Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.
Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Ninaomba hii isichukuliwe kama campaign ya serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 kwa maana dada zetu barmaids ni wengi hivyo wanaweza kuipa kura nyingi sana CCM. Mimi nimeandika hivi kama Mtanzania mwenye mapenzi mema na huruma kwa dada zangu na sio kama mfuasi wa chama cha siasa.
Kwa wafanyakazi wa jinsia ya kike wenye mazingira magumu ya kazi ni hawa akina dada kwa maana wana deal na walevi (watu wasio katika hali za kawaida za akili) sasa Kwanini wamiliki wa Bars wanashindwa kuwakatia bima ya afya CHF dada zetu Barmaids 30,000/= tu mwaka mzima? Serikali iwabane hawa jamaa.
Unakuta dada wa watu mshahara wenyewe 80,000 mwezi mzima, au wengine wanalipwa kulingana na idadi ya vinywaji wanavyouza, mara wateja wamshike shike mwili wake wana mdhalilisha hadharani, kazi anafanya zaidi ya masaa 8 kwa siku, sehemu ya kulala hana. Unakuta kina dada 9 wote wanalazwa kwenye chumba kimoja tu (Ghetto), hapelekewi pesa zake WCF wala NSSF.
Kwa mazingira magumu ya kazi kama haya mtu anakosa roho ya utu ya kumkatia mwezie bima ya shilingi 30,000 tu mwaka mzima? Kweli kabisa? Really?
OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.