Kuna haja ya Serikali kutumia sera ya "Train-Retain" kwa wanufaika wa HESLB ili kupunguza "makali" tatizo la ukosefu wa ajira nchini

Amanito

JF-Expert Member
Nov 20, 2015
259
551
Salam Wakuu!

Kuna kitu nimekifikiria sijajua kitaalamu kama linawezekana hili suala kwa hapa kwetu Tanzania.

Kwa jinsi hali ilivyo sasa ambapo wanufaika wengi wa bodi ya mikopo wakihitimu huwa wanarudi mitaani kusubiri ajira ambazo huwa hawana uhakika nazo, ni muhimu sasa serikali ikaanzisha utaratibu ambao utatoa nafasi kwa mhitimu kuitumikia serikali kwa muda maalum mfano miaka miwili (2) kwa makubaliano maalum na kwa ujira wa kiwango cha chini ili kufidia deni lake la Bodi ya mikopo na kuwapa uzoefu wa kazi wahitimu wa vyuo vikuu.

Badala ya mtu kumaliza chuo na kukosa ajira kisha kukaa tu mtaani huku deni lake likizidi kuongezeka kwa riba na faini za ajabu ni heri mtu huyo atumike na serikali katika uzalishaji na utoaji wa huduma kwaajili ya kuongeza ufanisi serikalini.

Hii inaweza kuwa kama ni "Internship program" ambayo itakuwa inaratibiwa vizuri kisera na vyombo husika kama HESLB, wakala wa ajira TaESA, wizara mbalimbali na mashirika ya umma etc.

Ni mfumo kama wa JKT baada ya kupata mafunzo unalazimika kutumika National Services kwa muda fulani kisha unaweza kupata ajira ukiwa katika huu mfumo au ukakosa ajira na kurudi mtaani angalau ukiwa na skills za kazi na uzoefu.

Badala ya mtu kuingia mtaani direct akitokea shule kiasi kwamba hana uzoefu wowote ule, hii huwa ni changamoto sana kwa wahitimu kwakweli.

Mfumo huu pia unatumika na nchi za Ulaya na Canada kwa kubakisha wanafunzi waliowapa scholarship kwa kuwapa ajira za muda ili angalau walipe fadhila za kusomeshwa na serikali.

Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote ila inaweza kuweka vigezo ambavyo vitachagua baadhi ya wahitimu hasa wale ambao ni wanufaika wa bodi ya mikopo na vigezo vingine watakavyo ona inafaa.
 
Mkuu mimi sijawahi kusikia kama upo.. Na kama upo sidhani kama umewekwa utaratibu mzuri wa kuwezesha wahusika hasa wahitimu kushiriki kikamilifu katika hili suala..
 
Binafsi niliamua kuvimba mwenyewe kujilipia, sikutaka kutegemea HESLB, maana nilijua mwisho wa siku tutaanza kulaumiana,japa nimeteseka sana.
 
Yani kuna ma Hr wana roho Mbaya sana, kwanza wanakuona unafaidi sana unapopata ujuzi,
Yani anapoona unafanya kazi anaumia kinoma yani kwa nini unafanyakazi hapa utazani Ela unazopata mshahara wake unapungua , Mmoja wa Hr mwenye roho Mbaya ni Essau , namchukia huyu mwamba kanialibia mipango.

Ila inabidi serikali itunge sheria za kuwabana Hawa watu, wanajimilikisha mashirika ya uma kama ya kwao.

Note : Ila wakina Essau mpo wengi mwenye roho Mbaya anajijua yupo shirika gani? Ukiona una roho nzuri unajitoa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamsingizia ni hr wa tanesco mbeya, mtu safi namjua ndani nje. Kama ajila saizi wanatoa tamisemi yeye unataka afanyaje acha bifu za ajabu mkuu.

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ungejiajiri tuu achana na hizi sarakasi
Mkuu mimi pia nasapoti suala la kujiajiri ila katika mchakato huo wa kujiajiri huoni kama itakuwa vizuri mhitimu apitie kwanza katika sekta fulani afanye kazi ili kujua changamoto zilizopo katika mifumo ya utoaji huduma kisha akipata SKILLS za kutosha kuhusiana na taaluma yake..

Kwa mantiki hiyo hata suala la kujiajiri linakuwa rahisi zaidi kwasababu anakuwa na ABC za kujua mifumo yetu ina mapungufu gani na yeye kama mtaalamu wa fani fulani ni nini afanye kutumia hiyo fursa...
 
Yani kuna ma Hr wana roho Mbaya sana, kwanza wanakuona unafaidi sana unapopata ujuzi,
Yani anapoona unafanya kazi anaumia kinoma yani kwa nini unafanyakazi hapa utazani Ela unazopata mshahara wake unapungua , Mmoja wa Hr mwenye roho Mbaya ni Essau , namchukia huyu mwamba kanialibia mipango.

Ila inabidi serikali itunge sheria za kuwabana Hawa watu, wanajimilikisha mashirika ya uma kama ya kwao.

Note : Ila wakina Essau mpo wengi mwenye roho Mbaya anajijua yupo shirika gani? Ukiona una roho nzuri unajitoa .

Sent using Jamii Forums mobile app
Kukiwa na sera nzuri, sheria na utaratibu mzuri hata hao HRs sidhani kama watakuwa na la kufanya ila itakuwa ni suala la kufuata utaratibu tu..

Leo hii wanafunzi wa kada mbalimbali za afya ni wanufaika wa huu mfumo wa kupata Internship kabla ya kurudi kitaani.. Na wengi umewasaidia kwa namna fulani.

Sasa ni vizuri tukautumia hata kwa kada zingine na kuuboresha katika namna ambayo itakuwa inawanufaisha wote yaani wahitimu na serikali..
 
Ulijua atumjui acha izo kaka haipendezi kumchafua mtu wakati hana kosa sio poa unaweza kuchukulia kawaida ila kuna mamilioni ya watu wanaona post yako wanamchukuliaje acha chuki binafsi muombe mungu akufungulie milango na ww, ukiona anafaidi na ww kasome hr

Sent from my Infinix X624B using JamiiForums mobile app
Jambo usilo lijua ni kama usiku wa giza? Roho Mbaya haijengi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom