Kuna haja ya Sports Pesa Cup? Walioshindwa kufuzu wanacheza na timu bora kuliko ile ya waliofuzu

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Povu Ruksa ila penye ukweli pasipindishwe na mnyonge hata mkitaka kumnyonga basi mpeni haki yake.

Hawa sports pesa kampuni ya kubeti walikuwa wanaandaa mashindano sports pesa super cup ambapo mshindi alikuwa anapata bahati ya kucheza na timu ya everton ambayo ina unafuu huko ligi kuu ya uingereza japo sio timu moto kama wale top 4 tunaowajua.

haya mashindano ya sports pesa super cup timu za kenya zimekuwa zikionesha uwezo mkubwa kitu kilichofanya washinde haya mashindano toka yaanze na hili lilifanya timu za Tanzania kama Simba, Mbao fc, Yanga na singida united kukosa bahati ya kucheza natimu ya everton ambayo ipo kwenye ligi kuu ya uingereza ambayo ina unafuu.

Sasa hiki kilichotokea majuzi sijui hata tukiitaje, kilichotokea hakina utofauti na kumpa mwanafunzi maswali ya mtihani uliovuja huku mwanafunzi hajui kuyafanya maswali kutokana na uzembe wa kutopenda kudanya maswali.

Mara paaap!!!! Tunasikia kwamba sport pesa wanaileta timu ambayo ina makombe ya uefa europa mengi kuliko timu nyingine kwa kubeba kombe hili mara tano, Pia ni timu ambayo imeshinda makombe la liga na hata kushinda super cup. Ukija kwa Everton ni timu ya kawaida tu ambayo labda kwa mbali ina heshima yake kombe la pembeni la FA cup.

Sports pesa walianza kwa kauli zao kwamba itaundwa timu yenye mchanganyiko wa simba na yanga ili kuikabili servilla, ikaanza mijadala ya pendekezo ya kwamba kuwe na mechi kati ya simba na yanga ili mshindi acheze na servilla ila hao sport pesa wakaja na kigezo kipya kwamba mshindi wa ligi kuu mwaka jana ambae ni simba ndio acheze na hao servilla:eek:

Ikumbukwe kwamba hapo Nyuma timu zilitia nguvu mno ili kuweza kushinda sports pesa super cup ili wakutane na timu ya everton, Sasa hili jambo la timu kuletewa timu kali mno kuliko ile ambayo washindi wa sport pesa cup wanaenda kucheza nayo ni kufanya mashindano yaonekane hayana hadhi tena.

Kwa hali hii endapo kigezo kitakuwa ni servilla kucheza na mshindi wa msimu uliopita basi hata hayo mashindano ya sports pesa cup timu zilizoshinda ligi kuu hazitahamasika kupigania taji kwa sababu timu watayoenda kucheza nayo ni ndogo kuliko sevilla

Pengine ingebidi timu ndogo kuzidi everton ndio itelezeshwe kuja kucheza na timu zetu hizi ambazo zilipata wakati mgumu sana kupambana na timu za kenya ambazo zilipigana kufa kupona kucheza na everton.
 
hivi simba imepata nafasi sababu sio ya kuwa bingwa wa vpl sababu ni ya kufika robo fainali ya sportpesa 2017,fainali 2018 na robo fainali 2019
 
  • Thanks
Reactions: Cyk
Back
Top Bottom