Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,806
- 18,784
Mimi ni muumini mkubwa wa demokrasia na utawala wa sheria, na ndiyo ni moja ya sababu iliyonifanya kuvutiwa na uongozi wa Samia kuliko uliopita
Lakini kuna kipindi demokrasia hutumiwa vibaya na kuigawa nchi kwa udini au ukabila, hapo ndipo nasema demokrasia inabidi iwekwe pembeni
Kumekuwa na dalili za ukabila zinaanza kuchipua nchini, kuna kundi flani linaanza kujinasibu kuwa wao ndio wengi nchini na ndio wanaamua rais awe nani, sijui hili lina ukweli kiasi gani, ila haya ni matumizi mabaya ya demokrasia
Kundi hili linalotaka kutumia vibaya demokrasia ndio hawa hawa waliokuwa wakipiga kelele kuwa demokrasia haina umuhimu Afrika mtu wao alipokuwa akikanyaga katiba na kuua demokrasia, sasa ghafla demokrasia imekua ya muhimu mtu wao anapokuwa hayupo
Mwalimu Nyerere alipochukua nchi kutoka kwa Wakoloni, aliona hatari ya nchi kutumbukia kwenye siasa za kikabila na ikabidi aongoze kama alivyoongoza na tukaipata Tanzania hii
Nchi kama Misri ilikuwa hatarini kumezwa na siasa kali za kidini, kutokana na makundi yaliyokuwa yakitumia vibaya demokrasia, ila kutokana na kuendeshwa kibabe nchi imetulia na ni moja kati ya nchi zilizoendelea sana Africa,
Demokrasia ikitumiwa vibaya ni vurugu