Kuna haja ya Tundu Lissu kuanzisha chama cha siasa kwa masilahi mapana ya Taifa

Habari JF,

Hivi katika mazingira yalivyo sasa ni nani anaweza kusema CHADEMA ya Mbowe ni wapinzani? ACT Wazalendo ya Zitto ni wapinzani? Au CUF ya Lipumba ni wapinzani?

Ukweli ni kwamba tumebakiwa na wapinzani wachache kama kina Mbatia, Heche, Lema, Tundu Lissu etc, na katika hawa Tundu Lissu bado atabaki kama mpinzani mwenye ushawishi mkubwa.

Hivyo kuna haja kwa Tundu Lissu kukusanya nguvu kutoka kwa wapinzani tajwa hapo juu na watu kama kina Bashiru waunde chama ili kuiokoa nchi. 2025 chama kikitia nguvu ya kutosha hata kwa katiba ya sasa CCM inaweza toka.

Tanzania inahitaji akili na mawazo mapya, ni aibu miaka 60 baada ya uhuru bado tunashida za maji, umeme, afya, vyoo mashuleni nk; kwa Nchi yenye madini, bahari, mito, maziwa, utalii, eneo kubwa la kilimo nk.
kwanza kabisa tuambie nchi gani imeyamaliza hayo matatizo
 
Bora akae atulie uko uko chadema ila atengeneze vijana wapya wenye uchungu na wazalendo (cjui atawatoa wap) ambao atawasaidia wapate elimu ya uzalendo na mwishowe awatengenezee njia ya kuanzisha chama Cha siasa .

Ila c rahis kushindana na ccm maana wako tayari hata kuuwa chcht kinachowakwamisha ktk uchaguzi ila n weupee tu wasipotumia mamlaka zao..

Ngoja tuone..
 
Back
Top Bottom