mkandalasi ni kuwa asafishe kwanza eneo lote la uwanja ili kuwe kweupe kwani kwa sasa kumejaa miti mingi pori na vitindi na abomoe baadhi ya mapagare yaliyobaki humo baada ya watu kuhama kwani ndimo wanamojificha wezi wezi wanaosafirisha mafuta hayo. Eneo lililo wazi ni lile analojenga run way tu. Kosa lingine kubwa lilikuwa ni kuwakodisha watu mashamba kulima katika eneo la uwanja wa ndege. Hata sijui ni mjinga gani aliwaza hivyo.

Kasoro nyingine kubwa ni kwa Tanroads kutowalipa kikamilifu waathirika wa kuhama ili kupisha upanuzi wa uwanja huo. Wananchi wengi waliohamishwa kutoka eneo la upanuzi hawajalipwa kikamili na wengine wamegoma kuhama bado wamo ndani ya eneo la uwanja wa ndege huku uwanja ukijengwa. Tunamwomba mkuu wa mkoa na wizara husika kushughulikia malipo ya fidia haraka ili watu wahame kabisa na wakafanye maendeleo sehemu nyingine kwakuwa bajeti ya serikali imeshapita.

Vinginevyo huu uwanja ukijengwa kwa kiwango kilichokusudiwa utakuja kuwa uwanja bora sana hata kuliko wa Chato. Ila ninaoma wasisahau kuuwekea fence kwaajili ya usalama ukitilia maanani kuna watu na mifugo ambao hukatisha uwanja humo isije siku ya siku dream line inashuka halafu inakutana na kundi la ng'ombe au mbuzi au watu.
 
Wamemruka kwenye mgao.Wachina wenyewe ndio wapangaji wa wizi huo hapo
 
Back
Top Bottom