Kuna haja ya watu wanaotaka kugombea ubunge kupimwa IQ zao, kwa Tanzania ndio nimeshudia watunga sheria wanatunga vitu visivyoeleweka

Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,199
1,346
*Mbunge* wa Tanzania akimalza muda wake anataka apewe *kiinua mgongo* chake chote kwa mkupuo na wamejiwekea utaratibu huo kisheria

Mbunge huyo huyo ametunga sheria kwamba *Mstaafu wa Tanzania* apewe 25% ya _*alichojikusanyia*_ kwa muda wake wote wa utumishi na 75% atalipwa kidogo kidogo kwa *miaka 12*.

Pia wanaenda mbali zaidi na kusema kuwa, kigezo cha mtu kugombea ubunge ni kujua kusoma na kuandika (la saba), dereva wake awe na cheti cha kidato cha nne(amefaulu). Mtu huyu huyu anaejua *kusoma na kuandika tu* (hana taaluma) anapewa jukumu la kutunga sheria, sheria hiyo inapelekwa kutafsiriwa na mtu mwenye *DEGREE*.
Siasa naiogopa sana.
 
Sasa nani mjinga kati yako wewe mpiga kura na mbuge mzigo. Unajua unapeleka bungeni mtu mzigo kisha baadae unalalama.
 
MIMI MPIGA KURA NITAFANYAJE KWANI IKIFIKA KARIBU NA UCHAGUZI MKE WANGU HUPEWA VITENGE NA MITANDIO YA RANGI KIJANI NA NJANO NA MIMI NAPEWA TSHIRT NA KOFIA RANGI HIYO INABIDI TUWAPIGIE KURA
 
Back
Top Bottom