Amanito
JF-Expert Member
- Nov 20, 2015
- 259
- 551
Salam Wakuu!
Kuna kitu nimekifikiria sijajua kitaalamu kama linawezekana hili suala kwa hapa kwetu Tanzania.
Kwa jinsi hali ilivyo sasa ambapo wanufaika wengi wa bodi ya mikopo wakihitimu huwa wanarudi mitaani kusubiri ajira ambazo huwa hawana uhakika nazo, ni muhimu sasa serikali ikaanzisha utaratibu ambao utatoa nafasi kwa mhitimu kuitumikia serikali kwa muda maalum mfano miaka miwili (2) kwa makubaliano maalum na kwa ujira wa kiwango cha chini ili kufidia deni lake la Bodi ya mikopo na kuwapa uzoefu wa kazi wahitimu wa vyuo vikuu.
Badala ya mtu kumaliza chuo na kukosa ajira kisha kukaa tu mtaani huku deni lake likizidi kuongezeka kwa riba na faini za ajabu ni heri mtu huyo atumike na serikali katika uzalishaji na utoaji wa huduma kwaajili ya kuongeza ufanisi serikalini.
Hii inaweza kuwa kama ni "Internship program" ambayo itakuwa inaratibiwa vizuri kisera na vyombo husika kama HESLB, wakala wa ajira TaESA, wizara mbalimbali na mashirika ya umma etc.
Ni mfumo kama wa JKT baada ya kupata mafunzo unalazimika kutumika National Services kwa muda fulani kisha unaweza kupata ajira ukiwa katika huu mfumo au ukakosa ajira na kurudi mtaani angalau ukiwa na skills za kazi na uzoefu.
Badala ya mtu kuingia mtaani direct akitokea shule kiasi kwamba hana uzoefu wowote ule, hii huwa ni changamoto sana kwa wahitimu kwakweli.
Mfumo huu pia unatumika na nchi za Ulaya na Canada kwa kubakisha wanafunzi waliowapa scholarship kwa kuwapa ajira za muda ili angalau walipe fadhila za kusomeshwa na serikali.
Serikali haiwezi kuajiri wahitimu wote ila inaweza kuweka vigezo ambavyo vitachagua baadhi ya wahitimu hasa wale ambao ni wanufaika wa bodi ya mikopo na vigezo vingine watakavyo ona inafaa.