Kuna harufu ya kujuana kwenye balozi zetu

Labda Mkuu William anaogopa kukujibu hili usijemletea Hansard nyingine hapa. LOL. Kuna list moja ya Wafanyakazi wa BOT niliiona kule Fesibuku, ilikuwa inatisha.
Atakuwa anatafuta jina langu la ukweli ili aje anitishe kuwa ananijua nina Rasta na mzuzu......Anyway mkuu pale BOT watoto wa vigogo bado wanapeta .....Ndulu alitupiga changa la macho
Watoto vigogo BoT wasafishwa

Na Ramadhan Semtawa

WAKATI watumishi wengine tisa wa Benki Kuu (BoT), wakifunguliwa kesi mahakamani kwa kughushi vyeti, watumishi wengine 18, maarufu kama watoto wa vigogo waliodaiwa kuajiriwa kinyemela wamebainika kuwa na sifa stahili.

Kukamilika kwa uchunguzi huo na matokeo, kunaondoa na kumaliza utata uliokuwepo tangu awali kuhusu ajira za watoto ambao baba zao wengine wapo serikalini na waliostaafu.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alithibitishia gazeti hili jijini Dar es Salaam kuhusu watoto hao kubainika na sifa stahili.

Watoto ambao wameonekana kuwa na sifa, majina ya koo zao ni pamoja na Lowassa, Sumaye, Kawawa, Lumbanga, Hassan Mwinyi, Muganda, Mahita, Nchimbi na Mkapa.

Katika orodha hiyo, majina mengine ya ukoo yanayotajwa ni pamoja na Luhanjo, Kamba, Mongela na Kigoda.

Akizungumzia mchakato huo ambao alisema uliendeshwa kwa uwazi na umakini, Profesa Ndulu alisema katika uchunguzi huo watoto wanane kati ya 18 ambao walikuwa wanafanya kazi za kitaaluma wote walikuwa na sifa.

Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, jambo la msingi lililotumika katika uchunguzi huo ni vigezo vya ajira kwa kuanzia mwaka 2000/01 hadi 2006/07.

Akifafanua hilo, Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kulikuwa na vigezo tofauti na baada ya mwaka huo, walioajiriwa baadaye 2006/07, walipaswa kuwa na vigezo vipya tofauti na vile vya mwaka 2000 hadi 2005.

Profesa Ndulu alisema kabla ya mwaka 2005, kazi za kitaaluma kigezo kikuu kilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini baada ya mwaka huo kigezo kikawa ni shahada ya uzamili (MA).

"Kwa hiyo, watoto hao wanane mnaoita wa vigogo wote walikuwa na basic entries (sifa za kujiunga), waliajiriwa kwa vigezo stahili, ambavyo kipindi hicho ilikuwa ni shahada ya kwanza, lakini pia waliendelea kusoma na kuweza kufikia shahada ya uzamili ambayo ni kigezo cha baada ya mwaka 2005," alifafanua Profesa Ndulu.

Alisema vijana hao ambao wanafanya kazi nzuri, waliingia na sifa stahili na bado wamekuwa wakijiendeleza kwa kusoma zaidi.

"Tena ni vijana wachapakazi tu, wamesoma vizuri, wanafanya kazi vizuri na tayari tumewapa barua za kuwataarifu kwamba wana sifa stahili," alisisitiza Profesa Ndulu.

Profesa Ndulu alisema watoto wengine kumi ambao hawakuwa wakifanya kazi za kitaaluma, nao waliingia wakiwa na sifa.

Kwa mujibu wa Profesa Ndulu, watoto hao walikuwa na kazi ambazo ni pamoja kuhesabu fedha.

Akizungumzia sifa zao za kujiunga, alisema kwa kazi ambazo si za kitaaluma, kigezo kikubwa kilikuwa ni kidato cha nne na kujua hesabu na Kiingereza.

"Hawa nao 10, wote walikuwa na sifa hizo, wanafanya kazi zao kwa mujibu wa taratibu na hakuna namna yoyote ya kughushi ambayo walifanya," alifafanua Profesa Ndulu, gavana ambaye amekuwa akiisafisha BoT.

Alisema uchunguzi huo uliangalia watumishi 50 wakiwemo hao 18 watoto wa vigogo na kuongeza kwamba, wengine pia walibainika na sifa huku wale ambao walikiuka walichukuliwa hatua.

Hata hivyo, alisema tayari BoT imetoa tangazo kwa kuwataka watumishi hao kujisomea kwa gharama zao wenyewe vinginevyo hawatapanda madaraja.

"Kwa hiyo, kama mtu hatajiendeleza, ajue hatapanda daraja, atabaki hapo hapo na kuathiri ajira yake," alisisiza Gavana Ndulu.

BoT ambayo ni taasisi nyeti katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 chini ya uongozi wa hayati gavana Daud Ballali, ilikumbwa na tuhuma mbalimbali.

Miongoni mwa tuhuma hizo, ni pamoja na hizo za watoto wa vigogo kuajiriwa katika mazingira yaliyohisiwa kuwa ni tata, kashfa ya ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na gharama kubwa za ujenzi wa majengo pacha ya benki hiyo.

.
Dogo wa Kigoda sijui ali re-seat lini form foo?
 
I am glad mmeleta ushahidi ambao unaonyesha udaku wenu, kichwa cha mada na maneno yenu havifanani, MZEE MWAKIKAGILE mimi unaweza kunitukana as much as you want huu ni mfupa umemshinda fisi ila unapotukana msichana mdogo wa damu yako kwa majina ya bandia ina raise a question on uwezo wako wa kufikiri na hasa umri ulionao. On undugu vyama vyote vimeoza hakuna wa kumsaidia mwingine! - Le Baharia
 
Hawa watoto wa vigogo wanaobebwa jaribu siku moja kaa nao, utaona jinsi walivyo na LOW THINKING CAPACITY ON HOW THEY ANALYSE ISSUES, just like most of their fathers.
Hivyo bila kubebwa unategemea nini? because they cant even think of being a Machinga, the first thing to think in moments of trouble is to COMMIT SUICIDE!
 
I am glad mmeleta ushahidi ambao unaonyesha udaku wenu, kichwa cha mada na maneno yenu havifanani, MZEE MWAKIKAGILE mimi unaweza kunitukana as much as you want huu ni mfupa umemshinda fisi ila unapotukana msichana mdogo wa damu yako kwa majina ya bandia ina raise a question on uwezo wako wa kufikiri na hasa umri ulionao. On undugu vyama vyote vimeoza hakuna wa kumsaidia mwingine! - Le Baharia

Kama "kichwa cha mada na maneno yenu havifanani" kwa nini hukuraise hii issue tokea mwanzo? Mbona ulianza kuchangia moja kwa moja na kuanza kurusha ngumi? Naamini umekamatwa na unatafuta pa kutokea. Mkuu imekushinda tuanchie sisi tuendelee kuchambua ulioita "udaku". Otherwise, wewe utaishia kuwa "mdaku". Halafu "MZEE MWAKIKAGILE" ndio nani hapa JF? Kuna Member mwenye ID ya "MZEE MWAKIKAGILE" hapa JF?
 
People Mmechemka Mkapa or Malecela hawana watoto ubalozi wowote Duniani, Mmechemka na muwache majungu! - Le Mutuz!

Field Marshall we kaa huko huko New York usifikili kuwakilimu wakina Nape wakija huko ndio leseni ya kupata ubunge wa Mtera; wagogo wamejanjaruka hakuna mtu wa jina kama lako atakuja kupata ubunge tena huko mkoa wa IDODOMYA, wazee wenu wameharibu miaka nenda rudi wagogo bado ombaomba tu!!
 
This is too low of you!!

Jibuni hoja, msianze kuleta habari za uchama hapa; kwani katika hilo the whole political system hapa TZ is corrupted with nepotism si CHADEMA, CCM, CUF, TLP, wala NCCR-Mageuzi.
Endeleeni na mabishano yenu bila kuchafua vyama pasi sababu, Nepotism katika NCCR umeiona lini?
 
Kama "kichwa cha mada na maneno yenu havifanani" kwa nini hukuraise hii issue tokea mwanzo? Mbona ulianza kuchangia moja kwa moja na kuanza kurusha ngumi? Naamini umekamatwa na unatafuta pa kutokea. Mkuu imekushinda tuanchie sisi tuendelee kuchambua ulioita "udaku". Otherwise, wewe utaishia kuwa "mdaku". Halafu "MZEE MWAKIKAGILE" ndio nani hapa JF? Kuna Member mwenye ID ya "MZEE MWAKIKAGILE" hapa JF?

Mkuu hiyo ni dalili ya wazi kwamba leo wadau wamekaba njia zote za kupitisha mipira, kila akitaka kupiga pasi anaona kuna mtu ameziba njia, sasa kilichobaki ni kurusha ngumi ili walau apate pa kuchomokea!! ha ha haaa-bahariaaaaaa.

Anyway, ukweli umedhihiri tusonge mbele.
 
Hilo halinihusu nafuatilia thread "Kuna harufu ya kujuana kwenye balozi zetu" nikitaka kujua kama ni pacha au la nitawauliza kwenye PM....not here....usibake thread....tafadhali sana

Fikra zako ni finyu sana, na hujui namna ya kuongea. Kumbuka kuwa kuchangia thread si kuingia tu na kuanza kupayuka, hoja hazijengwi namna hiyo, jaribu kujifunza kuangalia approach za watu ili upate labda kujifunza ni nini approach ya mdahalo ni nini "rapport" kama hujui ku "establish rapport" jifunze, usikurupuke.

Bado una mengi ya kujifunza na ikiwa unaingia JF unajifanya ndio unajuwa kila kitu, ujuwe wewe ni bado sana, hujajuwa ku "communicate" hata kidogo. Tazama ulichochangia na utazame wengine wanaelekea wapi, wakati hoja zinaendelea usikurupuke.
 
Well, people this is fun, vyama vyote vinanuka na undugu, isipokuwa Mleta mada amesema Uongo hakuna mtoto wa Mkapa ubalozi wowote Duniani. Tuwache majungu! - Le Mutuz
 
Mkuu hiyo ni dalili ya wazi kwamba leo wadau wamekaba njia zote za kupitisha mipira, kila akitaka kupiga pasi anaona kuna mtu ameziba njia, sasa kilichobaki ni kurusha ngumi ili walau apate pa kuchomokea!! ha ha haaa-bahariaaaaaa.

Anyway, ukweli umedhihiri tusonge mbele.

Ukiona mpaka mtu anajaribu kumkana dada yake, then he is ready kurusha ngumu regardless of what. He was trying contest factual information. Ndio maana hata juzi aliazisha thread akishauri kwenye Katiba Mpya kuwe na kipengele maalum kinachofuatilia safari za viongozi nje ya nchi na kwamba mikutano "Mikutano mingi wanayokwenda huko nje inaweza kuwakilishwa na Maofisa wa Balozi zetu zilizoko nje." Hapo kwenye red, you can see alikuwa anavutia wapi.
 
Well, people this is fun, vyama vyote vinanuka na undugu, isipokuwa Mleta mada amesema Uongo hakuna mtoto wa Mkapa ubalozi wowote Duniani. Tuwache majungu! - Le Mutuz

Wrong plus wrong does not make it right. Kwa vile "vyama vyote vinanuka na undugu" hailalishi kuwa na undugu kwenye ofisi za balozi. Halafu unaposema "hakuna mtoto wa Mkapa ubalozi wowote Duniani", unajua Mkapa ana watoto wangapi? Come on William. Mwanaume kama wewe unaweza kuwa na uhakika gani kuwa mwanaume mwingine kama Mkapa ana watoto wawili tuu?
 
MWAKIKAGILE ni Mzee mmoja yupo Michigan alikuja kusoma US in the 70s, mpaka leo hajawahi kurudi Bongo wala kuwasiliana na Familia yake, yeye yumo hapa JF kwa majina mengi ya bandia na amekuwa akinitukana kwa muda mrefu sasa kama leo akinihusisha na majina yasiyo nihusu ndio maana leo nimempa kamba yake mwenyewe na amejifunga nayo.

Maana ndugu zake wote wapo hapa ila walikuwa hawajui kuwa yupo hapa na ndiye anayewatukana na Details nyingi za ndani za familia Yake ni Msomi mkubwa sana lakini the way anavyo behave humu JF hasa kutukana ndugu zake huenda ana some serious ishus! Ha! Ha! MWAKIKAGILE nitukane tena na maneno ya Field Marshall na ndugu yako This is Mutuz Le Baharia On The Run! MERCI!
 
Katika hili inafahamika kwamba wewe na familia yako ni wanufaika, kwahiyo haishangazi kukuona ukianza kutokwa na mapovu badala ya kujibu hoja!
Na kwa uelewa wa kawaida kabisa na hata kwa mtu asiyeishi marekani kama wewe angeweza kuwa na majibu yanayoendana na mashaka ya mleta thread.
Kwa namna unavyohamisha mashambulizi kuelekea chadema ni dhahiri kwamba hao watoto wa vigogo wanaotajwa ni kweli kwamba walipata hizo kazi kwa kujuana na si kwa merits.
Na kwakuwa hii nchi ni yetu sote, hatuwezi kuacha kuhoji kila tutakapoona dalili za undugunization. Kama chadema wamebebana katika ubunge hiyo haiwezi kuhalalisha watoto wa wakubwa kubebwa bebwa kila mahali kuanzia BOT, Balozini, MFA, TRA, iKULU,CCM, Chadema na Kwingineko.

safi sana bora umempa ukweli anakurupuka tu huyu kila linaloibuka anaingiza CDM badala ya kujenga hoja.anashangaza sana huyu Malecela jr
 
To me uteuzi wa mabalozi ni kama uteuzi wa viti maalum vyote kwa ujumla huwa vinanichefua ukifuatiwa na uteuzi wa ma DC na MA RC
 
Udugunaizeshen ulimshinda Nyerere na kama haujafanyiwa kazi hautakwisha leo wala kesho. Watu waajiriwe kwa vigezo vya taaluma zao na kupasi "interviews" kihalali. Interview zisifanywe na wizara, idara au taasisi husika. Kampuni zinazo "specialize" mambo ya kuajiri, zipewe vigezo nazo ndio ziwe watahini wa waajiriwa. Na watapo ajiri mtu "incompetent" walipie gharama zote.[/QUOTE]

FaizaFoxy, nimekuwa nikisoma sana comments zako humu JF lakini nimekuwa nikiona hizo comments zinalalia sana kwenye UDINI, something which i HATE most in ma life, i am christian ( i think I'm purely christian) but i have been in many Mosques (one of them is Qaddafi Mosque in Uganda) like in Churches. I respect ALL PEOPLE OF ALL FAITH because i beleive in HUMANITY first RELIGION next
and i have hundreds of christian and muslim friends. I will NEVER criticise any person's religion in ma entire LIFE or in ma GRAVE.

Mtu anapo ku-CRITICISE MSIKILIZE SANA kuliko kumchukulia OTHERWISE............


Humu jamvini just a single word utaona next reply ni ya udini.............WHY? Tumefikia kweli mwisho wa kufikilia?
Nayasema haya kwa sababu leo umenikosha saaaaana Faiza. What u wrote today is what i beleive and have been telling many people, if we want this country (my country) DEVELOP kama Malyasia, Singapore, India, South Africa, Brazil etc

Tukitaka Tanzania iendelee tusifikilie sana vyama vya siasa (vyama hivyo iwe tu 20% ya mabadiliko tunayo yataka) 80% tufanye mabadiliko katika kuajiri right candidates for right jobs, isiwe mtu kapata kazi ila kazi ipate mtu. Interviews zifanyike kwa uwazi, mchujo ufanyike from A to Z ili tum-select the right person that fits the job. Siyo hiyo tabia ya undugunaizesheni yenye malengo ya kufichiana uozo unaofanyika katika sector zote za serikali na binafsi. Mfano Kenya wameanza baada ya Katiba yao mpya kama walivyompata AG wao and i beleive Kenya will never be the same again in Five years.
Leo ukiingia humu mawizarani na sector zingine za serikali utacheka tu,...............
 
Hakuna mtoto wa Mkapa Ubalozi wetu wowote Duniani Mkapa ana watoto Wawili Steve na Nico wapo Bongo, na hawapo Ubalozi wowote hapo Bongo Umekurupuka, nenda Bungeni uone Viongozi wa Chadema na ndugu zao wote ni Wabunge, Halafu uje utueleze hivi Chadema ilibidi Mwenyekiti lazima awe Mkwe wa Mtei tu? Hakukuwa na wengine? Wacheni kuchafua Majina ya watu. - William

walatini walikuwa na msemo " excusatio non petita,accusatio manifesta!" Malecela,nakuachia ukatafitue maana yake!!! Alichoandika Mpayukaji kina ukweli 150% personally I have been living in the western countries in the past 20yrs na nimewafahamu watanzania wengi wenye uhusiano wa karibu na vigogo wa CCM na serikali zilizopita na iliyoko madarakani hivi sasa ambao wanafanya kazi ktk balozi zetu nje hata bila ya kuwa na sifa, by the way do you know somebody NEEMA NGWILULUPI,born on Monday 11th of November of 1968??? Does the name tell you anything??? Nitaendelea kukurahisishia maana uwezo wako wakufikiri ni mdogo kiasi ambacho ambao hawakufahamu hawawezi kutegemea...Unamfahamu Weidi Mwasakafyuka ambaye alishakuwa balozi wetu France and then Nigeria?? Unamfahamu Mr. Brown Ngwilulupi??? na Balozi Francis Malambugi??? Waeleze wana JF hao watu ni akina nanani na Neema Ngwilulupi ni nani???

Neema Ngwilulupi alipata the so called DIV 5 (alipata Z-E-R-O) alipokuwa Loleza Sec. School - hana elimu yoyote na hana hata degree kama anavyowadanganya watu mitaani in short hana elimu yoyote!!! Mnafahamu huyo Neema ni nani na anafanya kazi gani??? NI SECRETARY WA TANZANIA MISSION TO THE UN na ndiye MKE WA W.J.MALECELA

My take!!
Ungekuwa na AKILI japo za kuendea chooni,topics kama hizi ungekuwa hauchangii hata kidogo - lakini Mungu amekunyima hizo akili si makosa yako!!!
 
Tatizo la undugunization halipo sehemu fulani tu Tanzania, ni tatizo sugu limeanza zamani, ukienda kwenye Wizara, Idara, Taasisi, Shirika hata NGO ambayo wakubwa ni wakabila fulani basi utafikiri kuwa Tanzania hakuna makabila mengine.

Hili ni tatizo sugu na lipo na siku hizi kuna trend mpya imeanza, toka yameanza haya makanisa ya kiajabu ajabu ya fungu la kumi, tunaona kuwa ukabila unachanganyika na kanisa lipi unasali ndio wanakuwa wengi, hii hususan kwenye mashirika na ma NGO ya nje. Yamelengwa kwa kuwa ndiyo yanayolipa zaidi na fungu la kumi linakuwa la uhakika. Hii haina utata.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom