Kuna haja ya Serikali kupitia wakuu wa wilaya na mikoa kuwabana wamiliki wa baa ili dada zetu wahudumu wapewe kadi za bima ya afya ya CHF?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Messages
3,541
Points
2,000

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2012
3,541 2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ninaomba hii isichukuliwe kama campaign ya serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 kwa maana dada zetu barmaids ni wengi hivyo wanaweza kuipa kura nyingi sana CCM. Mimi nimeandika hivi kama Mtanzania mwenye mapenzi mema na huruma kwa dada zangu na sio kama mfuasi wa chama cha siasa.

Kwa wafanyakazi wa jinsia ya kike wenye mazingira magumu ya kazi ni hawa akina dada kwa maana wana deal na walevi (watu wasio katika hali za kawaida za akili) sasa Kwanini wamiliki wa Bars wanashindwa kuwakatia bima ya afya CHF dada zetu Barmaids 30,000/= tu mwaka mzima? Serikali iwabane hawa jamaa.

Unakuta dada wa watu mshahara wenyewe 80,000 mwezi mzima, au wengine wanalipwa kulingana na idadi ya vinywaji wanavyouza, mara wateja wamshike shike mwili wake wana mdhalilisha hadharani, kazi anafanya zaidi ya masaa 8 kwa siku, sehemu ya kulala hana. Unakuta kina dada 9 wote wanalazwa kwenye chumba kimoja tu (Ghetto), hapelekewi pesa zake WCF wala NSSF.

Kwa mazingira magumu ya kazi kama haya mtu anakosa roho ya utu ya kumkatia mwezie bima ya shilingi 30,000 tu mwaka mzima? Kweli kabisa? Really?

OUR MOTTO:
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Messages
3,541
Points
2,000

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2012
3,541 2,000
Ongezea na wafanyakazi wa ndani majumbani,mafundi gereji,wafanyakazi wa mahotelin,makondakta wa magari,wafanya usafi barabarani,wafanyakazi wa saluni,n.k
Ishauri serikali kila mtu awe na bima ya afya.
Katika hao woooote uliowataja, barmaid ndiye mwenye mazingira magumu sana na hatarishi ya kazi.
 
emanuellyimo

Member
Joined
Aug 14, 2015
Messages
22
Points
75

emanuellyimo

Member
Joined Aug 14, 2015
22 75
Hakuna Watu wanaofanya Kazi kwenye mazingira magumu kama Mafundi gereji na wachimbaji wa Madini hao Wafanyakazi wa bar wanapewa vyumba wanapewa chakula na bado wanauwezo mkubwa wa kupata tuchenji chenji pindi wakihudumia vizuri Wateja nikushauri jaribu kutembelea mabaamaids ata kumi uone jinsi waishivyo kifahari kwenye vyumba vyao vya uko Uswahilini walikopanga Mwisho tuache kubebesha mizigo wamiliki wa bar maana nawao wanalipa Kodi Serikalini sasa izo Familia zanini?kwao?
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Messages
3,541
Points
2,000

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2012
3,541 2,000
Hakuna Watu wanaofanya Kazi kwenye mazingira magumu kama Mafundi gereji na wachimbaji wa Madini hao Wafanyakazi
Mkuu, ninapoongelea barmaid ninaongelea mwanamke na kaa ukijua kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu sana asiyehitaji misukosuko na udhalilishaji kama ambavyo walevi wanawafanyia hawa dada zetu.

Mafundi gereji wanaiba sana spares za magari pamoja na kuwapiga wamiliki wa magari bei za juu za matengenezo.

Hao watu wa madini ndio kabisaaaa wanaitwa wazee wa matanuzi, wazee wa kula bata nenda Arusha uone pesa walizonazo wachimba madini.
 
Patiee

Senior Member
Joined
Sep 20, 2018
Messages
157
Points
500

Patiee

Senior Member
Joined Sep 20, 2018
157 500
Jifunze kuwa muungwana. Pungunza ku panic. Punguza matusi
Infantry soldier kijana mdogo , umri miaka (23_26) , neno bullshit sio kipimo cha uungwana.Infact hakuna kitu kinaitwa "tusi",hiyo ni namna unavyopokea na kutafsiri ulichoambiwa.

Kila la kheri katika kuishauri serikali.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Messages
2,834
Points
2,000

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2019
2,834 2,000
Yaani mhudumu wa bar auze kwenye bar moja kwa mwaka mzima! Sasa si hiyo bara itafungwa kwa kukimbiwa na wateja. Hao viumbe ni kama makunguru! Huwa hawafugiki.
 
Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Messages
1,139
Points
2,000

Tape measure

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2015
1,139 2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ninaomba hii isichukuliwe kama campaign ya serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 kwa maana dada zetu barmaids ni wengi hivyo wanaweza kuipa kura nyingi sana CCM. Mimi nimeandika hivi kama Mtanzania mwenye mapenzi mema na huruma kwa dada zangu na sio kama mfuasi wa chama cha siasa.

Kwa wafanyakazi wa jinsia ya kike wenye mazingira magumu ya kazi ni hawa akina dada kwa maana wana deal na walevi (watu wasio katika hali za kawaida za akili) sasa Kwanini wamiliki wa Bars wanashindwa kuwakatia bima ya afya CHF dada zetu Barmaids 30,000/= tu mwaka mzima? Serikali iwabane hawa jamaa.

Unakuta dada wa watu mshahara wenyewe 80,000 mwezi mzima, au wengine wanalipwa kulingana na idadi ya vinywaji wanavyouza, mara wateja wamshike shike mwili wake wana mdhalilisha hadharani, kazi anafanya zaidi ya masaa 8 kwa siku, sehemu ya kulala hana. Unakuta kina dada 9 wote wanalazwa kwenye chumba kimoja tu (Ghetto), hapelekewi pesa zake WCF wala NSSF.

Kwa mazingira magumu ya kazi kama haya mtu anakosa roho ya utu ya kumkatia mwezie bima ya shilingi 30,000 tu mwaka mzima? Kweli kabisa? Really?

OUR MOTTO:
KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Wewe ni mkurupukaji mzuri unaehisi unaweza vingi kuliko wengine ungejua maana ya mtu kufanya kazi katika mazingira magumu ama hatarishi usingemtaja barmaids?

Hujui undani wa hiyo kazi kwanza wahudumu wengi huwa ni ngumu kufanya kazi eneo moja zaidi ya miezi 3 sio watu wakutegemea na huwezi kuingia nao mkataba wa kazi muda wowote anaweza kutoa udhuru na kutokomea kwingine ama kuolewa kwa muda.

Pia ungejua faida inayopatikana kwa kreti moja ya bia na anachopew mhudumu anapouza kreti moja + garama za kodi+ uendeshaji+ kuwahudumia. Ungejua kwa nini mchicha hautakaa ukue kufikia mbuyu japokuwa mbuyu ulianza kama mchicha
 
Forum statistics

Threads 1,390,030
Members 528,080
Posts 34,041,466
Top